tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,040
Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amehitimisha kampeni zake kisiwani Pemba siku ya Jumapili kwa kutoa ahadi kumi za kipaumbele ambazo amesema atazitekeleza endapo atachaguliwa kuendelea kuongoza serikali ya awamu ijayo.
Akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni uwanja wa Micheweni, Dk. Mwinyi amesema hakuna sababu kwa CCM kukosa nafasi ya urais kwani chama hicho kimeleta maendeleo makubwa katika visiwa vya Unguja na Pemba.
Soma pia: Hatuwezi kulinda amani ya mafisadi, watekaji, wauaji na watu wasio malengo mazuri na nchi yetu, Tutalinda amani ya nchi pekee
Amesema kuwa licha ya maendeleo yaliyopatikana katika kisiwa cha Pemba, serikali yake itahakikisha inakamilisha miradi iliyoanza Unguja, ikiwemo ujenzi wa barabara, mabweni, bandari na shule ili kuimarisha huduma za kijamii kwa wananchi.
Kuhusu ajira kwa vijana, amesema serikali yake katika kipindi cha miaka mitano iliyopita imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni 99 isiyokuwa na riba, na katika awamu ijayo ataendeleza mpango huo kwa kutoa fursa zaidi kwa vijana na wanawake.
Akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba 29, Dk. Mwinyi amewahimiza kudumisha amani, umoja na mshikamano wakati wa uchaguzi.