Exactly.
Sms fake ya kutengenezwa yenye nia ovu ya kutaka kuwaghiribu watu ili wasijue kiini halisi Cha Mauaji hayo.
Just a spinning Propaganda.
Hali mbaya kabisa Kama Hii inanikumbusha wakati ule wa nyakati za mwisho mwisho kabisa kabla ya kuanguka kwa Utawala dhalimu wa Dikteta Mobutu Sesseseko aliyekuwa Rais wa zamani wa Zaire (Sasa Congo DR), Watu wengi sana walikuwa wakitekwa na kuuawa katika Mazingira ya kutatanisha Sana kama hivi inavyotokea hivi sasa hapa Tanzania. Maiti za Watu wakosoaji wa Utawala wake zilitakapaa mitaani, kila siku Wananchi walikuwa wanaokota miili ya Watu mitaani.
Aidha, kila siku (hususani nyakati za usiku) ndege na helikopta za Jeshi zilikuwa zinatua nyumbani kwa Rais Mobutu kijijini kwake Gbadolite zikiwaleta 'Mateka' waliokusanywa kutoka katika miji na mikoa mbalimbali iliyopo kwenye nchi hiyo ya Zaire ili wàweze kuteswa mbele ya Rais Mobutu mwenyewe akishuhudia kwa macho yake na mwishowe mateka hao waliuliwa kikatili sana. But all in all, mwisho wa dhahama yote hiyo, Dikteta Mobutu aliishia kumteka hata Mkuu wake wa Majeshi (CDF) General Mahele na kumuua kikatili kama nguruwe pori, na hapo ndipo Utawala wake wa kidikteta ulipofika mwisho wake.
Watanzania tuzidishe sala na maombi kwani kunakaribia kukucha, Wakimaliza kututeka sisi Wananchi basi watageukiana wao kwa wao, kama ilivyofanyika nchini Zaire kwa Rais Mobutu.