Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Mrema wa Chadema anasema kuwa wana CCM wananufaika na hao mafisadi.kwani Chadema nao hawanufaiki na Mengi?

Mengi ndio mfadhili wa helkopta za Chadema unategemea watamsema vibaya?
kwenye ununuzi Ndege ya rais na rada kuna wafanyabiashara wazalendo toka mkoa wa kilimanjaro wanahusika na MENGI anawajua lakini hawajatajwa.
hapa kila upande unatizama maslahi yake.kama vijana wa UVCCM walivyotoa tamko kumsafisha RA na chadema nao wanamsafisha mfadhili wao.

Mrema ana kumbukumbu nzuri sana WENGI TUMEMSAHAHU CHAVDA na Dhahabu zilizokamatwa Airport.

tehee nasikia Chavda alimjengea nyumba Masaki MANGI wa watu, sijui mkweli???

KUWAFICHUA MAFISADI HUKU UKUMSIFIA JK ni ufisadi pia.
 
Mrema wa Chadema anasema kuwa wana CCM wananufaika na hao mafisadi.kwani Chadema nao hawanufaiki na Mengi?

Mengi ndio mfadhili wa helkopta za Chadema unategemea watamsema vibaya?
kwenye ununuzi Ndege ya rais na rada kuna wafanyabiashara wazalendo toka mkoa wa kilimanjaro wanahusika na MENGI anawajua lakini hawajatajwa.
hapa kila upande unatizama maslahi yake.kama vijana wa UVCCM walivyotoa tamko kumsafisha RA na chadema nao wanamsafisha mfadhili wao.

Umeelewa ujumbe wa Mr. mrema wa chadema au ilimradi tu na wewe uchangie?
 
Nataka Kumjua baba wa Mafisadi,Nani anawalea mafisadi?

Mie nimeona sasa Mengi ameenda mbali sana,Katumia Vyombo vyake vya habari vibaya sana na mpaka sasa nashindwa kuelewa ni kwanini Jukwaa la Habari limekaa kimya kuhusiana na habari hii.Tukiachia mambo kama haya siku mtu anweza kuamua kuwatangazia UMMA mambo ya ajbu ajabu tu!

Kama anajua Kila "flani" ni mapapa basi atuambie baba yao ni nani?hauwezi kuwa papa kama haujazaliwa na papa,na hauwezi kuishi kwa ujanja tu bila ya kulelewa na PAPA.Kwa maana nyingine aseme tu kuwa Na "flani" ni papa,awaorodheshe!

Inawezekana Mengi anawaju wazazi wa hawa Mapapa,ila kwa suala hili la kuchonga juzi mie nasema mzee amechemka,na maejenga chuki kati ya watu na pia ameleta "Ukaburu"!

Kama asipotaja baba wa Mapapa,anayawealea mapapa mie nitandelea na msimamo wangu kuwa Mengi ameamua kuwachafua kina RA na wenzake!

Tabia ya mtu kutaka Sympathy kwa wanachi imepitwa na wakati,

Yes,Mengi najua unaweza kuwataja wazazi wa hao mapapa.Come on do it Now!
 
Askofu amshambulia Sophia Simba

2009-04-30 14:37:56
Na Restuta James
Askofu wa Kanisa la Pentecostal Evangelistic lenye Makao Makuu mkoani Mbeya, Zebadiah Mwakatage, amemshambulia Waziri wa Nchi, Ofsi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, kuwa kauli yake ya kutetea mafisadi ni udhalilishaji serikali.

Alisema hali hiyo itafanya Watanzania kuamini kuwa waziri huyo na seikali yake wameajiriwa kuwa mawakili wa mafisadi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Askofu Mwakatage, alisema anashangaza na kukatisha tamaa kwa tamko la serikali kupitia Waziri Simba, kutetea mafisadi na huku akijua umaskini unaokabiliwa Watanzania umetokana na kuchotwa kwa mabilioni ya fedha.

Alisema hata baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaosema Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, anajipendekeza kwa Rais Jakaya Kikwete ni heri kuliko kujipendekeza kwa mafisadi kama alivyofanya Simba.

