PreGE2025 Mwita Waitara: ningekuwa na uwezo ningefuta Kamati ya siasa ya Musoma Mjini, Kamati ya siasa ya Tarime

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
"Ukitaka kufanya siasa safi hapa Mkoa wa Mara lazima tuambiane ukweli na kama ni jipu tulitoboe, tulikamue, tutoe kiini na mimi ningekuwa na uwezo ningefuta Kamati ya siasa ya Musoma Mjini, ningefuta Kamati ya siasa ya Tarime. Haki ya Mungu ningefuta. Its very Unfair. Hata kama hawamtaki Mbunge basi wapende maendeleo aliyoyasemea kwenye Bunge la Tanzania, penda huduma anazotoa kwa watu wake."

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mshikamano Manispaa ya Musoma aliposhiriki kwenye Mkutano wa Mbunge wa Jimbk la Musoma Mjini Mhe. Vedastus Mathayo.

Akisisitiza kuwa Viongozi wa Kamati hizo tayari wana wagombea wao, ameeleza kuwa anaamini katika mchujo wa wagombea, Kamati hizo hazitawatendea haki yeye na Mbunge wa Musoma Mjini, akisema hayupo tayari kukubaliana na maamuzi yatakayotolewa.

chanzo:jambo tv
​
 
Huyo Waitara anyamaze tu, ajue alipata ubunge kwa taratibu kurukwa baada ya kutumika kwenye zile siasa chafu za kuunga mkono juhudi. Kama ni kuwasemea wananchi, mtu yoyote akienda bungeni atafanya hivyo sio lazima awe yeye. Mwisho wa kutumika umefika, sasa ndio awe mwanaccm kweli kama kweli alifuata itakadi na sio madaraka.
 
Huyu anajua kwenye kura za maoni ndani ya chama mbogamboga hatoboi
 
Yeye nani, alipotoka chadema kuhamia ccm hakujua kwamba walikuwepo au kwakuwa alibebwa juu kwa juu?

Mbeleko imechanika sasa analialia, kuna maisha bila ubunge.

Alijiamini kafanya kazi kubwa na yeye ndiye mbunge wa kudumu au hakuelewa ubunge unatokana na taratibu za chama?

Akumbuke SSH alisema uchaguzi ujao ataleta wagombea wanao kubalika, akiona hivyo yeye hakubaliki, atulie mwenyekiti sasa anasuka team yake.

Yeye alikuwa team ya mwwnyekiti aliyepita marehemu JPM.
 
Aache kulia kulia! Kwani lazima achaguliwe yeye tu na huyo mwenzake kila awamu!
 
Kumbe anapenda Reforms, Ili awe na uachaguzi wa haki sasa kwanininalikataa vya CHADEMA
 
Waitara ameanza kutoa mlio mapemaa! Kazi ipo kwenye kura za maoni
 
"Ukitaka kufanya siasa safi hapa Mkoa wa Mara lazima tuambiane ukweli na kama ni jipu tulitoboe, tulikamue, tutoe kiini na mimi ningekuwa na uwezo ningefuta Kamati ya siasa ya Musoma Mjini, ningefuta Kamati ya siasa ya Tarime. Haki ya Mungu ningefuta. Its very Unfair. Hata kama hawamtaki Mbunge basi wapende maendeleo aliyoyasemea kwenye Bunge la Tanzania, penda huduma anazotoa kwa watu wake."

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mshikamano Manispaa ya Musoma aliposhiriki kwenye Mkutano wa Mbunge wa Jimbk la Musoma Mjini Mhe. Vedastus Mathayo.

Akisisitiza kuwa Viongozi wa Kamati hizo tayari wana wagombea wao, ameeleza kuwa anaamini katika mchujo wa wagombea, Kamati hizo hazitawatendea haki yeye na Mbunge wa Musoma Mjini, akisema hayupo tayari kukubaliana na maamuzi yatakayotolewa.
View attachment 3369636
chanzo:jambo tv
​
Kwani ccm inataka ukweli? Wewe wamekwishakukula kichwa
 
Akisisitiza kuwa Viongozi wa Kamati hizo tayari wana wagombea wao, ameeleza kuwa anaamini katika mchujo wa wagombea, Kamati hizo hazitawatendea haki yeye na Mbunge wa Musoma Mjini, akisema hayupo tayari kukubaliana na maamuzi yatakayotolewa.
Ameanza kutafuta visingizio vya kutoswa mapema mno.
 
No reforme No election IPO na inatakiwa Kila eneo Kwa level tofauti.Huyu tayari anataka reforms za uchaguzi ndani ya chama chake
 
Ccm hawakutaki
Silaha yako ya kumshambulia
Heche imeisha,vita unayo ndani mwako

Ova
 
"Ukitaka kufanya siasa safi hapa Mkoa wa Mara lazima tuambiane ukweli na kama ni jipu tulitoboe, tulikamue, tutoe kiini na mimi ningekuwa na uwezo ningefuta Kamati ya siasa ya Musoma Mjini, ningefuta Kamati ya siasa ya Tarime. Haki ya Mungu ningefuta. Its very Unfair. Hata kama hawamtaki Mbunge basi wapende maendeleo aliyoyasemea kwenye Bunge la Tanzania, penda huduma anazotoa kwa watu wake."

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini Mwita Waitara wakati akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kata ya Mshikamano Manispaa ya Musoma aliposhiriki kwenye Mkutano wa Mbunge wa Jimbk la Musoma Mjini Mhe. Vedastus Mathayo.

Akisisitiza kuwa Viongozi wa Kamati hizo tayari wana wagombea wao, ameeleza kuwa anaamini katika mchujo wa wagombea, Kamati hizo hazitawatendea haki yeye na Mbunge wa Musoma Mjini, akisema hayupo tayari kukubaliana na maamuzi yatakayotolewa.
View attachment 3369636
chanzo:jambo tv
​
NO REFORMS NO ELECTION
 
Back
Top Bottom