Intelligence Justice
JF-Expert Member
- Oct 23, 2020
- 3,443
- 4,006
Ndg wana JF salaam? Nimelazimika kuja hapa kuweka jambo hili sawa. Nimeona uzi unaoongelea kuwa mimi na mhe Nchimbi tumewashitaki vijana hao waliojitaja kwa kuingilia mawasiliano. Naomba kuweka wazi kuwa 1) Sijawahi kuwasiliana na mhe Nchimbi kwa E mail hata siku moja tangu nizaliwe. 2) Sijapeleka lalamiko la mambo hayo polisi wala vyombo vyovyote vya dola wala vya habari 3) E mail ilibandikwa ikionesha mimi nawasiliana na Nchimbi wala sio e mail yangu wala haijawahi kuwa e mail yangu. 4) Sikuwa hata na sababu ya kuwasiliana na Mhe Nchimbi kwa E mail kwakuwa muda mwingi tuko wote bungeni, kwenye vikao vya chama na mjini. Inawezekana ni kweli vijana hawa wameitwa polisi, basi kama ndivyo, watakuwa wameitwa kwa kutengeneza e mail kwa majina ya viongozi, kutunga ujumbe wao na kutengeneza kama vile viongozi wamewasiliana na kuusambaza kwa lengo baya la kutaka kuchafua taswira za viongozi mbele ya umma. Hii ni tabia mbaya kabisa na vijana wa aina hii ni mizigo kwa Taifa. Naunga mkono polisi wafuatilie uzushi na ujinga huo wa watu kutengeneza e mail bandia, mawasiliano feki na kusambaza kama ndio mawasiliano halali ili umma upokee matope waliopanga kupakazia viongozi. e mail yangu iko kika mahali kwenye business card zangu. Nalaani kitendo chao cha kubandika e mail batili, mawasiliano batili na kusambaza kwenye mitandao, nalaani pia kwa kutokuwa wakweli kama wameitwa kwa kuandaa e mail feki na mawasiliano feki wanakuja huku kuripoti kuwa wameingilia mawasiliano. yapi? Sio e mail yangu, wala sijawahi kuwasiliana na Nchimbi kwa e mail. E mail yangu inafanya academic issues, nawasiliana na supp wangu wa PhD na wanazuoni wengine kwa academic issues. Ben, look at you? MAJIBU ya BEN SAANANE
Kama hiki ndicho kilichotokea mwaka Dec 2013 kati ya Mr Clean na BeanSaa8 basi ni dhahiri JPM alisingiziwa kumpoteza kumbe wapo waliotumia mwanya kufanya yao ili alaumiwe mnamo mwaka Nov 2017!!!Ndg wana JF salaam?
Nimelazimika kuja hapa kuweka jambo hili sawa. Nimeona uzi unaoongelea kuwa mimi na mhe Nchimbi tumewashitaki vijana hao waliojitaja kwa kuingilia mawasiliano. Naomba kuweka wazi kuwa
1) Sijawahi kuwasiliana na mhe Nchimbi kwa E mail hata siku moja tangu nizaliwe.
2) Sijapeleka lalamiko la mambo hayo polisi wala vyombo vyovyote vya dola wala vya habari
3) E mail ilibandikwa ikionesha mimi nawasiliana na Nchimbi wala sio e mail yangu wala haijawahi kuwa e mail yangu.
4) Sikuwa hata na sababu ya kuwasiliana na Mhe Nchimbi kwa E mail kwakuwa muda mwingi tuko wote bungeni, kwenye vikao vya chama na mjini.
Inawezekana ni kweli vijana hawa wameitwa polisi, basi kama ndivyo, watakuwa wameitwa kwa kutengeneza e mail kwa majina ya viongozi, kutunga ujumbe wao na kutengeneza kama vile viongozi wamewasiliana na kuusambaza kwa lengo baya la kutaka kuchafua taswira za viongozi mbele ya umma. Hii ni tabia mbaya kabisa na vijana wa aina hii ni mizigo kwa Taifa.
Naunga mkono polisi wafuatilie uzushi na ujinga huo wa watu kutengeneza e mail bandia, mawasiliano feki na kusambaza kama ndio mawasiliano halali ili umma upokee matope waliopanga kupakazia viongozi. e mail yangu iko kika mahali kwenye business card zangu.
Nalaani kitendo chao cha kubandika e mail batili, mawasiliano batili na kusambaza kwenye mitandao, nalaani pia kwa kutokuwa wakweli kama wameitwa kwa kuandaa e mail feki na mawasiliano feki wanakuja huku kuripoti kuwa wameingilia mawasiliano. yapi? Sio e mail yangu, wala sijawahi kuwasiliana na Nchimbi kwa e mail. E mail yangu inafanya academic issues, nawasiliana na supp wangu wa PhD na wanazuoni wengine kwa academic issues.
Ben, look at you?
MAJIBU ya BEN SAANANE