Uchaguzi 2020 Mwita Waitara achanganyikiwa, awashtaki wanaompinga kwa wazee wa kimila wa koo yake

Uchaguzi 2020 Mwita Waitara achanganyikiwa, awashtaki wanaompinga kwa wazee wa kimila wa koo yake

nokwenumuya

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2019
Posts
820
Reaction score
2,896
Hali ya Mwita Waitara katika jimbo la Tarime Vijijini imezidi kuwa mbaya sana na hivi sasa amezidi kuishiwa pumzi. Katika hali isiyo ya kawaida imebidi aende kushitaki kwa Wazee wa kimila wa koo ya Wairegi kuhusu watu wanaompinga wanaotokana na koo hiyo.

Kwanza ameonyesha ubaguzi wa koo kuwa yeye lazima aungwe mkono na watu wote wanaotoka katika koo yake ya Wairegi.

Lakini hiyo ni tabia yake ya muda wote, ni MBAGUZI.

IFUATAYO NI MESEJI ALIYOANDIKA RUSTER NYAIKOBA KATIKA KUNDI LA KURYA WHATSAAP GROUP BAADA YA KUPIGIWA NA MMOJA WA WAZEE HAO, NAOMBA UISOME:-

Leo nimepigiwa simu na Mzee mmoja wa Kimira akitaka Maelezo kwa nini tunampinga Waitara.

Nikamuuliza nani amekwambia kuwa Ruster,Ngemo,Martin,Gichogo,Gasaya na Bisendo tunampinga NW?..Akaniambia kuwa Waitara alienda kwao kutoa Malalamiko.

Nikamuuliza amewahi kuwaambia alichotufanyia Wakurya hapa Ukonga?.Akasema wanaskia Tetesi.

Nikamuuliza upo Tayari nikulipie Tiketi uje Ukonga kwa Niaba ya Kimira ili ujue Mapungufu ya huyo Waitara?..Akasema yupo Tayari.

Kwa Taarifa Waitara ameomba tuitwe haraka sana na Wazee ili tusiendelee kumharibia Kampeni za kuwa Mbunge Tarime Vijijni.Hata hivyo kwa Niaba ya wenzangu nimetoa Maelezo ya kushiba kwa Mzee huyo,ambaye pia ameonesha Maskitiko mkubwa.

Aidha nimemwambia hakuna siku tutamuunga Waitara Mkono kwa kuwa tunajua Madhaifu anayetoka kuleta Tarime V.

Nikamkumbusha kuwa mimi ni Mwanachadema,hivyo nina haki ya kumpinga Mwanaccm yeyote hata kama ni Mzee Wangu.Finaly nikamwambia tupo Tayari kujieleza,hivyo Waitara atitumie Tiketi ya Ndege kwenda na kurudi Dar..

Nikasisitiza hiki ni Kipindi cha Corona,hivyo hatutahitaji kusafiri na Mabasi..Nimemshangaa sana Mh.Waitara.

Kuna siku ataenda kumshitaki Aloyce Nyanda wa Star TV kwa Wazee wa Kimira,sio kwa Akili hizi.
 
CCM wanamuogopa sana Mwita Waitara.

Ameanza kampeni kabla ya wakati lakini si Dr Bashiru wala Komredi Polepole mwenye ujasiri hata wa kumuonya tu.

Labda tuwasubiri Takukuru maana huko kwa wazee wa mila anapelekwa na gari ya serikali inayoendeshwa na dereva wa serikali.
 
Sasa Waitara atachanganyikiwaje? Yeye ni Mbunge wa viti maalumu jimbo la ukonga? Sasa TARIME na ukonga wapi na wapi?
 
Back
Top Bottom