macho_mdiliko
Platinum Member
- Mar 10, 2008
- 25,191
- 48,765
????Kabla ya kujibu swali kuhusu kitendo cha Mengi, ambaye anamiliki televisheni ya ITV na kituo cha redio cha Radio One Stereo, kutaja majina ya watu hao aliowaita mafisadi papa, Simba alihoji: " Hapa kuna mtu wa ITV?.
Akiongea na Mwananchi baada ya kupata taarifa za kauli ya Simba, Mengi alisema: "Namuombea kwa Mwenyezi Mungu na kwa maskini wa Tanzania ili wamsamehe kwa sababu hajui anenalo."
Naye Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali itamchukulia hatua za kisheria Mengi iwapo itabainika alikiuka taratibu na kanuni za nchi kwa kutangaza majina ya watu anaowatuhumu kwa ufisadi.
"Tumekusudia kupata ule mkanda wa video, pia tusome maelezo yake ya kimaandishi... tukigundua kuna mahala ambapo sheria haikuzingatiwa, (Mengi) atachukuliwa hatua," alisema Mkuchika.
Mengi ana haki ya kusema atakacho kama raia mwengine. Kama kuna mtu ambae ameona kuwa amechafuliwa jina lake kutokana na kauli yake, ampeleke mahakamani. Serikali ikijiingiza kwenye hili itakuwa imechemsha. Kwa kufanya hivyo wataonekana kama vile wanatumiwa na waliotajwa. Wangejimazia tu.
Amandla.....
Ah.... mpaka inachefua. Hivi rais alitoa wapi viwaziri pambafu kama hivi???
Walivyo na miguu myepesi kuchunguza mambo yanayotetea uhafidhina! wangekuwa wepesi kuchunguza upotevu wa pesa si tungekuwa tumefika mbali kimaendeleo! Kwanza Sophia asituchefua maana ofisi yake ndio kichaka cha mafisadi.
Ndivyo tulivyo...
Hivi nchi yetu ina taratibu na kanuni zipi katika kutangaza majina ya mafisadi? Zilitungwa lini na nani? Can somebody pse educate me on this!
Naye Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, George Mkuchika aliwaambia waandishi wa habari kuwa serikali itamchukulia hatua za kisheria Mengi iwapo itabainika alikiuka taratibu na kanuni za nchi kwa kutangaza majina ya watu anaowatuhumu kwa ufisadi.
Ninapongeza kauli za serikali kwani watanzania wote tuna haki sawa na hakuna wa kumuhukumu mwengine pasi na mamlaka halali yaani mahakama.
Kama Mengi ana ushahidi wa madai yake na ana vielelezo kwanini hakuviwasilisha katika mamlaka husika ili anaowatuhumu wachukuliwe hatua zipasazo?
Hivi leo hii kila mtu anayemtuhumu mwenzie atinge maelezo amchafue kwa nia ya aliyechafuliwa aende mahakamani? Hakuna mantiki hata kidogo, watu wote wafuate sheria na utaratibu uliopo na si kutumia nafasi maalum kupindisha mambo.
Endapo serikali ingekaa kimya maana yake ina kubaliana na uendeshaji wa nchi bila ya kuzingatia utawala bora.
Serikali haipo kwa ajili ya wanyonge tu bali hata akina Mengi na Rostam. Ni vema basi ni lazima ikemee yale yote mabaya ikiwa ni pamoja na kauli za uchochezi, kuchukua sheria mikononi, ufisadi nk.
Serikali yetu iko imara wakati wote na iendelee kufanya kazi kwa faida ya wananchi wote bila ya kuwaonea aibu watu wachache kama Mengi wanaotaka kutimiza matakwa yao binafsi kwa mgongo wa mafisadi nk.
Tuziachie mamlaka husika zifanye kazi ya kutoa hukumu na si vinginevyo.
Mengi kawa out hawa watu kama mafisadi, kama mtu anataka kumtaka Mengi ushahidi ili ku substantiate maneno yake nitaelewa.
Lakini habari ya kusema Mengi kachemka bila hata ya kujua Mengi ana ammunition gani, kesho keshokutwa unaweza kuaibika ukashindwa hata kumuomba radhi.
Mengi si mahakama na hana wajibu wala mamlaka ya kupitisha hukumu, yeye anatoa maoni yake kama mtanzania huru, kama mtu anajiona kapakaziwa na Mengi mahakama ziko, anaweza kufungua mashtaka.
Yaani hao walioitwa mafisadi wenyewe hawajasema viwaziri visharukia issue? Whats wrong with this picture, some puppeteering going on here?
Bottom line ni kwamba S Simba and G Mkuchika wametoa maoni yao kama mawaziri wa ziwara zao na sio tamko la serikali..... Serikali ya Tanzania itoe tamko hafifu kama hilo?? Whom am I kidding, it is an alinacha style of Govt anyway!!!
This is the saddest thang that has happened to Tz in its more than 45 years history...... we need some help and faaaast!!!