SI KWELI Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Bonny Mwaitege afariki dunia katika ajali ya barabarani

SI KWELI Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Bonny Mwaitege afariki dunia katika ajali ya barabarani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania Bonny Mwaitege amefariki dunia katika ajali ya barabarani. Bony alifariki katika ajali hiyo baada ya kutoka katika tamasha. Ni mmoja wa mwanamuziki wa nyimbo za injili anayejulikana Afrika Mashariki. Atakumbukwa zaidi kwa nyimbo zake kama vile 'Safari Bado.'

1721638271309.jpg

 
Tunachokijua
Leo Julai 22, 2024, imezuka taarifa kwenye mitandao ya Kijamii ikidai Mwimbaji wa Nyimbo za Injili nchini, Bony Mwaitege amefariki kwenye ajali ya gari akiwa anatoka kwenye tamasha.

Baadhi ya Akaunti zilizochapisha taarifa hiyo zimehifadhiwa hapa na hapa.

Ukweli upoje?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini taarifa hio haina Ukweli. Kupitia mahojiano ya mke wa Mwaitege yaliyofanyika kupitia AyoTV, amesema "Bony Mwaitege ni mzima kabisa ametoka safari kutoka Kenya na amefika nyumbani salama, amepumzika"

Pia, JamiiCheck imepata sauti ya kiongozi wa muziki wa Injili anayefamika kwa jina la Mtumishi Stella, akikanusha taarifa hiyo.

"Jamani haya matangazo yanayoendele kwenye mitandao kwamba Bonny Mwaitege amefariki siyo ya kweli. Bonny Mwaitege mzima wa afya, hajafa" amesema Stella.

Aidha, akizungumza na Gazeti la Mwananchi, leo Jumatatu Julai 22, 2024, Seme Shitindi ambaye ni mtu wa karibu wa familia ya mwimbaji huyo na mshirika wake katika Kanisa la Safina, amekanusha taarifa hizo akisema ni za uzushi.

"Ni uongo, Mwaitege ameingia asubuhi hapa alikuwa Mbeya, sasa hivi yupo nyumbani kwake wala hajafariki. Jana alikuwa anamaliza mkutano Tunduma, wala hakuwepo Kenya, hivi sasa nilikuwa naongea naye," amesema Shitindi.

Mwaitege anajulikana sana Afrika Mashariki hasa kwa wimbo wake wa ‘Utanitambuaje'
Mleta taarifa si utoe habari kamili?? au unataka uonekana wa kwanza husemi ajali imetokea wapi?? lini?? shida ni nn?? unasema tu ajali
 
Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka nchini Tanzania Bonny Mwaitege amefariki dunia katika ajali ya barabarani. Bonny alifariki katika ajali hiyo baada ya kutoka katika tamasha. Ni mmoja wa mwanamuziki wa nyimbo za injili anayejulikana Afrika Mashariki. Atakumbukwa zaidi kwa nyimbo zake kama vile 'Safari Bado.'

Wamekanusha kuwa sio Kweli.
 

Attachments

  • IMG-20240722-WA0024.jpg
    IMG-20240722-WA0024.jpg
    51.6 KB · Views: 7
Back
Top Bottom