Mwili wa Agnes Gerald 'Masogange' wawasili Mbeya tayari kwa mazishi

Numbisa

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Posts
301,221
Reaction score
1,172,274
Mwili wa msanii Agnes Gerald ‘Masogange’ tayari umewasili Utengule, mjini Mbeya, huku wimbo unaotumika katika maombelezo wa msiba huo ukiwa ni ule wa msanii Abelnego Damian ‘Belle 9’ uitwao Masogange.

Wimbo huo uliotoka mwaka 2011, ndio uliompandisha chati marehemu na kujikuta anaitwa Masogange hadi hii leo.

Mwili wa Masogange uliwasili majira ya saa tano asubuhi na kupokelewa na makada wa Chama cha Mapinduzi(CCM) waliokuwa wamevalia sare za chama hicho na kuingizwa moja kwa moja ndani ya nyumba ya baba yake aliyokuwa amemaliza kumjengea siku za hivi karibuni.

Kupigwa kwa wimbo huo kuliibua simanzi kwa waombolezaji waliofika katika msiba huo japokuwa wapo wengine waliokuwa wakiucheza.

Wasanii wameshindwa kujizuia na kuangua vilio.
 
Mtoto wa Marehemu Agnes Masogange Akiwa Msibani... Ni Mwenye majonzi na Huzuni Sana Mzazi mwenza na Mtoto wa Marehemu Agnes Masogange Pichani wakilia Kwa Uchungu Sana kutokana na Msiba Huu mzito

Marehemu Agness enzi za uhai akiwa na mwanae
 
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI!
kwa namna ya pekee kabisa nawapa pole UVCCM na Green Guard kwa kufiwa na mwenzenu Agnes Masogange.

Awali niliwapa pole wasanii tu nikawasahau ninyi nduguze muhimu. Nimetambua uwepo wenu hususani Mbalizi Mbeya ambapo vijana wa Green Guard waliokuwa wamevalia kijani walibeba jeneza kwa huzuni kubwa.

Najua wengine mlimkana enzi akiwa na tuhuma za madawa ya kulevya mkisema UVCCM hawawezi hata kutuhumiwa lakini walau mmeikubali maiti yake.

Poleni sana Green Mamba...sorry I mean Green Guard kwa kuulinda vyema na kuusitiri mwili wa dada yetu.

Sisi vijana wa Mbeya tumewapenda kwa moyo huo ila upendo wetu kwenu si kama tumpendavyo Sugu our genius hustler.

Mungu awabariki!
 
Msanii wa Filamu johari akiwa mwenye huzuni sana.. Msibani mbeya...
 
Hali ilivyo nyumbani kwao Masogange, Mbeya.
Mzee Gerald Waya, baba mzazi waarehemu Masogange.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…