Mwijaku alishindwa nini kununua kiwanja kinachoendana na mipango yake ya ujenzi? Kampuni ya ujenzi ilishindwa kumshauri?

Mwijaku alishindwa nini kununua kiwanja kinachoendana na mipango yake ya ujenzi? Kampuni ya ujenzi ilishindwa kumshauri?

Kwa Tanzania haswa mjini mjini, wengi nyumba zipo namna hiyo kwa sababu nyumba ikiwa na eneo kubwa lazma utaijua kwa ukubwa wa uzio wake kwa hiyo alichokifanya mwijaku sio kipya ila pia mtoa mada una point kiasi.

All in all Mwijaku apongezwe kwa kujitahidi maana ni watu maarufu wachache wanaweza kumiliki nyumba ya namna hiyo
 
Mnapojadili hii mada wekeni kwenye mbongo then maneno Great thinkers ; jukwaa limeandaliwa kwa ajili ya kujadili hoja siyo kusifu na kupeana moyo.

Kama huna uwezo wakufahamu nafasi ya bilioni moja kwenye ujenzi usijitutumue kujadili kwa sababu tu unataka kusema; katika ujenzi Ile nyumba ya Mwijaku haina thamani ya bilioni moja na milioni mia tatu.

Lakini kwa upande wa pili hoja hapa siyo thamani ya nyumba, ni kiwanja na eneo alipojenga. Tukubali kwamba huyu kakosea kujenga, alipaswa kujenga nyumba kwenye eneo ambalo limepimwa na lina nafasi ya kupata oxygen.

Lakini pia ifahamike hapa hatupo kumshauri Mwijaku, tupo kuwashauri wengine wanaotamani kujenga.....tunawafumbua macho.

Jambo jingine ambalo wasanii wanapaswa kulizingatia kwa huko tuendako ni utajiri unaoendana na uwezo wa kulipa kodi. Mwijaku angetamka 1.3 bilioni kwenye nchi zilizoendelea hoja ingekuwa anapata wapi hizi fedha? Analipa kodi kutokana na faida ya mapato yake? Kibongo bongo hakuna mtu anayejali analysis ya kodi za nchi na ndiyo maana hatuna tatizo na kutaja figure kubwa.

Kwa wale tunaopanga kujenga lazima tujione kwenye nafasi hiyo. Wapo wanasiasa wengi na watumishi wa umma wamekimbia majumba yao na makazi yao baada ya kuteuliwa kwa sababu walishindwa kujipanga wajenge wapi kabla yakupewa madaraka.

Tununue maviwanja siyo viwanja

Mkuu kuna watu wachache sana wanajua endorsements kwa hawa watu maarufu huwa zinafikia bei gani ndio maana tunaona ni issue ngumu sana kwa wao kutimiza 1 B..

Ila nikuhakikishie tu, kwa balozi anazozipata mwijaku wakati hana maisha ya ku_fake au starehe sana ambacho ni chanzo cha umaskini wa wasanii wengi. Hiyo pesa anafikisha
 
Tembea ndugu yangu ukijifungia ndani utabishana na kila anaekupa taarifa...
Kwahyo hii yumba ndo ya billion 1 na million 300?
IMG-20240105-WA0000.jpg
ni
 
Ipo

Ya Mwijaku ni 1.2 Bilioni na imejengwa kwa miezi kumi tu.....

Mwijaku ni mtu wa utani. Ile nyumba sio ya bilioni. Kaangalie nyumba ya Marehemu Mchungaji Rwakatare ambayo aliijenga kwa Bilioni 1 halafu linganisha na nyumba ya Mwijaku.

Kuna vitu anasema tu kunogesha kipindi. Kwamfano;

Swimming pool ndogo tu ambayo ipo juu kasema ni milioni 38

Taa moja anasema ni Laki 8

Taa za nje Moja anasema ni laki 5

Banda la mbwa (la kawaida sana) anasema laki 7

Unaona kabisa anadanganya ila dhumuni ni kunogesha tu kipindi.
 
Hongera zake DC Mwijaku. Watu tuna maono tofauti. Personally naona 1 B ipo mbali. Lakini kwa wengi tuliojenga, ni wachache wanajenga wakiwa na cash bank. So inawezekana.

Gharama ya nyumba ni finishing na furnishing. Unaweza kuweka mlango wa million mbili na mimi nikaweka mlango wa laki mbili.

In all hongera sana kidume mwijaku! Nyumba ni heshima.
Ameiheshimisha kigamboni..ni his voice.
 
Watanzania tunapaswa kubadili mawazo na fikra zetu hasa katika kufukia fedha kwenye ujenzi. Tuna watu wengi wanakosea kujenga kwa kukosa mawazo sahihi au exposure. Tafsi ya nyumba siyo mpangilio wa tofali bali ni muunganiko wa ramani na mazingira ya nje.

Viwanja vya masaki na osterbay vinaweza kuwa kielelezo cha fikra za ujenzi zinavyotakiwa kuwa. Alichofanya mwijaku na kampuni aliyowapa kazi ni aibu kwa karne hii.

