Mwingira amlaani mchungaji Loliondo!

Mwingira amlaani mchungaji Loliondo!

Naamani alipoambiwa akanawe mtoni utukufu ulikuwa wapi?
To me anayemponda babu ni mfanyabiashara bse either mapato yake yameshake au wateja wamepungua kwake so babu amecreate stiff competition.
Babu kutoza 500 ambayo kwa iyo anaambulia mia tuu ni kama ujira wake as kumbuka ni mchungaji mstaafu ameacha shughuli zake anatibu watu so familia yake ingeteseka kama si izo 100.
Kuna watu wanakuja na hoja za kutibu bure ivi 500 sio sawa na bureeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Babu kuwa makini as maabdui zako nao wako mbioni kukumaliza ila kama ni mpango wa mungu hautadhulika kamwe
 
Ukitupa jiwe kwenye kundi la watu na ukasikia mtu analia basi ujue huyo ndiye limempata

*
Habari za kuaminika toka ndani ya Wanachama ngazi ya juu chama cha CCM inasema, wataalamu kutoka South Afrika walitumia ujuzi wao wa kuongoza Raia kwa kuwafundisha Serikali ya Tanzania kumtumia Babu wa Loliondo (bila ya yeye kujua)*kuelekeza matangazo yote ya Redio, Tv, Magazeti n.k ihamie Loliondo badala ya kuwa kama yalivyokuwa yamehamishia nguvu zake za kumkosoa Raisi JK*na*chama cha*CCM.
*
Hata South Afrika, Watu weusi huwa wanakuwa na maamuzi ya ajabu wanaposikia neno SANGOMA (Mchawi), viongozi hao wa ngazi ya juu CCM wamesema, Vigogo wote wanaoenda Loliondo ni danganya toto bali ni *kwa ajili ya kuwahamashisha Raia wa kawaida waendelee kwenda Loliondo na kuwafanya wasahau matatizo yao ya kila siku!
*
Hata sisi tunaona labda kuna ukweli ndani yake, maana kama kawaida ya CCM wangeweza kuficha sura za Vigogo wao*kama wangetaka maana CCM ni watu mashuhuri sana kwa kuficha chochote kinachohusu chama au watu wao wa chama.
 
Mbona mfano wako haufanani na chochote hapa, umeishia darasa la ngapi wewe? maana hapa watu wanajibishana kwa hoja sasa wewe unafananishaje hapo? pmbf
Unakuwa kama sio great thinker bwana yaani hujamuelewa!!
 
tatizo ni nini? ni babu kuponyesha au ni babu kutoza fedha? watu wana maradhi yanayowasumbua kwa muda mrefu, ikitokea njia pekee ya kuweza kuponesha ni bora watu wapate tiba, tukisikiliza viongozi wa dini kama akina mwingira, turudi pale bwana yesu alipochora chini na kusema 'ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumpiga mwanamke mawe' hapo tutaona kuwa mwingira naye si safi.
 
si sahihi kuhalalisha ya babu kwa vile wengine pia kama kakobe, mwingira nk nao wanafanya. tupeni support ya kimaandiko please
Binafsi sina utaalamu sana wa mistari ya vitabu vya dini....ila ninachokiona toka kwako dada Judith ni kuwa unaonekana ulokole umekuingia sana kiimani. Hata jana niliisoma topic yako ya kumpinga Babu na nikaipotezea.....lakini nashukuru kunawatu walikujibu vizuri sana na walikuuliza maswali kadha wa kadha ambayo hukuwajibu kiufasaha....Dada Judith,kila kitu ni imani....hao unaowaona wanaenda kwa babu wanaimani ya kupona kama wewe ulivyo na imani na makanisa hayo ya BORN AGAIN. Mfano mimi binafs naamini makanisa yote haya ya BORN AGAIN ni wizi mtupu....people ar just doing busness there and nothing moo! Kwahiyo kwangu mimi ni Bora niende kwa Babu kuliko kwenye hayo makanisa yenu ya kitapeli.....yaani hata uniubirie nini kwa kunipa mistari...sidanganyiki ng'o....nitabaki na RC yangu till i die.
Na hakuna kanisa linalokusanya pesa nyingi kupitia michango ya kurazimisha kama Ephata ya Mwingira....jamaa ana domo la kukusanya mamilioni usipime!....na kwavile mang'ombe hayaishi hapa mjini basi wakina Mwingira,Kakobe nk. wanakula tu kiulaiiiini na wanaishi kama wafalme kwa pesa za walalahoi mang'ombe (mijitu mijinga) KWANGU MIMI...BORA BABU....KULIKO HIYO MISITARI YAKO UNAYODAI TUKUPE.
 
