Huyu ni gaidi..hayo huwa yanauliwa kimya kimya.
#MaendeleoHayanaChama
Sent using
Jamii Forums mobile app
Saazingine kumumunya maneno ama kukosa mtu wa kulisemea jambo kuna madhara makubwa sana.
Hivi, maiti zote zilizozalishwa "operesheni Kibiti" zilipelekwa kuzikwa wapi?
Hilo la kwanza, la pili mateka wote katika operesheni hiyo walipelekwa gereza gani la mahabusu kusubiria mwenendo wa kesi zao?
Kuna kesi ngapi za magaidi wa Kibiti zilizofunguliwa mahakamani mpaka sasa?
Dodoso la maswali yote hayo ni kuonesha namna Serikali inavyoweza kufanya kazi nzuri sana na kisha matokeo ya kazi hiyo mwishoni kuonekana kuichafua Serikali hiyo hiyo!
Ni kwa sababu gani, ni kwa sababu ya kutokupangilia vyema mustakabali wa jambo lolote jema linalopangwa kufanywa kwa ajili ya maslahi mapana ya umma.
"Operesheni Kibiti" imeacha doa kwa Serikali ya awamu ya5 kwa kushindwa kwake kupangilia vyema uendeshaji wa Operesheni hiyo.
Operesheni za kijeshi kwa lugha mbadala ni "vita".
Vinapopangwa vita, ukiacha gharama na maslahi ya wanajeshi watakao shiriki katika vita hivyo, huangaliwa pia namna wafungwa wa vita watakakohifahiwa na mustakabali wao.
Sasa ilikuwaje walioplan vita hiyo wakashindwa kuainisha kipengele hicho muhimu?
Hata kama ilikuwa imepangwa kuwaelliminate mateka wote, ilitakiwa kuwe na kituo cha kupokelea mateka hao, kuwahoji na kuwauwa na kisha kuwazika.
Na katika mazishi hayo lazima viwekwe vitambulisho vya majina yao halisi kila kaburi na siyo kuwazika halaiki.
Kosa walilolifanya la kiufundi kuwauwa mateka na kuwajaza kwenye viroba na kisha kuwatupa ovyo kihuni.
Kwa kuwa hapajasemwa wazi kadhia hiyo labda kwa kuhofia kuwajibishwa, wasiofahamu ukweli huu, mpaka leo wanaisema vibaya Serikali kuwa ilikuwa inauwa wapinzani na kuwatupa kwenye viroba na hakuna aliyefungua domo lake kukanusha!
Mambo hayo yangeliwekwa wazi pasingelitokea mtu wa kuchongoroa mdomo kuibebesha lawama nzito Serikali kwa jambo hilo lililoleta ushindi wenye manufaa.