kwa nini serikali inawajibia mafisadi???kwani wao wenyewe hawawezi kujibu??au hawazioni mahakama?
Ndugu yangu inaonekana kuwa umekata tamaa na huenda hali hiyo imesababishwa na kukosa mikakati thabiti ya kujadili hoja mbalimbali ili zilete manufaa. SIZE]
Wajibu wa kupamba au kuleta mabadiliko si wajibu wa mtu mmoja katika jamii, hata huyu Dkt Slaa itafika wakati kama binadamu atachoka tu. Kitu cha msingi ilikufikia mabadiliko kwanza nikujiuliza wewe mwenyewe kama uko tayarii kubadilika. !
Pili, jiulize are you doing the right things, either nyumbani kwako, kazini, shule nk. Endapo utakosa kujiuliza mambo kama hayo hutaweza kuwa na mikakati ya kweli ya msingi kabisa ya kuweza kuleta mabadiliko...matokeo yake utakuwa vulnerable na influences...2010 utaweza kushawishika kupiga kura kwa upande wa khanga na pilau.
Maana yangu ni kwamba tusipofanya mambo kwa kuzingatia utaratibu basi hatutaweza ku-influence changes at all, tusahau, tutakuwa wapiga kelele tu!
Hii ni kwa Pundamilia,
Wizi ni kosa la jinai (criminal). Mwenye uwezo wa kumfikisha mwizi mahakamani na kumsomea mashtaka ni Jamhuri. Raia ukishuhudia wizi, kama anaibiwa mwenzako, au jamii au mwenyewe, huna uwezo wa kwenda kumshitaki mwizi mahakamani.
Kazi yako ni kutoa ushirikiano kwa Jamhuri (kupitia jeshi la polisi), kwa kuiambia au kutoa taarifa na kuwa tayari kutoa ushahidi mahakamni utakapoitwa kama shahidi.
Mengi ameiambia serikali, si kwa kwenda polisi. Kwa kuwa ananguvu ya vyombo vya habari ametumia nguvu hiyo kuiarifu Jamhuri kuwa kuna mwizi ameonekana ameiba na ushahidi anao.
Sasa sioni tatizo hapo ndugu pundamilia. Kuiambia polisi au kuiambia jamhuri mpaka uende mwenyewe kituo cha polisi na makaratasi? Hivi mtu huwezi kupiga simu polisi ukasema Mimi fulani niko mahali fulani nashuhudia au nimeshuhudia tukio la wizi??
Sijaona kosa la raia kusema kuwa mali ya umma imefujwa na yeye anao ushahidi!! Vyombo husika vichukue hatua na baada ya kufanya uchunguzi vije mbele na viseme ushahidi hautoshi kuwafikisha mahakamani. Halafu walituhumiwa ni juu yao kufungua kesi ya madai.
Pundamilia unaposema Mengi ilitakiwa afuate taratibu; naomba uwe wazi ni taratibu zipi hizo?
Mengi kawa out hawa watu kama mafisadi, kama mtu anataka kumtaka Mengi ushahidi ili ku substantiate maneno yake nitaelewa.
Lakini habari ya kusema Mengi kachemka bila hata ya kujua Mengi ana ammunition gani, kesho keshokutwa unaweza kuaibika ukashindwa hata kumuomba radhi.
Mengi si mahakama na hana wajibu wala mamlaka ya kupitisha hukumu, yeye anatoa maoni yake kama mtanzania huru, kama mtu anajiona kapakaziwa na Mengi mahakama ziko, anaweza kufungua mashtaka.
Yaani hao walioitwa mafisadi wenyewe hawajasema viwaziri visharukia issue? Whats wrong with this picture, some puppeteering going on here?
this is the million dollar question... This is the question!
Kuna haja ya makala za uchambuzi juu ya hili swali.
FP,
Sina hakika kama umejaribu kuelewa nilichomaanisha kwenye post yangu. Na pia sikuona sababu kwa nini usiniulieze (kama hukunielewa) badala ya kuamua kutoa conclusion yenye kuonesha dharau kwa maoni yangu ambayo hayakuhusu wewe na si lazima uyakubali.
Kwa kuwa tumekuwa tukisema kuwa tunahitaji siku moja hili suala lifike mahakamani, na Mengi mwenyewe alisema hivyo kwamba kama wanaona wameonewa waende mahakamani, huoni kuwa kwa maelezo hayo ya Waziri Simba jamaa wakienda mahakamni tutaipata ile fursa tuliyokuwa tunaitafuta siku nyingi? Kama huoni hiyo basi eleza jinsi unavyoona wewe na siyo kujaribu kushusha hadhi ya wenzio kwa kuwapandia mgongoni!
