Mnapojadili hii mada wekeni kwenye mbongo then maneno Great thinkers ; jukwaa limeandaliwa kwa ajili ya kujadili hoja siyo kusifu na kupeana moyo.
Kama huna uwezo wakufahamu nafasi ya bilioni moja kwenye ujenzi usijitutumue kujadili kwa sababu tu unataka kusema; katika ujenzi Ile nyumba ya Mwijaku haina thamani ya bilioni moja na milioni mia tatu.
Lakini kwa upande wa pili hoja hapa siyo thamani ya nyumba, ni kiwanja na eneo alipojenga. Tukubali kwamba huyu kakosea kujenga, alipaswa kujenga nyumba kwenye eneo ambalo limepimwa na lina nafasi ya kupata oxygen.
Lakini pia ifahamike hapa hatupo kumshauri Mwijaku, tupo kuwashauri wengine wanaotamani kujenga.....tunawafumbua macho.
Jambo jingine ambalo wasanii wanapaswa kulizingatia kwa huko tuendako ni utajiri unaoendana na uwezo wa kulipa kodi. Mwijaku angetamka 1.3 bilioni kwenye nchi zilizoendelea hoja ingekuwa anapata wapi hizi fedha? Analipa kodi kutokana na faida ya mapato yake? Kibongo bongo hakuna mtu anayejali analysis ya kodi za nchi na ndiyo maana hatuna tatizo na kutaja figure kubwa.
Kwa wale tunaopanga kujenga lazima tujione kwenye nafasi hiyo. Wapo wanasiasa wengi na watumishi wa umma wamekimbia majumba yao na makazi yao baada ya kuteuliwa kwa sababu walishindwa kujipanga wajenge wapi kabla yakupewa madaraka.
Tununue maviwanja siyo viwanja
Huu uzi unazungumzia kujenga nini mzee baba na wewe unaniuliza nini?Amejenga nini?
Inakufikrisha wapi mkuu?Hii avatar yako huwa inanifikirisha mbali sana
Kwahyo hii yumba ndo ya billion 1 na million 300?Tembea ndugu yangu ukijifungia ndani utabishana na kila anaekupa taarifa...
Kama unataka nikuuzie lets talkKiko wapi hicho kiwanja😂🤣😀
Nakuchek mkuuKiko wapi?Kama unakichukia nnaomba uniuzie[emoji120]
Ipo
Ya Mwijaku ni 1.2 Bilioni na imejengwa kwa miezi kumi tu.....
Sukumizia na picha au unataka tuaminije?
Kama yeye kaanza na wenzake watajiongeza.Watanzania tunapaswa kubadili mawazo na fikra zetu hasa katika kufukia fedha kwenye ujenzi. Tuna watu wengi wanakosea kujenga kwa kukosa mawazo sahihi au exposure. Tafsi ya nyumba siyo mpangilio wa tofali bali ni muunganiko wa ramani na mazingira ya nje.
Viwanja vya masaki na osterbay vinaweza kuwa kielelezo cha fikra za ujenzi zinavyotakiwa kuwa. Alichofanya mwijaku na kampuni aliyowapa kazi ni aibu kwa karne hii.
Unapoweka malengo yakujenga nyumba hasa ghorofa unapaswa kuanza kuwaza kiwanja, eneo kiwanja kilipo na majirani wanaokuzunguka.
Unapotenga bilion moja ya ujenzi tunategemea kiwanja kitengeewe si chini ya milioni mia na hamsini endapo unataka kupata kiwanja mjini. Jengo la bilioni moja kibongo bongo linapaswa kujengwa kwenye eneo la heka moja endapo utajenga kigamboni ambapo maeneo ni makubwa.
Waliomshauri na kumjengea Mwijaku ndio washauri wa NHC, ambao wanajenga nyumba Tanzania kwenye kiwanja cha Sqmt 200 au 400 kwenye jiji kama Dodoma ambalo linakuwa . Poverty mentality ya wataalam wa ardhi wa nchi imepelekea watu kujenga kwa gharama kubwa lakini hawana uwezo wakupaki magari ishirini au kuwaalika marafiki nyumbani. Unakuwa na nyumba kama ya mwijaku lakini ukialika marafiki mia kuja kwako unalazimika ukatafute ukumbi. Leo Mwijaku akitazama chini akiwa ghorofani anawachungulia majirani.
Nyumba kama ile ingejengwa kwenye eneo sahihi hata wafanyakazi wenzake wangetuonyesha garden ya nje na wangepiga picha hata mandhari ya kwenda kwa huyu mjuba.
Nakubali kwamba tunanunua viwanja tukiwa hatujui tunajenga nini ila tunapochora ramani ya nyumba kama ile tutafute kiwanja. Alishindwa nini kwenda kujenga mbweni huko au bagamoyo ?
Nampongeza na niwapongeze wote wenye maono kama yake ila tubadili fikra tuje na maeneo ya uzunguni ambapo tukitaka kutembelea tunakuta miundombinu hata ya usalama ipo sawa.
Povu lazima
Unaweza ukawa upo sahihi ila kutokana na kupanda kwa vifaa vya Ujenzi nyumba zinatofautiana thamani kama walijenga vipindi tofauti Mkuu..Mwijaku ni mtu wa utani. Ile nyumba sio ya bilioni. Kaangalie nyumba ya Marehemu Mchungaji Rwakatare ambayo aliijenga kwa Bilioni 1 halafu linganisha na nyumba ya Mwijaku.
Kuna vitu anasema tu kunogesha kipindi. Kwamfano;
Swimming pool ndogo tu ambayo ipo juu kasema ni milioni 38
Taa moja anasema ni Laki 8
Taa za nje Moja anasema ni laki 5
Banda la mbwa (la kawaida sana) anasema laki 7
Unaona kabisa anadanganya ila dhumuni ni kunogesha tu kipindi.
Mamlaka ndo zimemwambia akajenge ghorofa kwenye kakiwanja ka kufugia kuku???
Jibu linaweza kuwa ndio au hapana kwasababu hatujui ndani kaweka facilities gani,katumia vifaa gani kwenye finishing.Kwahyo hii yumba ndo ya billion 1 na million 300?View attachment 2863228 ni
Watu hawabishi kuwa hana au hawezi kujenga nyumba ya bilioni,wanachobisha hio nyumba ya bilioni ndio hio? Labda huko ndani kuna vifaa vya high end.Hongera zake DC Mwijaku. Watu tuna maono tofauti. Personally naona 1 B ipo mbali. Lakini kwa wengi tuliojenga, ni wachache wanajenga wakiwa na cash bank. So inawezekana.
Gharama ya nyumba ni finishing na furnishing. Unaweza kuweka mlango wa million mbili na mimi nikaweka mlango wa laki mbili.
In all hongera sana kidume mwijaku! Nyumba ni heshima.
Ameiheshimisha kigamboni..ni his voice.
Kwamujibu wa vibali vya ujenzi yuko sawa kabisa, ila hayuko sawa kwa matumizi binafsi ya ardhi hapo baadae.Hujui kuna kitu kinaitwa kibali cha ujenzi au bado unaishi kwa shemeji?
Kwani mwikaju ndio nani huku mjini Daslamu Smart??🤔😁???