Mwita Waitara adai elimu bure maana yake ni wanafunzi kulipiwa ada na Serikali, mzee Mwamakula amshangaa na kusema mawaziri hawana maono

Mwita Waitara adai elimu bure maana yake ni wanafunzi kulipiwa ada na Serikali, mzee Mwamakula amshangaa na kusema mawaziri hawana maono

Kwa mujibu wa tafsiri ya leo "Ni mzazi/mlezi kutotozwa ada!"
Lakini kwa tuliosoma enzi za "Elimu bure" ya kiukweli ilikuwa: Hakuna ada,nauli unalipiwa,chakula ,matibabu,vitabu na vinginevyo muhimu hulipii! Hata hao wanaodanganya wanatoa elimu bure wanajua. (Labda kina Jafo,Kairuki,Waitara,Mavunde) hawajui kwani ni "mawaziri watoto)"
Umejibu vizuri.........elimu bure ni pamoja na kupewa warrant ya kusafiria wakati ule Railway na Kamata!
 
Wanataka maziwa lkn kunenepesha ng'ombe awataki.
Baba lao na mama lao wote walikuwa walimu wanajua shida na changamoto za ualimu eti leo wamewasahau walimu.Mwalimu ndo ilitakiwa awe ndo anaongoza kulipwa maslai na mazingira bora ili akili ikae sawa,sio yuko darasani anawaza maandazi yake yataishaje,au anawaza wateja wake wa bodaboda kijiweni,walimu ufikia kuwa waendesha bodaboda ili wajikimu tunajenga taifa la kizazi gani,kazi ya mwalimu yatakiwa iwe kumwaga material tu.
 
ELIMU BURE NI KIZUNGUMKUTI... HAKUNA CHA ELIMU BURE WALA NINI UJINGA MTUPU!
 
Saizi kuna waropokaji,sikumbuki lini nimeangalia taarifa ya habari ya bongo maana ni kichefuchefu sana,unaona viongozi wanatoa matamko ya kijinga,hotuba za kitoto,wanatukana watu ovyo.......yaani unajiuliza hivi hawa wana hata abc za kuwa viongozi?
Zitoke wapi,walioweka semina elekezi awakuwa wajinga,cv na kinga ya utumbuzi ni bidii yako binafsi ya kumsifia mungu wao na kulitajataja jina tukufu kila upatapo wasaa wa kuwa mbele ya kamera,
 
Naibu waziri wa Tamisemi anayeshughulikia miundombinu ya elimu ya msingi na sekondari mwalimu Mwita Waitara amesema maana ya Elimu Bure ni wanafunzi kulipiwa ada na serikali.

Waitara amedai kuwa wananchi wengi wanachanganya mambo kwa kudhani kuwa ujenzi wa miundombinu ya elimu yakiwemo madarasa, maabara, madawati, vyoo nk ni sehemu ya mpango wa elimu bure na hivyo hawapaswi kuchangia.

Naye kada wa CCM ambaye ni afisa wa polisi mstaafu mzee Mwamakula amemshangaa waziri Waitara na kusema kwa hakika mawaziri wa awamu ya 5 hawana maoni kabisa.
Mzee Mwamakula amesema anashindwa kuelewa majukumu ya waziri wa Utawala Bora endapo hata swala la ujenzi wa madarasa ya watoti linakuwa na mjadala wa kitaifa wakati linaeleweka kabisa ni jukumu la nani.

Chanzo: Malumbano ya Hoja ITV
Hivi kuna mwanafunzi ana lipiwa ada na serikali?? Mbona hawa mwendo kasi wa JPM hawajielewi? Juzi nimemsikia DC akiagiza kila mtoto aende na mahindi debe moja bado tuna ambiwa elimu bure ni kulipia wanafunzi ada.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sameheni bure maneno ya waitara, 'viroba na vibapa' ni hatari sana ktk ustawi wa afya ya akili za watu.
 
maendeleo sio ndege tu
elimu bure inaanzia wapi na kuishia wapii
 
Back
Top Bottom