Kipimapembe,
Kama ambavyo nilimsahihisha aliyejibu swali langu hapo awali, majibu yako yame-miss 'keyword' ambalo ni neno 'malalamiko'. Sasa katika majibu yako hili neno hukuligusa na ndiyo linajenga msingi wa jibu lako. Hebu incude hilo neno 'malalamiko; halafu uone kama maelezo yako uliyoyatoa hapo kama yatakuwa the same again.
Jaribu.
Nimelirudia lile swali hapo ili kukurahisishia usirudi nyuma sana.
Tom,
Hebu tafakari kwa mfano huu hapa chini:
Umeibiwa nguo zako na baada ya siku mbili tatu unamwona jirani yako amevaa shati kama lile la kwako lililoibiwa, je unachotakiwa kufanya nini, kuita press conference na kumuita mwizi au unafikisha malalamiko yako katika vyombo vya sheria?
Skills4ever!
Umenigusa it seems you are a great thinker!!!! Inanibidi niache kazi ninayoifanya ambayo its equally important nichangie na wajamii forums!
Tulishasema hawa mawaziri wengi wao ni kaput they are chosen for personal needs period!! na satili ni ile ile ya Salva kwa kupitia kwa makuwadi some ministers were given mere favours! Others for simply having had intimate relationships with the presida and associates period.
Sofia Simba na Mkuchika wanachunguza nini? Wote wako kwenye payroll za mafisadi na nina ushahidi!!! Mkuchika George alipokuwa DC wa Ilala alikuwa anamtembelea Manji pale kwenye maduka ya Honda kuchukua dola pamoja na Yusuf Makamba!!! hata IGP Said Mwema then RCO wa Dar!!!If they want nitawapa picha next time around!! MSIJE TU MKAFUNGIWA watch out!!!
Mafisadi walitajwa wapo na wana msururu wa mawakili uchwara let them go to court!!! Kwa nini serikali iwasemee!! Au ndio wamewaweka mfukoni!!!
As I said Mengi might be miopioc kwa muono wake ili ufanyike ufisadi there must be players na nilisema wako waswahili kibao from the police force,Jeshi Ikulu,Usalama wa taifa, TRA, and all kinds sitawataja wote kwani ni wengi who helped the ufisadi na wanajulikana wana mimali like hell tuwahoji! Huwezi ukawatenga na PAPA au whatever you call it!!
But the bottom line is hatuna utawala its all bull shit!!
Haya tuone kama akina MASILINGI /Manji they came and went :Masha walishindwa kumchukulia Mengi hatua with a lot of pomposity and law jargons/barons akina SOFIA na Bra zao wataishia na kuuza sura tu ?
Tom,
Hebu tafakari kwa mfano huu hapa chini:
Umeibiwa nguo zako na baada ya siku mbili tatu unamwona jirani yako amevaa shati kama lile la kwako lililoibiwa, je unachotakiwa kufanya nini, kuita press conference na kumuita mwizi au unafikisha malalamiko yako katika vyombo vya sheria?
ninapongeza kauli za serikali kwani watanzania wote tuna haki sawa na hakuna wa kumuhukumu mwengine pasi na mamlaka halali yaani mahakama. Kama mengi ana ushahidi wa madai yake na ana vielelezo kwanini hakuviwasilisha katika mamlaka husika ili anaowatuhumu wachukuliwe hatua zipasazo? Hivi leo hii kila mtu anayemtuhumu mwenzie atinge maelezo amchafue kwa nia ya aliyechafuliwa aende mahakamani? Hakuna mantiki hata kidogo, watu wote wafuate sheria na utaratibu uliopo na si kutumia nafasi maalum kupindisha mambo.
Endapo serikali ingekaa kimya maana yake ina kubaliana na uendeshaji wa nchi bila ya kuzingatia utawala bora.
Serikali haipo kwa ajili ya wanyonge tu bali hata akina mengi na rostam. Ni vema basi ni lazima ikemee yale yote mabaya ikiwa ni pamoja na kauli za uchochezi, kuchukua sheria mikononi, ufisadi nk.
Serikali yetu iko imara wakati wote na iendelee kufanya kazi kwa faida ya wananchi wote bila ya kuwaonea aibu watu wachache kama mengi wanaotaka kutimiza matakwa yao binafsi kwa mgongo wa mafisadi nk.
