Mwili wangu huwa unanuka mpaka sina raha ya kuishi

Mkuu kama una hilo tatizo sema nukusaidie utapona ndani ya week Tatu. Namshangaa anayetafuta ushauri kaebda mazima. Ni dawa za uhakika. Mimi sio mshirikina mkuu. Ila ukijichanganya siyo mbaya pia
Mi natafuta dawa ya kumtengeneza MTU kma uko vizuri tutafutane
 

Wewe ni daktari? Nataka nije unitibu.
 
Pole sana, yalimkuta jamaa yangu chumba alichokitumia chuoni nasikia hadi leo (10 yrs)
 
Usifanye chochote nenda hosipitali. Hakuna pafyumu ya kupaka sehem za siri. Ila unaweza kutumia deodorant inayokausha inakuwa kama na ute flani wa yai. Ukiipaka inazuia kulowana huko chini. Pia hizo ni dalili za fangasi. Kama unaogopa basi chikua vidonge vinaitwa gsufluvin unakunywa kimoja mara mbili kwa siku. Kwa muda wa wiki 6pia wakati huo nenda hospitali ya serikali wambie wakupe whitefield utakuwa unapaka muda wote unaokunywa dawa mpaka miezi 3
 
Yawezekana ni fungus. Jaribu kutafuta matibabu.

Njia nyinhine uwe unaoga maji ya ugali. Yaani baada ya kupika ugali loweka sufuria kwa muda mrefu hadi maji yapate harufu hiyo ya ugali, wastani masaa manne 4, kisha baada ya kuoga kwa medicated soap hasa Securex, ukimaliza kujisafisha na maji masafi., oga sasa na hayo maji ya ugali mwili mzima hasa sehemu hizo. Kisha acha ukauke bila kujifuta na taulo.
 
Pole sana. Nashauri yafuatayo:
1. Nenda hospital
2. Fuatilia tiba ya Mkuu Rais 2020 ( Mchawi/Mganga)
3. Tumia maji ya moto yenye limao glasi moja kwa 2weeks, kila asubuhi.
4. Kunywa supu ya kitunguu swaumu bakuli moja daily kwa 1week hii itabadili harufu yako kuwa ya kitunguu
Hatua zote kama majibu ni zero basi ingia kwenye maombi ... Kwani binadamu si watu wema. Hizo ni hatua zilizo chukuliwa na jamaa zangu zikawasaidia.
 
kiufupi wewe haunuki. tena bora ungesema unanuka kwapa lakini siyo kengele. una ugonjwa wa kisaikolojia unaitwa olfactory reference syndrome (ORS). ni aina ya delusions (false beliefs). Reference maana yake una refer tabia za wengine na kunuka kwako. mtu akikihoa, akijishika pua, akipiga chafya, akifungua dirisha, au hata mbwa kubweka wewe unahisi ni kwasababu unanuka.

wengi wenye hii shida unakuta hiyo harufu wao hawajawahi isikia. wengi huuliza watu wanaowaamini ikiwa wananuka, wakiambiwa hawanuki wanaona watu hao wamewadanganya kwa kuogopa kuwaambia ukweli. wengi huoga au kupiga mswaki mara nyingi,huvaa chupi au nguo nyingi na hujinusanusa. hii ishu ina haribu sana kazi, mahuiano na maisha kiujumla.

nashauri muulize mtu unayemuamini iwapo unanuka na jielimishe zaidi kuhusu ORS.
 
Mkuu nenda hospitali na kisha tembelea beach mara kwa mara ukaoge yale maj bahari
 
Utakuwanna fungal infection inaitwa Tinea Cruriz, ni common sana kwa wanaume kutoka na joto ,huwa ijakuwa kati ya mapaja na mapumbu ila yako itakuwa chronic, huwa inatibika kirahisi kwa dawa za kupaka ziko nyingi sana na kwa bei rahisi kabisa, ikiwa chronic itakubidi unywe dawa za kunywa, wala sio ishu kubwa hiyo. Nenda kamuonape Daktari Mohammed Amiti
 
Mohamed amiti hata usiende hospitali. Nakuelekeza dawa ukaitumie na mrejesho utauleta mwenyewe hapa baada ya week Tatu mpaka nne.
Mdogo Wangu alisumbuliwa sana na hilo tatizo ila sasa limekuwa ni historia kwake
 
Kuna zile strong perfume ambazo ukijipulizia kwenye shati au suruali inakaa hata wiki bado ipo hata ukifua shati au suruali, ila ni expensive kidogo zinaenda mpaka laki moja
Ukipuliza hyo umeharibu kabisa
 
Pole sana mkuu...
Umejaribu kuwaona madaktari? Wanaweza wakawa na njia ya kukusaidia.
Kuna rafiki yangu alikua anatafuna vitunguu saumu, kuanzia chumba chake hadi yeye mwenyewe mkipishana njiani alikua ananukia kitunguu saumu. Jaribu kutafuna vitunguu saumu labda harufu itapungua.
Pia nunua sabuni ya kuogea emperial... Ina harufu nzuri na hubaki mwilini.
Tafuta zile poda za watoto, zile za zamani zenye chupa ya blue. Hii poda inaziba sana harufu. Ukitoka kuoga jikaushe vizur, paka mafuta ya mgando haswa kwenye sehemu nanazosem zinatoa harufu alafu paka hiyo poda... Usiogope kujikandika.
Nunua spray au perfume yenye harufu kali, achana nao watakaoumizwa na harufu hiyo. Isiwe kali sana ikawa kero. Kuna spray moja inaitwa "BOD", ina harufu nzuri na haitoki kwenye nguo ata ukifua.

Cha ziada ni endelea kujiweka msafi, usirudie kuvaa nguo na be cheerful
 
Pole, cha kwanza jikubali.Tambua kila mwanadamu ana kilema(udhaifu) katika sehemu ya mwili wake,au akili awe amejijua au la.Pia waone wataalamu wa afya ikishindikana omba au uombewe kwa jina la Yesu nahisi ni pepo limekuchafua.
Amina! Yaani huyu ata sishangai! Kuna ndugu yetu tulikua tunaishi nae, akitoka bafuni huwezi ingia hiyo harufu itakayokua imebaki humo... Yaani alikua ananuka hadi nyumba nzima ikawa na harufu yake, akikaa kwenye kochi sebleni mwingine hawezi likalia. Cha ajabu nimekutana nae juzi kati kwenye harusi ya bro mwingine, hana hata kiarufu zaidi ya kunukia spray. Hii hali itaisha mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…