Mwigulu umewadanganya Wastaafu, Bunge na Rais. Laana ya wazee mtaiona

Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2018
Posts
861
Reaction score
2,515
Leo mkijifanya mnasherehekea kwa mbwembwe na ukwasi mkubwa kumbukumbu ya mashujaa, nimekaa hapa na askari mstaafu wa JWTZ aliyeishia cheo cha Staff Sargent na alikatikia mguu akiwa vitani Uganda 1979 na mzee huyu analipwa pension na Hazina shs 100,000/ kwa mwezi.

Hawa ndio wastaafu ambao baada ya Mwigulu kubanwa Bungeni alikiri kuwa kweli pension ya laki moja ni aibu kuwalipa na hiyo laki iliwekwa wakati wa Kikwete na ameunda tume kuangalia uwezekano lazima ipande walao ilingane na Zanzibar.

Leo wazee wamelipwa tena katika siku yao ya mashujaa lakini kumbe ni UONGO MTUPU. Ajabu ni kuwa hata Rais Samia sio kuwa hajui hayo, anajua ila naye anayadharau kuwa watafanya nini hawa wazee?

Mnasahau hadhi na heshima iliyopo sasa ni zao la hawa wastaafu sio wanajeshi tuu bali wote waliotumia ujana wao kuitumikia nchi na kuilinda. mwigulu Nchemba nakuambia ulichofanya kuwadanganya hawa wazee HAKIKA KITARUDI KWAKO SOON.

Wazee wanaolipwa na Hazina directly kwanza wamebaki wangapi? Wako wachache sana walio hai hadi sasa na uwezo wa kuhamia Burundi hawana kama upendavyo wewe na kiburi chako.
 
Wale wazee wanaolipwa na Hazina laki moja kwa mwezi kama pension huku mkiwaahidi kuwa mmeona kiwango hicho ni aibu kuwalipa wakati wazee wale wengine ni vilema kwa kuipigania nchi, madaktari waliowahi kuokoa maisha yenu utotoni na watumishi wengine waaminifu na ahadi hakuitimiza.
Amini amini nawaambia kwa vile baba na mama zenu wale mlitoa ahadi kuwawaongezea na mmedharau kwa vile "hawana cha kuwafanya" mtaona utawala wenu hautakaa utulie na mwisho lipo lisilo jema laweza kuwafata kokote mliko.
 
Kuna watoto wa hawa wanaotutesa wananchi, , kuna siku watalipa kwa niaba ya wazazi wao maana wanatutesa kunufaisha watoto wao
 
Wale wazee wanaolipwa na Hazina laki moja kwa mwezi kama pension huku mkiwaahidi kuwa mmeona kiwango hicho ni aibu kuwalipa wakati wazee wale wengine ni vilema kwa kuipigania nchi, madaktari waliowahi kuokoa maisha yenu utotoni na watumishi wengine waaminifu na ahadi hakuitimiza.
Amini amini nawaambia kwa vile baba na mama zenu wale mlitoa ahadi kuwawaongezea na mmedharau kwa vile "hawana cha kuwafanya" mtaona utawala wenu hautakaa utulie na mwisho lipo lisilo jema laweza kuwafata kokote mliko.
Naunga mkono hoja karma is real "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili Hapa Duniani!, Unahukumiwa kwa Matendo Yako!
P
 
Imagine Col mstaafu wa miaka ile aliyepigana vita Msumbiji na Uganda leo hii anasotea ka pension ka laki moja toka hazina na serikali haioni Soni wala huruma maana wao wameshiba za kuiba na kama wana wazee wao huko hawapati shida wao watawapa zile waibazo.
 
Hao wazee si ndo walijifanya ccm na wao damu damu kipind wapo vijana.........