kwa taarifa yako, mimi ni mlutheri sio mlokole!

hata upnde wako, hiyo RC unayoita yako, wala sio yako, hata tarehe ilipoanzishwa hijui. hata account yake ina shilingi ngapi hujui, utasemaje yako? ni upofu tu unakusumbua na uvivu wa kutafakai. bora ukae kimya kuliko kuwaadhiri wa-RC wenzako. mimi ni mwanamke, ukinitongoza lazima nikubali na nijue nikiingi chumbani kwako naenda kufanya nini ndio niondoke na kukufuata. siendi nkama kipofu, naenda nikitazama na macho yangu mawili!

wewe unajiita m-RC huku umefumba macho unasema tukuache na u-RC wako, labda babu atakuponya, pole zako wewe, Yesu ndilo jibu, fungua macho na uijue kweli, hiyo kweli ndiyo itakayokuweka huru, babu hatakuweka huru

haya ndiyo matatizo ya uvivu wa kufikiri. ukichoka kufikiri unatafuta kitu cha kurukia. ukiona mistari ya biblia unasema "mlokole huyu" huyoooo.........., unamrukia! shame on you all mnaojifanya wakristo kumbe mnatuaibisha na upofu wenu wa maandiko na uvivu wa kutafakari neno la Mungu!

kwa kweli utakufa na u-RC yako. si kuwa utaenda jehanum kwa jaili ya RC kama dini, la hasha utaangamia kwa kukosa maarifa. kwa kuwa umemkataa Bwana na maarifa yake, ukaubatiza upofu wako jina la "RC", basi utaangamia na jina lako hilo la UREMBO. si maneno yangu haya, bali ni ya Bwana

sijakasirika ila wivu wa neno la Mungu umenila. be at peace!

Glory to God!
 
Mmmh....Naona umepanic sana!.....nimekugusa nini? zatzwhy nilikuambia binafsi sijasoma sana hivi vitabu vya mungu....ila nimepitiapitia kidogo. Siwezi poteza mda wangu kubishana na wewe kwa hizi dini za kuletewa na wazungu,waarabu.....,siwezi poteza mda wangu wa kubishana na wewe kwa hivi vitabu vilivyoandikwa na binadamu kama mimi na wewe....what i bealieve ni kuishi maisha ya kumpendeza mungu kwa kuacha kitu chochote ambacho unajua ukikifanya kitakuwa ni zambi mbele ya mwenyezi mungu......,naamini mungu yupo na ninaamini mungu anapenda tuwe na matendo mema.....So, huo ushabiki wa dini na vitabu vyake hapa duniani...,nawaachia watu kama nyie.
 
jamani si vyema kumwangalia mwingira kama mjasrimali pekee, bali pia tujiulize mengine aliyoibuka nayo. mfano kuna point hapo kwenye bold.

hata mimi naungana naye kuhoji hapo kwenye bold. anayejua atusaidie. mchungaji anaponya watu bila kuwahubiria kwa namna yoyote, ............we njoo, kamata kikombe chako, kwa heri!............ ni uchungaji gani huu?

Mungu anapewaje utukufu hapo?

tusaidiane please

Glory to God

MUNGU=YESU. Kwani babu anahubiri? Yeye anaponya maana kama ni kuhubiriwa mnahubiriwa sana lakini bado visukari, ukimwi vyawaandama. Hizo ni karama mbali mbali ambazo Mungu humpa mja ampendaye.
 
