Mnapojadili hii mada wekeni kwenye mbongo then maneno Great thinkers ; jukwaa limeandaliwa kwa ajili ya kujadili hoja siyo kusifu na kupeana moyo.
Kama huna uwezo wakufahamu nafasi ya bilioni moja kwenye ujenzi usijitutumue kujadili kwa sababu tu unataka kusema; katika ujenzi Ile nyumba ya Mwijaku haina thamani ya bilioni moja na milioni mia tatu.
Lakini kwa upande wa pili hoja hapa siyo thamani ya nyumba, ni kiwanja na eneo alipojenga. Tukubali kwamba huyu kakosea kujenga, alipaswa kujenga nyumba kwenye eneo ambalo limepimwa na lina nafasi ya kupata oxygen.
Lakini pia ifahamike hapa hatupo kumshauri Mwijaku, tupo kuwashauri wengine wanaotamani kujenga.....tunawafumbua macho.
Jambo jingine ambalo wasanii wanapaswa kulizingatia kwa huko tuendako ni utajiri unaoendana na uwezo wa kulipa kodi. Mwijaku angetamka 1.3 bilioni kwenye nchi zilizoendelea hoja ingekuwa anapata wapi hizi fedha? Analipa kodi kutokana na faida ya mapato yake? Kibongo bongo hakuna mtu anayejali analysis ya kodi za nchi na ndiyo maana hatuna tatizo na kutaja figure kubwa.
Kwa wale tunaopanga kujenga lazima tujione kwenye nafasi hiyo. Wapo wanasiasa wengi na watumishi wa umma wamekimbia majumba yao na makazi yao baada ya kuteuliwa kwa sababu walishindwa kujipanga wajenge wapi kabla yakupewa madaraka.
Tununue maviwanja siyo viwanja