Fuga mbuzi utmla mjuzi ila fisi ipo siku atakufilisi...........
Kumbuka hawa wazee ni wale waliostaafu 1997 kurudi nyuma, na CCM ya wakati ule sio hii ya sasa.
Hata hiyo laki waliongezewa na JK toka 50k na hakuna tena anayefuatilia ile sheria pension isemayo lazima iwe percent ngapi ya mishahara.
Wao wanakumbuka kuwalipa viongozi 80% mishahara pamoja na wenzi wao lakini wale waliokuwa wanalala kwenye mahandaki kule Kyaka na Mutukula nani anajali?
 
Imagine Col mstaafu wa miaka ile aliyepigana vita Msumbiji na Uganda leo hii anasotea ka pension ka laki moja toka hazina na serikali haioni Soni wala huruma maana wao wameshiba za kuiba na kama wana wazee wao huko hawapati shida wao watawapa zile waibazo.
Acha walipwe hizo laki kwakuwa hawana Akili wanatumiwa na Serikali kutisha wananchi na kuvunja Katiba,hawachukui hatua yoyote
 
Hatuwez na mess na watu waliompinga King kambona kutaka kuleta changes ndani CCM.........

We remember u ...the king Kambona.........
 
Imagine Col mstaafu wa miaka ile aliyepigana vita Msumbiji na Uganda leo hii anasotea ka pension ka laki moja toka hazina na serikali haioni Soni wala huruma maana wao wameshiba za kuiba na kama wana wazee wao huko hawapati shida wao watawapa zile waibazo.
Wakati kila siku wanasema serikali haina fedha huku wananunua mashangingi ya mil 600 na kujilipa mishahara minono
 
Imagine Col mstaafu wa miaka ile aliyepigana vita Msumbiji na Uganda leo hii anasotea ka pension ka laki moja toka hazina na serikali haioni Soni wala huruma maana wao wameshiba za kuiba na kama wana wazee wao huko hawapati shida wao watawapa zile waibazo.
Kwani nao SI ni wastaafu?

Kwanini RAIS mstaafu alipwe pensheni nusu ya mshahara wa RAIS aliyepo madarakani,

Sasa nawao kwanini nao wasilipwe pensheni nusu ya mshahara wa Col aliyepo madarakani Sasa?
 
Hii serekali sijui wanapigaje hesabu zao. Kuna mdau ametoa mfano wa kanali mstaafu aisee ni majanga haswa. Na ndio maana wanakufaga mapema hawa watu. Na shida ni kwamba kanali aliyestaafu 1997 anapata laki moja pensheni na aliyestaafu 2023 anapata milioni na ushehe! Sasa unajiuliza hawa wamestaafu na cheo sawa na wanaingia maduka Yale Yale mtaani na ukipima zaidi hawa wa zamani ndio walikuwa waadilfu haswaa!

Shida sana yaani.

Kuna kanali mmoja namjua masikini hadi huruma. Kapiganisha vita ya Uganda, kapigana ushelisheli, kapigana msumbiji full battle, kaseti miundo mbinu na systems kibao jeshini na sasa hivi anasota balaa mtaani
 
Namkumbuka Kanali wangu wa 841kj miaka hiyo ya early 90s,sijui maskini atakuwa yu hali gani sahizi!
 
Hii serekali sijui wanapigaje hesabu zao. Kuna mdau ametoa mfano wa kanali mstaafu aisee ni majanga haswa. Na ndio maana wanakufaga mapema hawa watu. Na shida ni kwamba kanali aliyestaafu 1997 anapata laki moja pensheni na aliyestaafu 2023 anapata milioni na ushehe! Sasa unajiuliza hawa wamestaafu na cheo sawa na wanaingia maduka Yale Yale mtaani na ukipima zaidi hawa wa zamani ndio walikuwa waadilfu haswaa!

Shida sana yaani.

Kuna kanali mmoja namjua masikini hadi huruma. Kapiganisha vita ya Uganda, kapigana ushelisheli, kapigana msumbiji full battle, kaseti miundo mbinu na systems kibao jeshini na sasa hivi anasota balaa mtaani
mwigulu. Soma hii labda utaelewa na kujua kuwa ile lugha ya kuwaambia raia wakiona magumu waende Burundi ilikuwa ni lugha isiyofaa!
 
Back
Top Bottom