``Hivi Waziri Simba ameajiriwa uwakili na mafisadi kuyatetea, maana wao wana fedha tena wana midomo yao ambayo wao ndio wangelalamika, kwanini aibuke na kuwatetea eti ni wafanyabishara safi, hapa kuna mashaka,`` inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Alisema kutokana na maandiko matakatifu, Mengi asione ajabu kuchukiwa na mafisadi na baadhi ya viongozi wa serikali bila shaka wana maslahi wanayopata kutoka kwa mafisadi.

Askofu Mwakatage alisema kwa kuzingatia kuwa msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Watanzania wataendelea kuwaombea waadilifu, wanaouchukia ufisadi kama Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroud Slaa, Dk Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Same, Anne Kilango, Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka.

``Nchi yetu tajiri kwa kila kitu, imebatizwa jila la dharau na aibu la umaskini, Mungu tuokoe. Wachonganishe ndimi zao mafisadi na waongo wote wasielewane,`` alisema Askofu Mwakaatage.

Juzi, Simba alijitokeza hadharani na kutetea wanaotuhumiwa kuwa mafisadi mapapa watano waliotajwa na Mengi na kwamba, kitendo cha kuwataja ni sawa na lugha ya kijiweni.

Simba alisema mapapa hao waliotajwa na Mengi ni watu safi na waadilifu kwa sababu, hawajahukumiwa na mahakama.
Alisema Mengi ameingilia kazi za serikali na kumtaka aiache ifanye kazi.

SOURCE: NIPASHE
 
Inawezekana Mengi anawaju wazazi wa hawa Mapapa,ila kwa suala hili la kuchonga juzi mie nasema mzee amechemka,na maejenga chuki kati ya watu na pia ameleta "Ukaburu"!

Kama asipotaja baba wa Mapapa,anayawealea mapapa mie nitandelea na msimamo wangu kuwa Mengi ameamua kuwachafua kina RA na wenzake!

Tabia ya mtu kutaka Sympathy kwa wanachi imepitwa na wakati,

Yes,Mengi najua unaweza kuwataja wazazi wa hao mapapa.Come on do it Now!

Kwa nini wewe unaamini kuwa kuna baba zao? inawezekana hawa ndio mababa labda kama unataka Mengi e-expand list yake.
 
Njaa yao itawaua..hamna kingine zaidi ya njaa..

Kwa njaa yao vijana hawa wa Tabora naomba niwape laana mbili kuu ambazo ziwafikie na kuwaganda mpaka uchaguzi wa 2010
  1. ADUI YAKO MWOOMBEE NJAAA!
Mwaka huu mvua Tabora ni haba na mwakani naomba mvua ziwe haba ili njaa iwaingie mpaka utosini halafu tuone kama huyo RA atawasaidia, kwani atakuwa ametingwa na uchaguzi

2. STATIC GLOBAL FINANCIAL CRISIS

Bei ya pamba imeshuka mpaka Tsh 150/Kg, Na iendeleeeeeee hivyo hivyo mpaka watakapokuwa na masikio na adabu wasukuma hawa, labda 2010 watajua kuwa kumbe maharage si chakula cha jela peke yake

Nawakilisha kwa mola maulana!
icon8.gif
 
The saga continues, jana ITV walitoa dakika kama 5 hivi kwenye taarifa yao ya habari ya saa mbili wakirusha maoni ya watu kama saba hivi. Cha ajabu wote waliorushwa hewani walimpongeza Mengi kwa hatua yake ya kutaja mafisadi papa na kulaani vikali wanaompinga akiwamo Sophia simba.

Sasa sijui watu wote waliohojiwa ilitokea by coincident wakawa in favour of Mengi au wale walioponda walieditiwa na kuondolewa wasisikike!!
 
the saga continues, jana itv walitoa dakika kama 5 hivi kwenye taarifa yao ya habari ya saa mbili wakirusha maoni ya watu kama saba hivi. Cha ajabu wote waliorushwa hewani walimpongeza mengi kwa hatua yake ya kutaja mafisadi papa na kulaani vikali wanaompinga akiwamo sophia simba.

Sasa sijui watu wote waliohojiwa ilitokea by coincident wakawa in favour of mengi au wale walioponda walieditiwa na kuondolewa wasisikike!!
seeking public sympath
 
The saga continues, jana ITV walitoa dakika kama 5 hivi kwenye taarifa yao ya habari ya saa mbili wakirusha maoni ya watu kama saba hivi. Cha ajabu wote waliorushwa hewani walimpongeza Mengi kwa hatua yake ya kutaja mafisadi papa na kulaani vikali wanaompinga akiwamo Sophia simba.

