SI KWELI Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Bonny Mwaitege afariki dunia katika ajali ya barabarani

SI KWELI Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Bonny Mwaitege afariki dunia katika ajali ya barabarani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania Bonny Mwaitege amefariki dunia katika ajali ya barabarani. Bony alifariki katika ajali hiyo baada ya kutoka katika tamasha. Ni mmoja wa mwanamuziki wa nyimbo za injili anayejulikana Afrika Mashariki. Atakumbukwa zaidi kwa nyimbo zake kama vile 'Safari Bado.'

1721638271309.jpg

 
Tunachokijua
Leo Julai 22, 2024, imezuka taarifa kwenye mitandao ya Kijamii ikidai Mwimbaji wa Nyimbo za Injili nchini, Bony Mwaitege amefariki kwenye ajali ya gari akiwa anatoka kwenye tamasha.

Baadhi ya Akaunti zilizochapisha taarifa hiyo zimehifadhiwa hapa na hapa.

Ukweli upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini taarifa hio haina Ukweli. Kupitia mahojiano ya mke wa Mwaitege yaliyofanyika kupitia AyoTV, amesema "Bony Mwaitege ni mzima kabisa ametoka safari kutoka Kenya na amefika nyumbani salama, amepumzika"

Pia, JamiiCheck imepata sauti ya kiongozi wa muziki wa Injili anayefamika kwa jina la Mtumishi Stella, akikanusha taarifa hiyo.

"Jamani haya matangazo yanayoendele kwenye mitandao kwamba Bonny Mwaitege amefariki siyo ya kweli. Bonny Mwaitege mzima wa afya, hajafa" amesema Stella.

Aidha, akizungumza na Gazeti la Mwananchi, leo Jumatatu Julai 22, 2024, Seme Shitindi ambaye ni mtu wa karibu wa familia ya mwimbaji huyo na mshirika wake katika Kanisa la Safina, amekanusha taarifa hizo akisema ni za uzushi.

"Ni uongo, Mwaitege ameingia asubuhi hapa alikuwa Mbeya, sasa hivi yupo nyumbani kwake wala hajafariki. Jana alikuwa anamaliza mkutano Tunduma, wala hakuwepo Kenya, hivi sasa nilikuwa naongea naye," amesema Shitindi.

Mwaitege anajulikana sana Afrika Mashariki hasa kwa wimbo wake wa ‘Utanitambuaje'
Kumekuwa na tabia chafu ya watu kuzushiwa kuwa wamefariki ingawa wapo hai.
Leo mwimbaji wa injili Bon mwaitege amezushiwa kuwa amefariki, kibaya zaidi waliozusha taarifa hizo ni media ambayo ipo kwenye game kwa muda mrefu (Rick Media)
Binafsi naona wanatakiwa washugulikiwe na rungu la serikali ili iwe fundisho
 

Attachments

  • IMG-20240722-WA0023.jpg
    IMG-20240722-WA0023.jpg
    132.8 KB · Views: 1
  • Screenshot_20240722-134450.png
    Screenshot_20240722-134450.png
    814.8 KB · Views: 3
  • Screenshot_20240722-133625~2.png
    Screenshot_20240722-133625~2.png
    1.5 MB · Views: 2
Kumekuwa na tabia chafu ya watu kuzushiwa kuwa wamefariki ingawa wapo hai.
Leo mwimbaji wa injili Bon mwaitege amezushiwa kuwa amefariki, kibaya zaidi waliozusha taarifa hizo ni media ambayo ipo kwenye game kwa muda mrefu (Rick Media)
Binafsi naona wanatakiwa washugulikiwe na rungu la serikali ili iwe fundisho
Tunaomba majina ya wamiliki wa hii Blog,
 
Yani hiyo media walitoa hiyo habari kisha ndio wakawa wanawasiliana na watu wa karibu wa huyo Rick ili kupata uhakika! kwa lugha rahisi wanafanya kazi kwa kutumia gia ya rivasi.

Mbele wamepeleka nyuma na nyuma wakapeleka mbele!
 
Back
Top Bottom