Tuziachie mamlaka husika zifanye kazi ya kutoa hukumu na si vinginevyo.
Pundamilia nami kwa upande wangu sioni kwamba Mengi kafanya kosa kubwa sana given the circumstances.
Hivi kweli unafikiri ukizingatia hawa jamaa akina rostam walivyo 'heavy weights' hili swala lingefika popote kama angeenda na makaratasi yake TAKUKURU au pale kituo cha polisi Oysterbay?
Naomba nitumie mfano huo huo uliotumia wewe:
Umeibiwa nguo zako na baada ya siku mbili tatu unamwona jirani yako amevaa shati kama lile la kwako liliobiwa, UKIMCHEKI JAMAA NI BOUNCER WA NGUVU NA MARA KADHAA POLISI WENYEWE WANAONEKANA KUMWOGOPA KWANI SI MARA YA KWANZA KUSIKIA AMEIBA WASIFANYE KITU, je utakachofanya ni kujitoa mhanga kuiambia jamii msaidiane au unafikisha malalamiko yako katika vyombo vya sheria ambavyo on countless occasions vimeonyesha incompetence ku deal na huyu heavy weight!!!??
Kumbuka kipindi flani DPP na AG walisema kabisa bungeni kuwa mtandao wa hawa mafisadi ni mkubwa na wana hela sana kiasi ambacho serikali ikienda kwa pupa wanaweza yumbisha mambo nchini. IMAGINE THEY SAID SO in PUBLIC yani hio ni njia mbadala ya kusema hatuwawezi!!
NILIKUWA DODOMA WAKATI WA UCHAGUZI WA UWT NA SOPHIA SIMBA ALIKUWA AKIGAWA KATI YA Sh 150,000 na 200,000 KWA WAJUMBE, JE, HUYO ANAWEZA KUPIGA VITA RUSHWAA? UNADHANI ATAWATENGA WALIOMPA FEDHA ZA KUGAWA?
Ndugu,
Mfano wako ni mzuri, lakini hauendani na tukio hili hata kidogo au kwa lugha nyingine mfano wako ni mfu!
Hao mafisadi hawajamwibia Mengi, wameiba raslimali za nchi ambazo watawala wetu wanajukum la kuzilinda kwa kushilikiana na wananchi, Na Mengi kama mtanzania amejitolea kutoa maoni yake ambayo anaushahidi, kwa hiyo Polisi, na waendesha mashitaka wanatakiwa wawahoji na kupeleka mashitaka Mahakamani huko ndiko mbivu na mbichi zitajulikana.
Kipimapembe,
Kama ambavyo nilimsahihisha aliyejibu swali langu hapo awali, majibu yako yame-miss 'keyword' ambalo ni neno 'malalamiko'. Sasa katika majibu yako hili neno hukuligusa na ndiyo linajenga msingi wa jibu lako. Hebu incude hilo neno 'malalamiko; halafu uone kama maelezo yako uliyoyatoa hapo kama yatakuwa the same again.
Jaribu.
Nimelirudia lile swali hapo ili kukurahisishia usirudi nyuma sana.
Tom,
Hebu tafakari kwa mfano huu hapa chini:
Umeibiwa nguo zako na baada ya siku mbili tatu unamwona jirani yako amevaa shati kama lile la kwako lililoibiwa, je unachotakiwa kufanya nini, kuita press conference na kumuita mwizi au unafikisha malalamiko yako katika vyombo vya sheria?
Pundamilia,
Nimesema kwanza swali lako halishabihiani hasa na suala linalojadiliwa. Hata hivyo kwa muktadha wa swali lako jibu lako ni hivi. Malalamiko yako utayafikisha kwenye vyombo vya sheria kwa njia utakayoona inafaa. Suala hapa ni njia utakayotumia kuvifikia vyombo vya sheria. Njia yoyote itakayopeleka taarifa kwa vyombo vya sheria itafaa.
Lakini vilevile njia utakayotumia itategemeana na ukubwa wa kosa au jinai yenyewe. Kwa mtu aliyezungushia ukuta kwenye mtaa mzima na kutangaza kuwa ni eneo lake na huruhusiwi kutoka humo ndani ya ukuta na ukaona majirani zako hawajui kinachoendelea, kupiga kelele ili majirani wote wajue na polisi walio kituo cha jirani wajue inaweza kuwa njia sahihi. au?