MUNGU=YESU. Kwani babu anahubiri? Yeye anaponya maana kama ni kuhubiriwa mnahubiriwa sana lakini bado visukari, ukimwi vyawaandama. Hizo ni karama mbali mbali ambazo Mungu humpa mja ampendaye.
Ahsante.....I like thiz sound from u.....wakipatikana watu 10 kama nyinyi....basi neno ubishi litatoweka kwa kasi....Ubarikiwe mkuu!
 
Mmmh....Naona umepanic sana!.....nimekugusa nini? zatzwhy nilikuambia binafsi sijasoma sana hivi vitabu vya mungu....ila nimepitiapitia kidogo. Siwezi poteza mda wangu kubishana na wewe kwa hizi dini za kuletewa na wazungu,waarabu.....,siwezi poteza mda wangu wa kubishana na wewe kwa hivi vitabu vilivyoandikwa na binadamu kama mimi na wewe.....what i bealieve ni kuishi maisha ya kumpendeza mungu kwa kuacha kitu chochote ambacho unajua ukikifanya kitakuwa ni zambi mbele ya mwenyezi mungu.....,naamini mungu yupo na ninaamini mungu anapenda tuwe na matendo mema.....So, huo ushabiki wa dini na vitabu vyake hapa duniani...,nawaachia watu kama nyie.

1. kwani RC ulizaliwa nayo toka tumboni mwa mama yako? si nayo ililetwa na wazungu?
2. hayo maisha ya kumpendeza Mungu unayajuaje bila kiusoma Biblia?
3. hicho kitu ambacho ukikifanya kitakuwa dhambi mbele za mungiu ulikijuaje bila hizo unazoita "DINI ZA KULETEWA?"
4. utajuaje kuwa Mungu yupo na anapenda matendo mema kama hutaki kusoma na kujifunza neno la Mungu?
5. Sisis uliotuachia kazi ya kukusomea hivyo vitabu vya dini kwa nini unatubishia badala ya kukubali kuwa "kwa kuwa hujasoma, basi hujui na kutusikiliza?"
6. kama vitabu vimeandikwa na wanadamu kwa nini unaviamini kirahisi namna hiyo?

amka ndugu yangu. maarifa si mzigo kwamba unaogopa kuubebea. maarifa ni nguvu. kwa maneno machache uliyotumia kujibu post zangu umedhuhirisha kuwa huna maarifa ya Mungu. amka sasa nuru ikuangazie na Bwana akubariki.

glory to God
 
jamani si vyema kumwangalia mwingira kama mjasrimali pekee, bali pia tujiulize mengine aliyoibuka nayo. Mfano kuna point hapo kwenye bold.

Hata mimi naungana naye kuhoji hapo kwenye bold. Anayejua atusaidie. Mchungaji anaponya watu bila kuwahubiria kwa namna yoyote, ............we njoo, kamata kikombe chako, kwa heri!............ Ni uchungaji gani huu?

Mungu anapewaje utukufu hapo?

Tusaidiane please

glory to god

nina kila sababu ya kusema kuwa judi sio tu haujaongea na mtu aliyeenda kwa babu kupata tiba bali pia haujafika kabisa loliondo na ndio maana unacomment kwa uhakika hayo maneno yako bila kujua nini hasa kinafanyika kabla ya babu kuanza kutoa hiyo tiba. Unatoa comment just kwa kusoma habari za babu kwenye vyombo vya habari pasipo kufanya uchunguzi yakinifu.

Kwa taarifa yako na kwa faida ya wana jf wengi ambao hawajafika ila wanaongea mengi pasipo kuwa na uhakika, ni kwamba babu kabla ya kuanza kutoa tiba yake asubuhi huwa anaiombea dawa akiwa pamoja na wagonjwa wanaokuwepo muda huo wa asubuhi na vilevile huwa anaruhusu watu kama kuna maswali ya aina yoyote, pia fahamu babu yupo user friendly sana kuliko wengi mnavyomfikiri.

