Pre GE2025 Mwinyi kugombea Urais wa JMT mwaka 2025 makamu wake kuwa Dkt. Titus Mlengeya Kamani

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mbona hilo litakuwa jambo jema kabisa.Kiongozi huyu anapiga kazi huko Zenji hadi ningependa aje atufanyie hivyo hivyo huku.
 
Wewe umesikia wapi ?
 
Kwa huyu Dr. Hussein Ali Mwinyi naunga mkono hoja, kura yangu ni moja kwa moja.

Ikiwa tofauti na huyo CCM msinisumbue kuomba kura kwangu kwa kutumia ile njia yenu ya meseji plus 20per!.
 
Sawa.Sawa.
 
Titus Kamani yule aliyeshindwa ubunge akaanzisha vurugu? Video zake ziko youtube.
 
Toka Magufuli afariki kuna watu wanateseka sana.
Kila siku wanakuja na ngonjera mpya!
Eti "tetesi" πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Naomba sana hili litokee, siyo kwakua simwamini SSH Bali nchi hii inahitaji mtu mkali kidogo na ambaye ni mstaarabu kama Mama SSH. Rais wetu ni mzuri ila hawezi vurugu za waovu waliokubuhu nchi hii...In the other hand JPM alikosa calibre ya utulivu na uelewa. Mtu wa katikakti ya SSH na JPM ni HE Mwinyi
 
Hii nafasi hakuna mtanzania mwingine anae iweza isipokuwa hawa?maana tutatoka kwa mwinyi mtakuja kutuambia ridhiwan
 
Dr Hussein Mwinyi Daktari wa binadamu na Rais wa Zanzibari kuwa Rais wa JMT 2025 na mgombea mwenza wake Ni Dr Titus Mlengeya kamani huyu ni waziri mstaafu na Daktari wa Wanyamapori Tanzania
Mkuu @Nigrastratatract, kwanza hongera sana kwa kuwa jasiri kwenye kutoa maoni, kufuatia kuingia kwa dhana ya uchawa, machawa wote kwao 2025 ni Samia tuu!, hivyo mtu ukiibuka na mawazo tofauti, utabezwa sana.

Pili unapotoa opinion serious kama hii, kwanza lazima useme source of such opinion
1. Mawazo yako
2. Umenusa
3. Umeshikwa sikio
4. Umeota ndoto
5. Umesikia Sauti
6. Umeonyeshwa maono
7. Wewe ni mnajimu
8. Wewe ni mtabiri
9. Wewe ni mbashiri
10. Wewe ni nabii

Baada ya kutaja source, you gives reason, why?, kila mtu anajua mgombea urais wa JMT wa CCM 2025 ni Rais Samia, na mgombea urais wa Zanzibar ni Dr. Mwinyi, sasa lazima ueleze kwanini Samia hatagombea kwa nini Dr. Mwinyi na kwanini Dr. Kamani?.

Mimi binafsi nakuunga mkono kwenye hoja zako 2.
1. Kwamba sii lazima Rais Samia awe mgombea urais wa JMT kwa CCM 2025, na hili nimelisema. Watanzania, tuunge mkono 2025 ni zamu ya Mwanamke, ila sio lazima awe yeye bali yule aliyepangiwa na 'YEYE', kama ni yeye aliyepangiwa, then ni yeye!

2. Pia mimi nilimpendekeza Mwinyi 2025 na nilitoa reasons Voices From Within: Japo 2025 Tumepanga Twende na Mwanamke, 2025 Mama Akabidhi Kwanza Mwanamume, Kisha 2030 Ndipo Aje Mwanamke humo nilisema

3. Pia kuna mwana jf mwandamizi, akasema kitu humhusu Dr Mwinyi Kinyang'anyiro cha Urais 2025 kwa tiketi ya CCM: Dkt Mwinyi kuwania Urais wa Muungano?

P
 
Hivi Tanganyika haina mtu anayefaa kuongoza ila atoke Zenji? Utawala wa Kisultani umerudi kwa kasi ya ajabu
 
Si tumesikia samia keshachangiwa na walimu pesa za kuchukua form?
 
Hakuna wa kumzuwia Commander in chief of the armed forces kugombea labda atake mwenyewe !

Hakuna wa kumtingisha Mwenyekiti wa Chama ndani ya CCM labda atake mwenyewe !

Iko vile ilikuwa vile vile na itabaki vile labda mpaka hapo itakapo patikana Katiba mpya bora !

Rasimu ya Katiba ya Mzee Warioba ndio muarobaini !
Ngoja Tusubiri tuone !! πŸ™πŸ™πŸ™
 
Kwanza tupate clarification kuhusu madai ya wapinzani zanzibar eti Mwinyi anafanya ufisadi sana huko Zanzibar. Naona hizi kama njama tu kuwapoteza maboya wanamapinduzi ndani ya chama cha mapinduzi na nchini kwa jumla. Huku bara tuna hazina ya watu tunawajua kwa msimamo wao dhabiti kiitikadi na uwezo wa kuingoza hii nchi. wapinga maendeleo na vibaka wa ubeberu msitupoteze maboya kutaka kutuchomekea watu. Mama hakua na uwezo ila ni rais wa katiba na pia alidakwa haraka na wapinga maendeleo waliyokua wengine wamebwaga manyanga kustaafu kuhofu muziki wa jpm na wengine walitemwa mama akawarudisha. La msingi ni chama kutambua uwezo wa mama kiitikadi na kiutendaji haukidhi. Huku bara tuna hazina ya wanamapindu. Lazima tukubaliane ni aina ya uongozi wa kimapinduzi tu ndio unaweza kuletea nchi hii maendeleo ya kweli. Yaani kuinua umma wa wananchi kutoka umaskini na kunyanyaswa na ubwanyenye wa kimataifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…