Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Wakuu Kwema!
Vijana katika utafutaji ni vizuri kuelekezana ili kufanya kazi zetu zizidi kuwa na manufaa. Katika hilo, nimeona nimshauri na kumuelekeza Ndugu Mwijaku kuwa aache Kushika Mikono wake za watu anapoendesha kipindi chake yeye na Ndugu Soudy.
Hii tabia anaweza akaiona ni yakawaida lakini Kwa upande mwingine inaathiri kazi yake hasa Kwa Watazamaji, pia hata Kwa Wale anaowahoji.
Mwijaku unapomhoji mtu hasa mwenye jinsia ya kike, haupaswi kumshika Mkono, labda iwe ni salamu tu.
Lakini wewe, unawang'ang'ania Wadada wa watu licha ya wao kujaribu kujinasua kwenye mikono yako.
Haipendezi, na kisaikolojia mtu anayeongea huku anamshika mtu mwingine ni kwamba anatumia nguvu kumshawishi.
Lakini pia, Kisaikolojia, Mtu anapoongea huku akipendelea kutumia mikono yake kumshika mtu wa jinsia nyingine wakati wa mazungumzo inaashiria anaongozwa na hisia za mapenzi zaidi.
Kwa mwanaume, ni kwamba mtu huyo anapenda wanawake, na msukumo wake wa kihisia umezidi kupitiliza mpaka anashindwa kujizuia ndio maana anaongea huku akitumia mikono kumshika mwanamke.
Mwijaku, kipindi chako kinaweza kikawa ni kizuri kwani Kwa jamii yetu ya kitanzania kipo relevant kutokana na kuwa Watanzania wengi wanapenda kujua habari za watu wengine. Lakini embu fanyia marekebisho kidogo kwenye suala la uendeshaji wa kipindi, usimshike mtu hasa WA jinsia nyingine iwe aliyeolewa au asiyeolewa.
Soudybrown yeye anajitahidi Kwa nafasi yake. Wewe unachoharibu ni kipengele kimoja nilichokitaja, usishike shike wanawake za watu Mikono.
Ni ushauri tuu!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro