Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Vyovyote vile, lakini hii haibatilishi kwamba alio wataja ni mafisadi papa na ushahidi upo hata humu JF umeanikwa nje nje. They have to face it regardless of their race, they are thieves! We cant let them kwa kutafuta vijisababu kwamba hoo tunabaguliwa, nooo, kwani wako wahindi wangapi mbona wao hawajatajwa?
 

Labda wewe ndiye..
 

Hawa walikuwa wanajulikana kabla hata ya Mengi kuwarusha hewani,
wanaotafuta umaarufu ni wakina Lipumba kwa kupinga ukweli unaojulikana ili mradi aonekane nae amezungumza
 
Hawa walikuwa wanajulikana kabla hata ya Mengi kuwarusha hewani,
wanaotafuta umaarufu ni wakina Lipumba kwa kupinga ukweli unaojulikana ili mradi aonekane nae amezungumza

Kumbe Mengi nae kadandia!

Mangi Mengi hajatulia kabsaaaa, anahitaji kupepewa. Asipoonekana ITV kwa muda hajisikii visuri aisee. Msee misifa achia fijana mbeee.
 
Kweli usilojua ni kama usiku wa giza nene inanikumbusha mwaka fulani watamzamia tuliandamana kupongeza ufaransa kwa kukataa kuwauzia makaburu nyambizi tuliipongeza ufaransa ni kitendo cha kishujaa.lakini ukweli ufaransa ilikuwa inawaadhifu makuburu kwa kuwauzia wamarekani dhahabu.mgogoro huu ulimfanya dr kissinger kutembelea tz, hatimaye afrika ya kusini.sasa vita hivi mengi vs rostam na wengine havina tafauti na hivyo nilivyovieleza.wa tz wepesi kushawisha kwa muhubiri ya askofu yeyote hata kama hajui maandiko matakatifu.matokeo yake tuna dini zaidi ya elfu tatu hapa nchini
 
Mwezi uliopita kuna msamaria mwema alitoa taarifa kwa mamlaka ya chakula na madawa kuhusu uwepo wa dawa feki za malaria.
Mtu huyo alizawadiwa na serikali ikazi burn dawa hizo.

Mbona kwenye hili la Mengi kuna kigugumizi na matokeo yake mawaziri wanawatetea watuhumiwa????

Mzee wa Upako (Mch Lusekelo) jana nae alihoji, " iliyetoa taarifa za DECI alizawadiwa na Deci ikashughulikiwa, iwaje Mengi atoe taarifa halafu ashughulikiwe yeye???
 
Tafadhali Mode futa hii topic haina tija kwa taifa.
 
Wahenga walisema " Amlipaji wa mpiga zumari ndie atakae chagua wimbo..." acheni ITV na Nipashe wa dance ngoma ya boss wao...
 
Hoja ni moJa tu... UFISADI-PAPA!!!.

Hao Vijana wa CCM- Tabora, kusafiri all the way from Tabora hadi Dar kwaajili ya kumtetea fisadi ni jambo la hatari sana....!

Mmepewa nauli na nani? Mmefikia wapi? Mnakula nini hapo Dar?.. Just for that goal? Tabora kuna hospitali ngapi, shule ngapi, na barabara ngapi, mkaacha kuongelea matatizo hayo, mnantetea FISADI PAPA, ANAYEPELEKA HELA ZENU INDIA???

Vijana...!! Are you Vijana... Na sio Wazee!!! Kweli nyie vijana, whom i officially call you VIBARAKA, mnatuachia mzigo mkubwa sana sisi wapenda Utawala Bora!
 

Anayeingiza habari za uhindi ndiye anaye water down hii issue na kuwapa msemo. Kulikuwa hamna haja ya kuingiza uhindi, hawa ni mafisadi na waandamwe kama mafisadi, mkiingiza uhindi mnawapa msemo kwamba wanaandamwa kwa sababu wao ni wahindi.
 

Kwahiyo unapendekeza angechomeka mtanzania asiye na asili ya kiasia kwenye top 5 yake kwa lengo la kuepuka maswali mengi tu?

Kama unahisi wapo watanzania wasio na sili ya kiasia ambao walistahili kuwa kwenye top 5 yake, jisikie huru kupendekeza top 5 yako mbadala
 
Last edited:

Mpendwa, hiyo maana sipati picha umeifikiaje. Wengine uelewa wetu mdogo, labda utusaidie kuelewa ni vipi hicho ndio kilichomaanishwa.

Kwa uelewa wangu mdogo, kusema Zitto ni mwizi hakuwezi kamwe kumaanisha wabunge wote ni wezi. (Of coz siamini kwamba Zitto ni mwizi; huo ni mfao tu. Na hata kama ningekuwa naamini hivyo, vile vile hakuwezi kuamaanisha kwamba Zitto ni mwizi; mantiki101).
 
kutoka nipashe nimemalizia sentensi ambayo dikteta alikuwa hataki kumalizia

Pia, hafla hiyo licha ya kumpongeza Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi kwa ujasiri wa kutaja Watanzania wenye asili ya kiasia na madhara yao hadharani, wabunge waliwataka mawaziri kufuatilia kero za wananchi badala ya kutumwa na mafisadi kuwasafisha.

hao jamaa ni top five kwa wizi na wote ni wa asia....
ni ukweli wa asia wengi TZ ni mafisadi, kila kitu wao ni short cut tuu
wao ndio kiini cha rushwa africa......

watu msitake kutafuta political correctness mkabadilisha ukweli na ukweli ni indians are thieves and not patriotic
 

Mengi hawezi kupewa zawadi kwa vile hana moral authority ya kutaja wafanyabiashara wa kiasia kuwa ni mafisadi papa wakati yeye ni fisadi mzawa aliyejivisha ngozi ya malaika. 'Conflict of interest'.


Na kama ni kupewa zawadi, wangepewa kina Slaa, walitaja mafisadi miaka kadhaa iliyopita. Tena kupitia mkutano wa hadhara sio press conference.
 
Sasa mbona haisemwi nini kimepotoshwa?wengine hatukuona hiyo habari tungependa kujua nini kilionyeshwa ....
 

Umenena mdau, sitashangaa kama MC wa chama tawala pamoja na mafisadi wenyewe ndo wamemtuma.
Tukumbuke kuwa RA aliwahi kuwa mweka hazina wa chama tawala, CV ya RA kali sana
 
Kanisa lamtetea Reginald Mengi
Saturday, 02 May 2009 09:38
Na Said Mwishehe
Majira

KIONGOZI wa Kanisa Kipentekoste la Gospal Rivival Centre( GRC) Mchungaji Anton Lusekelo amemtetea Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Bw. Reginald Mengi kwa kauli yake ya kutaja majina ya watu alidai ni mafisadi papa na kutaka Serikali impe ushirikiano katika mapambano hayo.

Mchungaji amewashangaa watu wanaodai Bw.Mengi anajipendekeza kwa Rais Jakaya Kikwete na kubainisha kwamba 'ni bora kujipendekeza kwa Rais kuliko kwa mafisadi papa.'

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, jana Mchungaji Lusekelo alisema, tuhuma alizozitoa Bw. Mengi kwa kutaja majina ya mafisadi papa ni nzito hivyo Serikali haipaswi kupuuza bali kushirikiana naye kuhakikisha watuhumiwa wanachunguzwa na hatimaye kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

Alisema haoni sababu baadhi ya watu kuaza kupuuza kauli ya Bw. Mengi kwa sababu ni mtoa taarifa mwema ambaye ameamua kuanika uhalifu hadharani hivyo ni jukumu la Serikali kumlinda mtoa taarifa kwa mujibu wa taratibu za utawala bora .

"Kwa sasa Serikali inachotakiwa kufanya ni kuona jinsi gani inashughulikia majina ya mafisadi papa ambao wametajwa na Bw.Mengi. Naamini Serikali imekuwa mstari wa mbele kushughulikia mafisadi,"alisisitiza Mchungaji Lusekelo.

Alidai anashangazwa kuona wakati Bw.Mengi anatekeleza kazi ya kupambana na mafisadi inayosimamiwa na Serikali, baadhi ya mawaziri akiwemo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Bi.Sofia Simba na Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Bw. George Mkuchika wanamshambulia badala ya kumpongeza.

"Tulitegemea Serikali kuyafanyia kazi maneno ya Mengi dhidi ya mafisadi papa ambao wanaweza kumdhuru wakati wowote baada ya kuanikwa hadharani,"alisema.

Aliongeza kuwa Bw. Mengi alishasema ana vielelezo vyote vya ushahidi wa tuhuma alizotoa dhidi ya watu hao, hivyo ni jukumu la Serikali kuwasiliana naye ili kuchukua hatua zaidi kisheria.

Alitoa mfano kuwa Jeshi la Polisi kwa sasa linahimiza programu ya Polisi Jamii na Bw. Mengi ni miongoni mwa Watanzania walioamua kutumia fursa hiyo kama raia kutaja watu anawatuhumu kwa ufisadi.

Alitoa rai kwa viongozi wa dini, washirikiane na wanasiasa wachache ambao wamejitokeza hadharani kupiga vita ufisadi.

Pia ametoa mwito kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuchukua hatua ya kumfukuza uanachama Bw. Rostam Azizi ambaye ni Mbunge wa Igunga (CCM) ili kulinda heshima ya chama hicho.

Alisema tuhuma zinazomkabili Mbunge huyo ni nzito na zinaligawa Taifa , jamii na Bunge.

Aliongeza ripoti ya REDET ya hivi karibuni inaonesha wananchi bado wanaimani na CCM na vyama vya upinzani havina uwezo wa kushika hatamu, wanachama wanaoandamwa na kashfa mbalimbali kama Bw. Rostam wanaweza kukiathiri chama hicho kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao.

"Mwalimu Nyerere aliwafukuza akina Juma Duni , Sharif Hamad, Shabani Mloo na wenzake ili kuimarisha chama. Alitoa mfano Malikia aliyetuhumiwa kwa ukahaba na kuachwa na Mfalme,"alisema Mchungaji Lusekelo kwa lengo la kuitaka CCM kuchukua hatua dhidi ya wanachama wote wanaohusishwa na tuhuma mbalimbali.

Mchungaji huyo alimpongezi Rais Kikwete kwa juhudi zake za kusimama kidete kupinga ufisadi na kuhimiza uwajibikaji.

Aliwapongeza baadhi ya wanasiasa wakiwemo wabunge waliojitokeza na kuamua kupambana na ufisadi.
 

Sidhani kama kwa kumtetea Mengi ndio anajitengezea mkakati wa kubaki... unless there is something missing!!!

His response was spot-on!!!
 
watu wanaodai Bw.Mengi anajipendekeza kwa Rais Jakaya Kikwete na kubainisha kwamba 'ni bora kujipendekeza kwa Rais kuliko kwa mafisadi papa.'

kwa maana hiyo lipumba, sofia s, mkuchika wanajipendekeza kwa ma papa.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…