Unapoweka malengo yakujenga nyumba hasa ghorofa unapaswa kuanza kuwaza kiwanja, eneo kiwanja kilipo na majirani wanaokuzunguka.

Unapotenga bilion moja ya ujenzi tunategemea kiwanja kitengeewe si chini ya milioni mia na hamsini endapo unataka kupata kiwanja mjini. Jengo la bilioni moja kibongo bongo linapaswa kujengwa kwenye eneo la heka moja endapo utajenga kigamboni ambapo maeneo ni makubwa.

Waliomshauri na kumjengea Mwijaku ndio washauri wa NHC, ambao wanajenga nyumba Tanzania kwenye kiwanja cha Sqmt 200 au 400 kwenye jiji kama Dodoma ambalo linakuwa . Poverty mentality ya wataalam wa ardhi wa nchi imepelekea watu kujenga kwa gharama kubwa lakini hawana uwezo wakupaki magari ishirini au kuwaalika marafiki nyumbani. Unakuwa na nyumba kama ya mwijaku lakini ukialika marafiki mia kuja kwako unalazimika ukatafute ukumbi. Leo Mwijaku akitazama chini akiwa ghorofani anawachungulia majirani.

Nyumba kama ile ingejengwa kwenye eneo sahihi hata wafanyakazi wenzake wangetuonyesha garden ya nje na wangepiga picha hata mandhari ya kwenda kwa huyu mjuba.

Nakubali kwamba tunanunua viwanja tukiwa hatujui tunajenga nini ila tunapochora ramani ya nyumba kama ile tutafute kiwanja. Alishindwa nini kwenda kujenga mbweni huko au bagamoyo ?

Nampongeza na niwapongeze wote wenye maono kama yake ila tubadili fikra tuje na maeneo ya uzunguni ambapo tukitaka kutembelea tunakuta miundombinu hata ya usalama ipo sawa.

Povu lazima
Kama yeye kaanza na wenzake watajiongeza.

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Mwijaku ni mtu wa utani. Ile nyumba sio ya bilioni. Kaangalie nyumba ya Marehemu Mchungaji Rwakatare ambayo aliijenga kwa Bilioni 1 halafu linganisha na nyumba ya Mwijaku.

Kuna vitu anasema tu kunogesha kipindi. Kwamfano;

Swimming pool ndogo tu ambayo ipo juu kasema ni milioni 38

Taa moja anasema ni Laki 8

Taa za nje Moja anasema ni laki 5

Banda la mbwa (la kawaida sana) anasema laki 7

Unaona kabisa anadanganya ila dhumuni ni kunogesha tu kipindi.
Unaweza ukawa upo sahihi ila kutokana na kupanda kwa vifaa vya Ujenzi nyumba zinatofautiana thamani kama walijenga vipindi tofauti Mkuu..
 
Hongera zake DC Mwijaku. Watu tuna maono tofauti. Personally naona 1 B ipo mbali. Lakini kwa wengi tuliojenga, ni wachache wanajenga wakiwa na cash bank. So inawezekana.

Gharama ya nyumba ni finishing na furnishing. Unaweza kuweka mlango wa million mbili na mimi nikaweka mlango wa laki mbili.

In all hongera sana kidume mwijaku! Nyumba ni heshima.
Ameiheshimisha kigamboni..ni his voice.
Watu hawabishi kuwa hana au hawezi kujenga nyumba ya bilioni,wanachobisha hio nyumba ya bilioni ndio hio? Labda huko ndani kuna vifaa vya high end.
 
Hujui kuna kitu kinaitwa kibali cha ujenzi au bado unaishi kwa shemeji?
Kwamujibu wa vibali vya ujenzi yuko sawa kabisa, ila hayuko sawa kwa matumizi binafsi ya ardhi hapo baadae.

MICHORO ILIYOANDALIWA IONYESHE NINI:

Michoro itakayoandaliwa inatakiwa ionyeshe mambo yafuatayo:-

  • Namna jengo litalavyokuwa ”sections elevation”, "foundation”, “roof plan”, “site plan”.
  • Ramani ya kiwanja (location plan)
  • Namba na eneo la kiwanja kilipo
  • Jina la mmilikaji ardhi inayohusika
  • Jina la mchoraji, ujuzi na anwani
  • Ukubwa wa kiwanja kwa mita za mita za mraba
  • Ukubwa wa jengo kwa mita za mraba
  • Ujazo wa kiwanja (plot coverage).
  • Uwiano (Plot ratio)
  • Urefu wa jengo kwenda juu (Height)
  • Matumizi yanayokusudiwa
  • Idadi ya maegesho yatayokuwepo
  • Umbali wa jengo kutoka kwenye mipaka ya kiwanja (setbacks) na
  • Mfumo wa kutoa maji taka hadi kwenye mashimo, au bomba la maji taka
 
Back
Top Bottom