The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Nawaambia kila siku uzeni meno ya tembo mjenge uzio kwenye Vijijini vinavyopakana na hifadhi kuzuia binadamu na Wanyamapori hamsikii..Namsikiliza mbunge wa Tarime vijijini ana hoja nzito juu ya raia ambao ni wananchi wa jimbo la Tarime vijinini anatoa ushahidi wa majina na ya raia waliopigwa risasi na waliouwawa na waliojeruhiwa.
Blah blah za George Simbachawene zikataka kumziba Waitara. Spika akaomba ushahidi juu ya tuhuma hizi. Mwita Waitara kasema anaoushahidi na atauwakilisha.
Migogoro ya ardhi kati ya wananchi jimbo lake na hifadhi ya Serengeti ni mkubwa. Na askari wa Tanapa wanatuhumiwa kuua raia wa wakazi wa Tarime vijijini.
Mwita anatakiwa kuwasilisha ushahidi ifikapo siku ya Jumanne.