sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Yes, mimi kiukweli ni mmoja wa watu ambae huu muungano sijawahi kuupenda hata kidogo hasa pale ninapoona uongozi wa bara tunachangiana na wazanzibar lakini huko kwao ni wao wenyewe wanajiongoza, huwa inaniuma mno.
Ila kuna kitu nimetafakari hapa juu ya mchango wa hawa wenzetu wanaposhika madaraka. Nimeona kwamba ,Mwinyi alifanya kitu ambacho huenda tungewapata arais kama wa Bara aliekolezwa na siasa za Nyerere sidhani kama kingetokea, Mwinyi aliweza kuleta vyama vya upinzani mwaka 1992, kumbuka kwamba zamani kulikuwa na vyama pinzani lakini Nyerere alifuta.
Tukija kwa huyu mama, nae ana mambo yake huwa simwelewi lakini ameweza kuwapa ahueni hata wapinzani ambao kipindi kilichopita walipata taabu mno ambayo hawakuistahili, licha ya hivyo swala la katiba mpya tunaona kuna mwanga wa matumaini wa kuwepo katiba mpya japo raisi anaenda hatua kwa hatua, ni siku za mwanzo kabisa za uongozi wake alimtembelea hata Warioba na kunamengi yanaendelea juu ya Katiba,
mfano leo hii nimemuana Shaka akizungumzia katiba na ninamnukuu "Chama cha Mapinduzi tunasisitiza umuhimu wa uwepo wa Katiba mpya kwa kuzingatia mazingira ya sasa na kuona namna bora ya kufufua, kukwamua na kukamilisha mchakato wa katiba mpya kwa masilahi mapana ya taifa na maendeleo kwa ujumla" ukiangalia kwa makini unaona kaisa behind the scenes yupo rais wetu nyuma ya hayo maneno, Hakika ni swala la timing tu inaetwa katiba mpya
Mark my words, Mkombozi ataeliokoa taifa hili atakuwa mzanzibari .
Hata saa mbovu kuna muda inaoneha muda wa kweli