Mwili wa mwanamuziki mashuhuri, marehemu Tabia Mwanjelwa kuwasili nchini Jumatatu

Mwili wa mwanamuziki mashuhuri, marehemu Tabia Mwanjelwa kuwasili nchini Jumatatu

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
Mwili wa mwanamuziki mkongwe, Bi. Tabia Shabani Mwanjelwa, aliyefariki dunia Januari 25, 2025, huko Saarbrücken, Ujerumani, anakoishi na familia yake, unatarajiwa kuwasili nchini siku ya Jumatatu, Februari 17, 2025, saa tano asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa binti yake kipenzi, Jane Jackson, mwili wa marehemu utawasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam. Baada ya kuwasili, taratibu za mazishi zitaelekezwa Tukuyu, mkoani Mbeya, ambako atapumzishwa katika nyumba yake ya milele.

1739366433289.png

Marehemu Tabia Mwanjelwa atakumbukwa kwa vibao vyake maarufu kama "Jane Mimi Nahangaika" na "Kweli Maisha ni Safari Ndefu", alizoimba akiwa na bendi ya Maquis du Zaire miaka ya 1980.

Ingawa aliishi Ujerumani kwa zaidi ya miaka 40, hakuwahi kusahau nyumbani kwani mara kwa mara alitembelea Tanzania, hususan kwao Mbeya, kila alipopata fursa.

Kwa mujibu wa Jane, mama yake alikuwa akisumbuliwa na uvimbe kooni kwa muda mrefu kabla ya kufariki dunia Januari 25, 2025, saa moja na dakika 10 asubuhi.

Jane, ambaye si mwanamuziki kama kaka yake Moses, amesema ameshangazwa na simu na salamu nyingi alizopokea kutoka kila pembe ya dunia, akisema hakuwahi kutambua kuwa mama yake alikuwa maarufu na mwenye marafiki wengi kiasi hicho.

Mola ailaze pema roho ya marehemu - AMINA
 
KKuna Wanyakyusa na sisi Waswahili. Je ni Nani haswa mlengwa wa swali lako?
Kwa nini alikuwa anaishi ujerumani enzi za uhai wake alafu nyie waswahili mnataka azikwe huku?
 
Back
Top Bottom