Sasa sijui watu wote waliohojiwa ilitokea by coincident wakawa in favour of Mengi au wale walioponda walieditiwa na kuondolewa wasisikike!!

Chombo chake mkuu. Hata ni wewe hautaupendelea mkono unao kulisha? Sishangai hata kidogo kama hao wote walio onyeshwa IPP are in support of Mengi. Lets see whats next.
 
Pesa ilitumika kumsaliti yesu...haya ni madogo kwa kweli makubwa yaja
 
The saga continues, jana ITV walitoa dakika kama 5 hivi kwenye taarifa yao ya habari ya saa mbili wakirusha maoni ya watu kama saba hivi. Cha ajabu wote waliorushwa hewani walimpongeza Mengi kwa hatua yake ya kutaja mafisadi papa na kulaani vikali wanaompinga akiwamo Sophia simba.

Sasa sijui watu wote waliohojiwa ilitokea by coincident wakawa in favour of Mengi au wale walioponda walieditiwa na kuondolewa wasisikike!!

Mwaka huu tutasikia mengi na si kutoka kwa Mengi tu bali kutoka kwa wengi maana kuna mengi yamejificha ndani ya vifua vya watu na sasa yatatoka tu, vinginevyo itakuja, "Uchiteme uchimumunye", sasa waliokula nyama, "wachiteme wachimumunye" waendelee kutete nyama zao
 
Chadema yawashukia wanaompinga Mengi

Kutokana na hali hiyo, alimtaka Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba aueleze umma kwanza alikopata fedha za kampeni ya uchaguzi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kabla ya kumjadili Mengi kuhusu suala hilo.

He he he!

Huyu mama alikurupuka kuwasafisha mapapa. Tuone sasa akijiokoa.
 
MwanaFalsafa1;439155]Askofu amshambulia Sophia Simba

``Hivi Waziri Simba ameajiriwa uwakili na mafisadi kuyatetea, maana wao wana fedha tena wana midomo yao ambayo wao ndio wangelalamika, kwanini aibuke na kuwatetea eti ni wafanyabishara safi, hapa kuna mashaka,`` inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Hapo ndipo kazi inapoanzia. Laiti Sophia angeweza kutupa ufafanuzi. Ila kwa tabia yake anaweza kuja na maneno yake ya kiswahili na kutwambia kuwa "mtajiju"!

``Nchi yetu tajiri kwa kila kitu, imebatizwa jila la dharau na aibu la umaskini, Mungu tuokoe. Wachonganishe ndimi zao mafisadi na waongo wote wasielewane,`` alisema Askofu Mwakaatage.

Mtumishi wa mungu, hakuna zaidi. AMINA.
 
Mrema wa Chadema anasema kuwa wana CCM wananufaika na hao mafisadi.kwani Chadema nao hawanufaiki na Mengi?

Mengi ndio mfadhili wa helkopta za Chadema unategemea watamsema vibaya?
kwenye ununuzi Ndege ya rais na rada kuna wafanyabiashara wazalendo toka mkoa wa kilimanjaro wanahusika na MENGI anawajua lakini hawajatajwa.
hapa kila upande unatizama maslahi yake.kama vijana wa UVCCM walivyotoa tamko kumsafisha RA na chadema nao wanamsafisha mfadhili wao.

Kuna mtu anaweza akatuwekea hapa concise definition ya neno 'fisadi'?

Nahisi wengi tunapoteza muelekeo.
 
kwa hiyo CHADEMA wanaungamkono uvujwaji sheria? hata kama ndo iwe kweli wanaotuhumiwa si wapya.
 
Unajua kwenye crisis kubwa kubwa kama hii tuliyo nayo ya ufisadi, tunapata nafasi ya kujua na ni kiongozi wa aina gani.Nafikiri SS amejidhihirisha waziwazi yeye ni nani. Wananchi kazi kwetu kumpa upande tunaoonna unamfaa kadri ya mang'amuzi yetu tofauti tofauti.
Kazi ipo sio mzaha
 
Back
Top Bottom