Mimi nachoweza kukuambia, kama unaumwa wewe nenda, usije ukawa kama askari wa kijerumani unakufa na tai shingoni, jamani tiba ya babu ni ya uhakika. Kiukweli kabisa wana jf kama unaumwa nenda kapate kikombe cha babu na kama una ndugu yako anaumwa mpeleke kwa babu, mtajiona werevu kwa wakati huu na mkaona maelfu ya watu wanaopanga foleni kwa babu ni wapuuzi.

Naweka msisitizo tena, wana jf achaneni na propaganda, if u are sick, loliondo is not very far.
 
Mtume na Nabii Josephat Mwingira wa Kanisa la Efatha amemuombea mabaya Mchungaji Ambikile Mwasapile anayetoa tiba ya magonjwa sugu katika eneo la Samunge, Loliondo kwamba anapaswa kulaaniwa hadi kufa kutokana na kutoa huduma hiyo.

Mwingira alisema hayo katika mahubiri ya ibada ya Jumapili aliyoyatoa katika Makao Makuu ya Kanisa hilo lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam. “Imeandikwa katika Biblia kwamba,ukipewa bure nawe toa bure. Iweje yeye anauza dawa hiyo, ikiwa Mungu amesema aponye watu. Hakuna sababu ya kuwatoza fedha yoyote wagonjwa.

“Hizi ni roho za kishetani zinazotaka kuwaangusha walio wengi ambao hawamjui Yesu Kristo kwani haiwezekani mtu atumiwe na Mungu halafu hata siku moja asimtaje Yesu. Asitumie Biblia hata kuwahubiria watu wamtumaini muumba wao,”alisema Mwingira.

Mwingira alisema huduma hiyo ni uongo na kwamba haina tofauti na Deci iliyokuja kiujanja ujanja na kuteka watu wengi baadaye walijutia maamuzi yao. “Kama mpakwa mafuta wa Bwana niliyeitwa kwa kusudi lake.

Nailaani Loliondo ife pamoja na Mchungaji wake na itoweke kama Deci ilivyotoweka,” alisema Mwingira. Mwingira alisema Mchungaji Mwasapile ni mwongo, anataka kuwadanganya watu na kuwapoteza kiimani.

Alisema kama alivyoilaani Deci na ikafa, anailaani huduma ya Loliondo ili ife kwa kuwa mchungaji huyo ni roho ipotezayo, inayotaka kuwateka watu walioko gizani na kuwaangamiza. Alisema baadhi ya viongozi tayari wamepigwa ngwara na roho hiyo na kunywa dawa, bila wao kujijua.

“Sitakubali kuendelea kuona roho hiyo ikipoteza watu. Nailaani itoweke Loliondo na iangamie kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti,”alisisitiza. Mwingira alisema haiwezekani kwa mtu aliyeitwa na Mungu kuwahudumia watu wake, baadhi ya watu hao wafe kwenye huduma yake.

“Ni wagonjwa wangapi wamepelekwa kule na wengine wamefariki nyumbani kwake kabisa na wengine njiani, je mlishawahi kujiuliza? alihoji Mwingira.

Mwingira alitoa kauli hiyo siku chache baada Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kulieleza gazeti hili:"Miujiza haiji kwa urahisi hivyo na watu kuponya kiasi hicho, huenda wanaweza kuponywa kwa ‘Illusion’ na baade ikaleta madhara."

Alisema cha msingi watu wanapaswa kuwa makini na serikali pia kwa sababu, wingi wa watu kuponywa huenda baadaye ukaleta vifo vingi zaidi kutokana na dawa yenyewe.

Pengo alisema: “Ninachoamini miujiza haiji kwa urahisi na watu wakaponywa kiasi hicho kwa mara moja, huenda ikawa ni kuponya kwa ‘illusion’ na baadae watu wakapata madhara makubwa.

“Ila sina jibu la kutoa kuhusu uponyaji huo, nabaki tu kushangaa nayayotendeka kwa Mchungaji huyo hadi kufikia watu kuamini kiasi hicho,”alisema.

Pengo alisema huenda akawa ameamua kutumia njia hiyo akawavuta hata wa waumini waingie kwenye imani yake na kuacha dini zao.

