Aramun
JF-Expert Member
- Nov 8, 2023
- 461
- 2,213
Mwili wa Dr. Dismas Chami aliyekuwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Ulyankulu, Tabora umeokotwa maeneo ya Malolo, Tabora asubuhi ya leo. Dr.Chami aliondoka nyumbani (Kaliua) Jumatano ya September 4 na kumuaga mkewe kuwa anakwenda mjini Tabora kikazi na angerejea kesho yake. Hata hivyo hakurejea na simu zake hazikupatikana
Familia ilimtafuta kwa wiki nzima bila kujua alipo, lakini ilipofika Jumatano ya September 11 simu zake zilipatikana. Hata hivyo alipopigiwa hakupokea. Baadae alituma sms kwa mke wake iliyosomeka "Nisamehe sana, baada ya dakika chache sitakuwa nanyi duniani. Simamia kila kitu nilichokiacha. Pesa zote zipo CRDB bank, simamia watoto wasome. Kwaheri"
Baada ya kutuma sms hiyo, simu yake ilizimwa na hakupatikana tena. Polisi kwa kushirikiana na familia waliendelea kumtafuta bila mafanikio. Hatimaye leo mwili wake umeokotwa maeneo ya Malolo, ukiwa umechomwa sindano. Pembeni ya mwili huo kuna madawa mbalimbali ya hospitali ambayo inadaiwa yalitumika kujidunga/kudungwa.
Bado haieleweki kama amejiua mwenyewe kwa kujidunga madawa au ameuawa na watu waliomdunga madawa hayo. Haijafahamika pia kama sms aliyotuma kwa mkewe alituma kwa utashi wake au alikuwa chini ya shinikizo. Polisi wamesema wanachunguza chanzo cha kifo chake kujua kama kimetokana na migogoro ya kifamilia, Msongo wa mawazo, madeni, ugomvi binafsi au sababu nyinginezo. Rest easy Dr. Chami.!
Credit: Malisa GJ, X Page