Na Dustan
Shekidele,Morogoro.
Ikiwa takriban siku 40
tangu baba yao, Dk.
Ephraim Njawala
Mwampamba, Mhadhiri
wa Chuo Kikuu cha Kilimo
Cha Sokoine (SUA) afariki
dunia, mwanaye Mwisho
Ephraim Mwampamba
ameburuzwa mahakamani
na kaka yake, Robert
Ephraim
Mwampamba'Ras',
Jumatatu iliyopita.
Kesi hiyo namba 197/2016
ilisikilizwa katika
Mahakama ya Mwanzo
Chamwino iliyopo
Mazimbu mkoani hapa,
ambapo Robert
alimburuza mahakamani
hapo mdogo wake huyo
waliyechangia baba,
akimtuhumu kumtukana
matusi ya nguoni huku
sehemu kubwa ya matusi
hayo yakiwa ya kibaguzi.
Kabla ya kufikishwa
mahakamani hapo,
Mwisho alitokea
mahabusu alikolala kwa
siku moja ambapo baada
ya kesi kusikilizwa, alipata
dhamana huku ikidaiwa
kuwa kesi hiyo imemkalia
vibaya kutokana na
ushahidi unadaiwa upo.
Akisoma kesi hiyo
mahakamani hapo,
Hakimu Amina Chungulu
alidai Mwisho
anatuhumiwa kumtukana
matusi ya nguoni
(hayaandikiki gazetini)
kupitia namba za simu
(tunazihifadhi) ambayo
inaaminika inamilikiwa na
Mwisho Mwampamba.
Mwisho alipoulizwa na
hakimu huyo alikana
kutenda kosa hilo na
Robert alipoulizwa kama
ana ushahidi ndipo
aliposema anao wa meseji
hizo kwenye simu yake.
Hakimu huyo aliahirisha
kesi hiyo hadi Aprili 11,
mwaka huu huku Robert
akitakiwa kufika
mahakamani hapo na
meseji hizo kama
ushahidi.
Aidha, Hakimu Amina
alisema dhamana iko wazi
kwa mshitakiwa;
mdhamini mmoja na
shilingi laki 4 ambapo
kaka mwingine wa Mwisho
aliyezaliwa naye baba
mmoja na mama mmoja,
lsambe alimdhamini
mdogo wake huyo.