Niendelee kuwaelekeza; mmepewa dhamana, na kwenye barua haujandikiwa inaisha lini, endelea na kazi. Na kwa kweli wale wanaosubiri PDF na wale wanaosubiri mkeka tutawatoa, lakini wale wanaofanya kazi wataendelea na kazi kwa sababu tunataka wananchi wapate huduma zilizo bora.
Kwani nielekeze taasisi zetu zinazofuatilia mienendo ya viongozi; tubainishieni wale wanaosubiri mkeka, wale wanaosubiri PDF tuwatoe ili tuwaweke watu wanaotaka kufanya kazi. Hatutaki shughuli za ofisi za umma zisimame kwa sababu kuna watu wanasubiri uteuzi. Haya ni mambo ya ajabu.
Hivi tungekuwa tunasubiri... wote tunajua kuna kifo, hivi tungekuwa tunasubiri kufa kuna mtu angefanya kazi? Unasubirije uteuzi na una jukumu umepewa la kufanya?
Naasisitiza tena; swala la teuzi, tena teuzi zinazofanyika kwa 'pleasure' ya anayeteua zisisubiriwe. Usisubiri, tuendelee na kazi. Watu waendelee na kazi. Tunataka watu wakimbie mchakamchaka kuhudumia Watanzania. Na wale ambao hawatasikiliza maelekezo haya, kwa kweli watakuwa wameshajitambulisha kuwa wamechoka au hawastahili kuendelea kuwa maofisini.
Viongozi na watendaji katika kila ngazi wasimamie na kutekeleza kikamilifu maagizo na maelekezo mbalimbali yanayotolewa na viongozi wa kitaifa ikiwemo kutatua kero za wananchi, ikiwemo kuwasikiliza wananchi, ikiwemo kusimamia miradi ya maendeleo. Haya ni majukumu ya kila siku.
Na watenge siku za kusikiliza, watenge siku za kufuatilia miradi, utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Taasisi zote zinazotoa huduma watenge muda wa kutatua kero wananchi wanazozipata kupitia huduma wanazozitoa."