Mwijaku alishindwa nini kununua kiwanja kinachoendana na mipango yake ya ujenzi? Kampuni ya ujenzi ilishindwa kumshauri?

Mwijaku alishindwa nini kununua kiwanja kinachoendana na mipango yake ya ujenzi? Kampuni ya ujenzi ilishindwa kumshauri?

Kwenye akaunti ya Instagram ya Msechu ameweka mwonekano wa nje wa nyumba yake.....kwamwambia Mwijaku akatafute watu wakufanya finishing ......lakini mchechu katika video yake unasikia ndege wakilia means amepanda miti kwake na anazo garden zakuvuta oxygen

Nyumba ya Mwijaku inakosa garden, inakosa uoto wa asili na haina privacy kwani imebanwa kwenye kiwanja kidogo
 
Bongo hakuna nyumba ya kuishi yenye thamani ya billioni 1
Iyo ya ngurumo ya upako
1704541985147.jpg
 
Webongo wengi ukiwashauri utasikia we unayo, mchawi, wivu nk. Hawawezi kupokea ushauri au challenge kama watu wazima. Bado wabongo wengi wana akili za kitoto. Namaanisha wabongo wengi wamekomaa miili ila akili zao wengi za kitoto.
Ni swali zuri sana. "We unayo?" Kama unayo na inafanana na ushauri unaotoa ni rahisi kuaccept challenge yako kama huna uwezekano kuwa una wivu ni mkubwa.
 
Watu 100 wanakuja kwako kufanya nn? Kucheza kigodoro au mdumange
Yaani hapo maswali mengi sana,watu 100+?
Kwangu wawili tu ntaishia kuwafukuza,sasa 100 hao watu utadeal nao vipi.
Unaweza kutoka kijijini ila kijiji kisikutoke.
 
Watanzania tunapaswa kubadili mawazo na fikra zetu hasa katika kufukia fedha kwenye ujenzi. Tuna watu wengi wanakosea kujenga kwa kukosa mawazo sahihi au exposure. Tafsi ya nyumba siyo mpangilio wa tofali bali ni muunganiko wa ramani na mazingira ya nje.

Viwanja vya masaki na osterbay vinaweza kuwa kielelezo cha fikra za ujenzi zinavyotakiwa kuwa. Alichofanya mwijaku na kampuni aliyowapa kazi ni aibu kwa karne hii.

Unapoweka malengo yakujenga nyumba hasa ghorofa unapaswa kuanza kuwaza kiwanja, eneo kiwanja kilipo na majirani wanaokuzunguka.

Unapotenga bilion moja ya ujenzi tunategemea kiwanja kitengeewe si chini ya milioni mia na hamsini endapo unataka kupata kiwanja mjini. Jengo la bilioni moja kibongo bongo linapaswa kujengwa kwenye eneo la heka moja endapo utajenga kigamboni ambapo maeneo ni makubwa.

Waliomshauri na kumjengea Mwijaku ndio washauri wa NHC, ambao wanajenga nyumba Tanzania kwenye kiwanja cha Sqmt 200 au 400 kwenye jiji kama Dodoma ambalo linakuwa . Poverty mentality ya wataalam wa ardhi wa nchi imepelekea watu kujenga kwa gharama kubwa lakini hawana uwezo wakupaki magari ishirini au kuwaalika marafiki nyumbani. Unakuwa na nyumba kama ya mwijaku lakini ukialika marafiki mia kuja kwako unalazimika ukatafute ukumbi. Leo Mwijaku akitazama chini akiwa ghorofani anawachungulia majirani.

Nyumba kama ile ingejengwa kwenye eneo sahihi hata wafanyakazi wenzake wangetuonyesha garden ya nje na wangepiga picha hata mandhari ya kwenda kwa huyu mjuba.

Nakubali kwamba tunanunua viwanja tukiwa hatujui tunajenga nini ila tunapochora ramani ya nyumba kama ile tutafute kiwanja. Alishindwa nini kwenda kujenga mbweni huko au bagamoyo ?

Nampongeza na niwapongeze wote wenye maono kama yake ila tubadili fikra tuje na maeneo ya uzunguni ambapo tukitaka kutembelea tunakuta miundombinu hata ya usalama ipo sawa.

Povu lazima
Siwezi kuwa na 300M nikajenga kwny eneo lenye chini ya nusu heka

NASEMA SIWEZI
 
Nimemsikiliza maelezo yake, nikagundua Mwijaku bado ana ushamba wa Kigoma.

Anadai alipata ardhi kubwa Bagamoyo (kama ekari 2) lkn eti akaona hati ya nyumba yake itasoma Pwani. Yeye alitaka isomeke Dar.

Ndiyo maana akaamua kupachik jumba la 2 b huko uswekeni Kigamboni kwenye kiwanja cha 20 kwa 20. Jinga kabisa.
Hahahaha Yeye anajua Dar ndo kila kitu!
 
Back
Top Bottom