Katika aibada iliyofanyika jumapili ya tarehe 13/03/2011, Mwingira ambaye pia anajiita nabii, alifanya maombi ya nguvu kumuomba Mungu ili Mchungaji Mwasapile wa Loliondo afe. Mwingira ambaye alikuwa akionyesha dhahiri kuwa amekasirishwa na uwepo wa Babu huyo aliwataka waumini wake waombe kwa nguvu zao zote ili babu huyo atoweke katika dunia hii. Muumini mmoja ambaye hakuridhika na maombi hayo nilimsikia akikiri wazi kuwa ameshangaa mtu anayejiita nabii kufanya maombi ya kutaka mtu afe huku akijua wazi kuwa kisasi sio cha Binadamu bali ni cha Mungu. Kitu ambacho kimemuudhi mwingira ni kutokana na ukweli kuwa mchungaji mwasapile anapata umaarufu siku hadi siku kitu ambacho ni tishio kwa makanisa mengi ya aina ya mwingira yanayotegemea shida na matatizo ya waumini wao kujinufaisha. Aidha kwa wale wanaofuatilia mahubiri ya mwingira watakubaliana nami kuwa mwingira anahasira na KKKT kutokana na namna alivyoondoka huko akiwa kama mwinjilisti.
Kwa watu wasiomfahamu Mwingira, kwa kifupi ni kuwa Mwingira alikuwa Mwinjilisti wa kanisa la KKKT jimbo la kibaha kwa miaka kadhaa. Mwingira pamoja kwamba alikuwa mwinjilisti Dayosisi ya mashariki na Pwani, pia kwa nyakati tofauti alikuwa akifanya mikutano ya kiunjilisti ya nje (hadhara) iliyokuwa ikiandaliwa na sharika pia huduma mbalimbali za kanisa hilo. Kwamfano kwenyE miaka ya 1996 alipokuwa anafanya mikutano ya injili katika mikoa ya Ruvuma na Kilimanjaro, Mwingira ambaye sasa anadai ni nabii, aliwahi kutamka na kuapa kuwa kamwe hataanzisha Kanisa kwani huduma aliyoitiwa ni kuhubiri injili. Baada ya kuona itikio la waumuni kwenye mikutano aliyokuwa akifanya, mwingira akaanza tabia ya kuondoka kituo chake cha kazi bila ruhusa ya mchungaji kiongozi wa usharika, hata baada ya kuonywa mara kadhaa akitakiwa afuate utaratibu mwingira alikuwa akikaidi. Baada ya mchungaji kiongozi wake kuchoka na tabia yake ya kufanya mambo bila utaratibu, ilibidi azuie kumpa mshara wa mwezi mwingira kitu kilichomuudhi mwingira na kumfanyia fujo aliyekuwa mchungaji wake jimbo la Kibaha. Baada ya tukio hilo kufika Makao makuu ya Dayosisi ya Mashariki na pwani wakati huo Askofu akiwa Mzee Sendoro, kwa hekima za kimungu mwingira alipewa uhamisho kwenda kutumika Zanzibar kwenye usharikia wa Mwanakwerekwe, jambo hilo lilimuudhi sana mwingira kwani alichokifanya ni kukusanya nguo alizokuwa anazivaa akiendesha ibada (majoho) na kwenda kumtupia mchungaji wake na huo ndiyo ulikuwa mwisho wa mwingira KKKT. Alipoibuka ndiyo amesema kuwa yeye ni mtume tena nabii. Hivyo dunia ielewe sababu za mwingira katika mahubiri yake mengi kukandia KKKT pamoja na watumishi wake. Huyo ndiye nabii aliyeondoka katika huduma moja kwa ugomvi, dharau na jeuri