Mwinyi Zahera: Yanga walitaka kumpeleka Clement Mzize Singida kwa Mkopo, Mimi nikamshauri Nabi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
1754983153154.png

Mwinyi Zahera, kocha wa zamani wa Yanga, amesema Yanga walikuwa tayari kumpeleka Clement Mzize Singida kwa mkopo, lakini yeye alimshauri kocha Nabi asikubali. Ameongeza kwamba walitaka kumtoa Mzize wakati hajaanza hata mazoezi na timu kubwa, na hata baada ya barua kutoka Marseille, bado msimamo wa Yanga ilikuwa kumpeleka Singida;

"Yanga walishataka kumpeleka Clement Mzize huko Singida kwa mkopo na tayari walishamuingiza kwenye system ya TFF ila ni Mimi nikamwambia Nabi usikubali huyo Mtoto aende Singida na walitaka kumtoa wakati hajafanya hata mazoezi timu kubwa, hata Marseille walipotuma barua kumtaka wao wakasema tumpeleke Singida tu maana Wachezaji watapatikana wengine"

Chanzo: ITV
 
Kwa mara ya kwanza katika zama hizi ITV wameweza kuwa mbele (exlusively) kutoa habari katika jambo linalo trend.
ITV tulishawazoea kuja na habari za michezo ya mbuzi, bao na marudio ya habari zilizopitwa na wakati.
 
Yanga wana historia ya kuwaonea wivu wachezaji wao...

Hata Msuva asingekomaa huenda tusingemuimba leo...
 
Labda walikuwa wanammegea pande Bwana Fedha maana yupo pande zote za shilingi. Haya mambo ya usajili yana magumashi mengi sana.

Mashabiki wa Yanga walikuwa wanamkataa Mzize misimu miwili tu hapa iliyopita.
 
Imebaki historia kwa sasa ni mali ya Yanga wao ndiyo watakaoamua kumuuza
 
Mwinyi Zahera, kocha wa zamani wa Yanga, amesema Yanga walikuwa tayari kumpeleka Clement Mzize Singida kwa mkopo, lakini yeye alimshauri kocha Nabi asikubali. Ameongeza kwamba walitaka kumtoa Mzize wakati hajaanza hata mazoezi na timu kubwa, na hata baada ya barua kutoka Marseille, bado msimamo wa Yanga ilikuwa kumpeleka Singida;

"Yanga walishataka kumpeleka Clement Mzize huko Singida kwa mkopo na tayari walishamuingiza kwenye system ya TFF ila ni Mimi nikamwambia Nabi usikubali huyo Mtoto aende Singida na walitaka kumtoa wakati hajafanya hata mazoezi timu kubwa, hata Marseille walipotuma barua kumtaka wao wakasema tumpeleke Singida tu maana Wachezaji watapatikana wengine"

Chanzo: ITV
Haya maneno unaweza kuwaambia Man U kwa Ganacho au wao hawajui thamani ya mchezaji? Yaani timu inayomiliki mchezaji uanze kupangiwa cha kufanya? Wangempeleka Singida Kwa mkopo Nani angeenda kupinga mahakamani? Kama Zahera alimshauri Nabi alimshauri kama nani kwa Yanga? Nabi si alikuwa sehemu ya uongozi wa Yanga kuhusu hatima ya Mzize?
 
Yanga wana historia ya kuwaonea wivu wachezaji wao...

Hata Msuva asingekomaa huenda tusingemuimba leo...
unajua lolote kuhusu mkataba?
unajua lolote kuhusu biashara ya wachezaji?
una comment kama mtu wa kilungule bhana
 
Kwa mara ya kwanza katika zama hizi ITV wameweza kuwa mbele (exlusively) kutoa habari katika jambo linalo trend.
ITV tulishawazoea kuja na habari za michezo ya mbuzi, bao na marudio ya habari zilizopitwa na wakati.
Na mimi nimeshangaa. Wamepataje pataje Zahera hao ITV mana siyo kawaida yao kuwa habari kama hizi za michezo! Wenyewe ITV wapo vizuri kwenye habari za kitaifa tu!
 
Haya hakwenda Singida na sasa mchezaji halali wa Yanga. Mnataka kusema nini nyie?
Umewaza kama mimi. Sawa hakwenda Singida! Na hata sasa Esperance de Tunis wameweka mezani dau la dola milioni 1 za Kimarekani (Tsh. Bilioni 2.6) kutaka kumnunua.
Kwa hiyo Mwinyi Zahera anataka mgao iwapo atauzwa, au na yeye anataka aonekane ni mtu muhimu kwenye maisha ya Mzize?

Na mpaka muda huu matokeo yako hivi; Jasmine Fc 0 Yanga Sc 3!
 
Watu wanataka kukuza mambo kipuuzi puuzi sana. Huyu Zahera hatakagi jambo limpite anajiona kama yeye ndio master kwa kila kitu.

Sasa sisi hatukatai ni kweli Mzize alikua aende Singida ila hakwenda kwa ushawishi wake. Yeye anataka tufanye ni nini?
 
YANGA shikilieni hapo hapo, kuna shule ya muhimu sana mnatoa hata Mzize asipouzwa kabisa achilia mbali kuuzwa kwa bei juu. Ni rejea nzuri sana kwa wazawa kuhusu mikataba. Ulisaini nini na unataka nini? Hili ni shamba darasa la wachezaji wazawa baada ya lile shamba darasa la Fei alipoonyesha umuhimu wa vipengele vya kununua mkataba wako iwapo hutaki kuendelea na Club.
 
Zahera alikuwa Mkurugenzi wa ufundi pale Yanga kipindi hicho. Kwa hiyo ilikuwa wajibu wake kushauri, na alikuwa sehemu ya uongozi.
 
Back
Top Bottom