Mawembasa1979
JF-Expert Member
- Feb 26, 2015
- 2,540
- 3,333
Mwinyi Zahera ambaye ni Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga kwa kweli anaijua sana Saikolojia ya Wachezaji. Ikumbukwe kuwa, mara alipopata nafasi ya kazi ya Ukocha Mkuu kwenye Klabu ya Yanga, Klabu ilikuwa na matatizo lukuki hasa ya kiuchumi. Lakini kwa kutambua hilo Kocha Zahera alijitahidi kwendana na hali halisi iliyokuwepo wakati huo. Kitu cha kwanza alichofanya ni kuuomba Uongozi wa Yanga kuweka kambi nje ya Jiji la Dar es Salaam ambapo ilikubaliwa kambi hiyo iwekwe mjini Morogoro.
Ikumbukwe kuwa kabla ya kambi ya mjini Morogoro, Yanga ilikuwa haifurukuti hata kwa Timu za kawaida sana. Katika kipindi hicho tulishuhudia ikifungwa zaidi ya michezo 6 na kwenda sare michezo 2 tu kama sikosei na kushinda mchezo 1.
Kilichowashangaza wapenzi na mashabiki wengi wa mpira wa miguu ni pale alipoanza kuipima Timu yake ya Yanga na Timu za mtaaani na za Daraja la Chini za mjini Morogoro. Mashabiki wengi wa mpira wa miguu wakiwamo wale wa Yanga walianza kumbeza kwa kuona kuwa Kocha huyo hana mbinu za ziada za kuifanya Yanga itishe. Aidha, Timu pinzani hasa Simba zilianza kuibeza Yanga kuwa hata ikichezesha Kikosi C ingeweza kuishinda kirahisi Yanga.
Waswahili wanasema “Muda ni Mwalimu Mzuri” ambapo kadri muda ulivyosogea Yanga ikaanza kuimarika na kuanza kuvifunga vitimu vidogo kila ilipocheza mechi, ingawa wengi waliendelea kubeza kuwa utajipimaje na Mkamba Rangers ya Kilosa na huku unasubiri kuja kupambana kwenye Ligi Kuu na Timu kama Simba, Azam, Mbao n.k. Kwa wachezaji wa Yanga kwa kujifua na timu ndogo iliwajengea uwezo na kupata mbinu mpya za kupambana uwanjani.
Ikumbukwe pia kuwa Wachezaji wenye majina makubwa (Kichuya, Mzamiru, Juma Abdul, Kapombe n.k) kwenye Timu za Simba, Yanga na Azam wengi ni mazao ya Timu ndogo ambazo Yanga ilibezwa wakati ikijipima nazo.
Kwa sasa Timu ya Yanga walau inatisha kiasi kwamba hata Timu pinzani inabidi zijipange vilivyo pindi zinapokuwa na mchezo na Yanga. Yote hayo ni matunda mazuri ya Kocha Mwinyi Zahera.
Mwisho, Mwinyi Zahera pamoja na kuwa na Saikolojia ya kujua matatizo na uwezo wa Wachezaji wake amekuwa hana mzaha kwenye suala la nidhamu ya wachezaji ndani na nje ya uwanja. Amesikika akiwafukuza wachezaji waliochelewa kwenye mazoezi au kuwapa mazoezi magumu ili waendane na wenzao waliopo kambini.