Mwinyi Zahera: Kocha mwenye Saikolojia ya hali ya juu kwa Wachezaji wake

Mwinyi Zahera: Kocha mwenye Saikolojia ya hali ya juu kwa Wachezaji wake

Mawembasa1979

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2015
Posts
2,540
Reaction score
3,333
Mwinyi Zahera ambaye ni Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga kwa kweli anaijua sana Saikolojia ya Wachezaji. Ikumbukwe kuwa, mara alipopata nafasi ya kazi ya Ukocha Mkuu kwenye Klabu ya Yanga, Klabu ilikuwa na matatizo lukuki hasa ya kiuchumi. Lakini kwa kutambua hilo Kocha Zahera alijitahidi kwendana na hali halisi iliyokuwepo wakati huo. Kitu cha kwanza alichofanya ni kuuomba Uongozi wa Yanga kuweka kambi nje ya Jiji la Dar es Salaam ambapo ilikubaliwa kambi hiyo iwekwe mjini Morogoro.

Ikumbukwe kuwa kabla ya kambi ya mjini Morogoro, Yanga ilikuwa haifurukuti hata kwa Timu za kawaida sana. Katika kipindi hicho tulishuhudia ikifungwa zaidi ya michezo 6 na kwenda sare michezo 2 tu kama sikosei na kushinda mchezo 1.

Kilichowashangaza wapenzi na mashabiki wengi wa mpira wa miguu ni pale alipoanza kuipima Timu yake ya Yanga na Timu za mtaaani na za Daraja la Chini za mjini Morogoro. Mashabiki wengi wa mpira wa miguu wakiwamo wale wa Yanga walianza kumbeza kwa kuona kuwa Kocha huyo hana mbinu za ziada za kuifanya Yanga itishe. Aidha, Timu pinzani hasa Simba zilianza kuibeza Yanga kuwa hata ikichezesha Kikosi C ingeweza kuishinda kirahisi Yanga.

Waswahili wanasema “Muda ni Mwalimu Mzuri” ambapo kadri muda ulivyosogea Yanga ikaanza kuimarika na kuanza kuvifunga vitimu vidogo kila ilipocheza mechi, ingawa wengi waliendelea kubeza kuwa utajipimaje na Mkamba Rangers ya Kilosa na huku unasubiri kuja kupambana kwenye Ligi Kuu na Timu kama Simba, Azam, Mbao n.k. Kwa wachezaji wa Yanga kwa kujifua na timu ndogo iliwajengea uwezo na kupata mbinu mpya za kupambana uwanjani.

Ikumbukwe pia kuwa Wachezaji wenye majina makubwa (Kichuya, Mzamiru, Juma Abdul, Kapombe n.k) kwenye Timu za Simba, Yanga na Azam wengi ni mazao ya Timu ndogo ambazo Yanga ilibezwa wakati ikijipima nazo.

Kwa sasa Timu ya Yanga walau inatisha kiasi kwamba hata Timu pinzani inabidi zijipange vilivyo pindi zinapokuwa na mchezo na Yanga. Yote hayo ni matunda mazuri ya Kocha Mwinyi Zahera.

Mwisho, Mwinyi Zahera pamoja na kuwa na Saikolojia ya kujua matatizo na uwezo wa Wachezaji wake amekuwa hana mzaha kwenye suala la nidhamu ya wachezaji ndani na nje ya uwanja. Amesikika akiwafukuza wachezaji waliochelewa kwenye mazoezi au kuwapa mazoezi magumu ili waendane na wenzao waliopo kambini.
 
"kwani tunacheza na wanawake" Coach Zahera
Haha haa ..
Nilisikia hiyo kauli wakati anajibu kwanini wachezaji wa timu yake wanaonekana kuchoka kipindi cha pili?
Nikatamani nimuulize ukicheza na wanawake michezo mingine ile mwanaume hauchoki?

Ingekuwa Ulaya au Marekani angejikuta matatani na feminist kwa kauli yake hii. Amuulize Amre Can wa Juve alipojaribu kumtetea CR7 kuhusu redcard yake. Nae alitumia kauli inayofanana na hii.
 
Wasiwasi wangu mkubwa huyu kocha anaenda kuzipoteza hizi sifa zote tar 30
 
Baada ya kuwadhishia kipigo kizito.. 30/09 ndo itakua siku yake ya mwisho kufanya kazi Ndala Microfinance.
 
Mawembasa1979 Prince Kunta issue ya Masoud Djuma ni complicated sana, ndo mana tangu imeanza, sikuwahi kuizungumzia.

Narudia tena.. Kutokana na matatizo ya kiufundi yaliyotokea 30/09/2018.. 'dozi' yenu tumeihifadhi mpaka tutakapokutana tena.
 
Mawembasa1979 Prince Kunta issue ya Masoud Djuma ni complicated sana, ndo mana tangu imeanza, sikuwahi kuizungumzia.

Narudia tena.. Kutokana na matatizo ya kiufundi yaliyotokea 30/09/2018.. 'dozi' yenu tumeihifadhi mpaka tutakapokutana tena.
Masoud kaona isiwe taaabu karudi hapo kariakoo mitaa ya Jangwani na Twiga ha ha ha!!!
 
Juzi kati nilikuwa nikiangalia clip moja kwenye YouTube nikamsikia Kocha wa Yanga Mwinyi Zahera akijibu maswali ya waandishi wa Habari. Mojawapo ya swali aliloulizwa ni Kuhusu ubora wa Ibrahim Ajibu na kwa nini hachaguliwi ili acheze Timu ya Taifa. Bila kupepesa macho Mwinyi zahera alijibu kuwa Ajibu ni mchezaji mwenye akili sana awapo uwanjani. Hata hivyo hawezi kuitwa kuchezea Timu ya Taifa kwa sababu hachezi mpira wa nguvu. Kwa kweli hata mimi nakubaliana na Kocha Mwinyi zahera Ajibu inabidi aongeze nguvu kwa kukaba na kucheza mpira wa nguvu. La sivyo mpira wa kulipwa wa maana atausikia na kuuona kwenye TV.
 
Tulisha jiandaa kuzika lakini tukiwa mochwari maiti (Yanga) ikapiga chafya, zoezi likashindikana
Habari za siku mkuu!!! Vipi Mwinyi Zahera ameshafungasha kwenda kwao kama ulivyotabiri au ilikuwa ni pilot study yako ya kurithi mikoba ya Sheikh Yahaya?
 
Back
Top Bottom