Hii serekali sijui wanapigaje hesabu zao. Kuna mdau ametoa mfano wa kanali mstaafu aisee ni majanga haswa. Na ndio maana wanakufaga mapema hawa watu. Na shida ni kwamba kanali aliyestaafu 1997 anapata laki moja pensheni na aliyestaafu 2023 anapata milioni na ushehe! Sasa unajiuliza hawa wamestaafu na cheo sawa na wanaingia maduka Yale Yale mtaani na ukipima zaidi hawa wa zamani ndio walikuwa waadilfu haswaa!
Shida sana yaani.
Kuna kanali mmoja namjua masikini hadi huruma. Kapiganisha vita ya Uganda, kapigana ushelisheli, kapigana msumbiji full battle, kaseti miundo mbinu na systems kibao jeshini na sasa hivi anasota balaa mtaani