Kuna tabia inazidi kukuwa ya waTz kupenda wenzao wawe na maisha mabaya au wafulie. Huu mjadala hapa ni ushaidi sielewi ni maisha yamekuwa magumu sana au ni vipi.
Mwisho ajawai kuwa na maisha mazuri ila watu wamempa utajiri pia mwisho ajawai kuwa na maisha ya dhiki ila watu wamempa kufirisika. Mwisho always ana maisha ya kawaida tu na ni mtu simple sana labda kinachowasumbua watu ni ushombe wake wake wakampangia mpaka maisha anayotakiwa kuishi.
Kwa sasa ameamua kukaa pembeni na maswala ya media kwa kuwa ayamlipi, ana familia yake ana ishu zake nyingine anafanya kaamua kuwa baba haswa. Wala ajafulia maisha yake ni yale yale.
Kaka yake Isambe namfahamu pia rafiki yangu alikuwa na mdogo wake marehemu kwa sasa walikuwa wana date so namfahamu kiasi. Ni kama Mwisho mtulivu na yupo simple hana makuu anafanya kazi ya mshahara wa six figures lakini anaenda kazini na baiskeli ilihali wenzake wana magari ya kufuru.
Nafikiri watu mumuelewe tu Mwisho ni watu wapo hivyo kwao wapo simple sana wanaishi kama watu wa uswazi ilihali wamekulia uzunguni forest hill moro na mama yao ni mzungu kabisa ila alishindwa kuwashep waishi kizungu.