Nahisi Mwingira amepotoka na ana chuki binafsi isiyo kifani kwa huyu mchungaji. Kwa wasoma bibilia matamko yake yamekwenda kinyume na maandiko bibilia, usihukumu etc etc. Ningemwelewa ki dogo kama angekuwa constructive kwa kushauri mchungaji aboreshe vipi huduma hiyo. Hivi hiyo kwa hiyo TZS 500 ndio Mwingira awe na asira hivyo? Je huduma wanayotowa wao wameitwa na Mungu? kama ni hivyo kwanini kuna sadaka?
 
i hate mwingira.yuko kifedha zaidi.waumini wamemkimbia anaanza kutapatapa.jiamini baba,wewe si mtume na nabii????hofu ya nini sasa?au hujiamini?au wivu babu anawapiga bao?na utajiri wote alionao mwingira wala haridhiki.mungu atakuumbua tu
 
Hapa ndo tunajua wachungaji wa kweli na mijizi tu inayokanganya waumini kwa maneno na tamaa zao...babu for real!
 
Waseme yote, walaani sana, wafundishe sana. Lakini mimi nitabaki nikisema hivi WAKATI UTAAMUA MAMBO.Tena mi noinavyoona waache wale wanaoiamini hiyo dawa ya babu wanywe na kama wanapona na wapone kabisa.

Hawa/sisi ambao tunamashaka nayo, basi tumuombee ulinzi wa Mungu uwe pamoja naye, na Mkono wa Mungu uhusike katika huduma nzima. Kama ni huduma ya uongo haitadumu!!

Kama ni ya Ukweli hata mkeshe na kufunga siku arobaini mchana na usiku haitakufa ng'o!!! Kwa sababu cha Mungu kinadumu. Kwa mtu anayemwamini Mungu na kumjua huyo Mungu anayemwamudu hapaswi kulaani wala kulumbana kwa sababu ya kitu ambacho kinamhusisha Mungu ndani yake.

Tunadhani Mungu ameshindwa kazi kiasi hicho? Tunadhani Mungu anahitaji wewe na mimi mtetee ktk kazi zile zifanywazo kwa jina lake kiasi hicho?
Tunadhani Mungu haoni uongo au ukweli wa mambo yafanywayo na mwanadamu chini ya jua hili?

Hapana Mungu hajafilisika kiasi hicho, wala hatuwezi kumsaidia kazi hata kidogo. Mwenye ufahamu na amuombee Babu tu, uwepo wa Mungu umzingire. Palipo na nguvu ya Mungu uongo lazima udhihirike tu!!! Na ukweli unadumu daima.

Ndivyo moyo wangu unavyonambia mimi. TIME WILL TELL!!!!
 
sawa LD, TIME WILL TELL.

but we are the salt of the world, we are the light of the world. mji hausitiriki ukuwa juu ya mlima wala watu hawawashi taa na kuiweka chini ya pishi, bali huiweka juu ya kiango ili nuru yake iangaze. vvyo hivo na matendo yetu yapaswa kuonekana na watu ili wamtukuze Baba yetu aliye mbinguni (Mt 5:13-16)

Glory to God
 
Jamani jamani? Askofu mwingira una maanisha kuwa unampinga babu wa loliondo sababu ya kutoza fedha (500/=) au unalingine? Hata sadaka kanisani 500/= haikubaliki. Please find other reasons
 
Haya makanisa yanayojiita ya kiroho usanii mtupu - pesa mbele. Babu mwendo mdundo hadi wakose waumini, bado na Mbunge wetu mama Lwakatare naye aje ya yake.
 
Jamani jamani? Askofu mwingira una maanisha kuwa unampinga babu wa loliondo sababu ya kutoza fedha (500/=) au unalingine? Hata sadaka kanisani 500/= haikubaliki. Please find other reasons

give me a break.... hivi Mwingira ni askofu? hivi vyeo vya uaskofu unaweza kujipa tu? au imekuwa kama kina Prof Maji marefu?
 
Back
Top Bottom