Baada ya kufuatilia interview nzima(part 1 - 3 )ya mwisho mwampamba nimekuja kugundua jamaa ni mtu poa sana tena sana, halafu ni mtu anaejielewa kuliko mastaa wengi wa kibongo.
Ukisikiliza interview ya mwisho(part 3) ameongea mengi sana hasa changamoto mwanaume anaweza kupitia ila aliweza kuzishinda kwa kishindo.
Kwa changamoto alizopitia Mwisho, angekua star mwingine nahisi angeingia kwenye madawa moja kwa moja.
Anakwambia pamoja na u staa wote aliokua nao, aliweza kupanga chumba kimoja(ghetto) mitaa ya sinza na pisi kali zilikua zinatoa mpaka ofa ya kutaka kumpangia nyumba nzima ila anasema si kwamba alikua hana uwezo wa kupanga ila ni maamuzi tu.
Anasema kuna kipindi alipitia depression mbaya mpaka akawa hana hata uwezo wa kumiliki simu ya kitochi lakini alishinda.
Aliacha sigara na pombe kwa siku moja tu baada ya kukaa na kuwaza watoto wake watamchukuliaje huko Namibia kama mama yao anawalisha sumu kwamba baba yenu ni mlevi mbwa halafu wakija wakakuta ni kweli ni mlevi? Anasema alipowaza kuhusu watoto aliamua bila kupepesa kuacha kila kitu na kuanza maisha upya.
Leo hii anapiga dili nyingi tu za halali na hela ya hapa na pale hakosi.
Nawashauri ndugu zangu sikilizeni interview yake hasa part 3 muone ni namna gani mwanaume anaweza kukabiliana na changamoto.
Hii interview ni ndefu lakini it worth it.
View: https://youtu.be/rje8jFCdV2w?si=1ED6LPSBjwa9U4XM