Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Kamanda ndo vijana wenu hao mnawaandaa kuchukua uongozi wa juu wa chama na serikali...wamekaa kama mafisi kuvizia mizoga bila hata kufikiri.....wanatumika kwa njaa zao wala maslahi ya taifa hayapo! Rostam ni balaaa

Masa,

Inawezekana Bashe huwa anaenda kwa Mwalimu Juma kule Urambo na kupata kizizi cha kumsaidia kidogo. Sasa akisifiwa na wale Mambumbu Manyamwezi, anakuwa kama senene aliyejificha kichwa na kuacha Kipengule chote juu. Mhaya akipita anamuona na kumchomoa.

FMes, kama ndiyo CCM mnaanda watu, basi andaeni wa maana maana huko Tabora naona hamna watu. Hawa wakipata nafasi kidogo tu, hata nyie watawauza. Tena Wanyamwezi ni kuwatafutia vibinti vyeupevyeupe na Kitaarabu kidogo, watakuwa kama Samson, tena hawa kama lilivyo joka, watatema wenyewe siri bila ya kuulizwa mara mbili. Kama Masha vilee pale Rose garden akipata kinywaji (nasikia).

Masa hebu leta tena ile picha ya Mwalimu Juma na utibabu wake.
 
Mrema wa Chadema anasema kuwa wana CCM wananufaika na hao mafisadi.kwani Chadema nao hawanufaiki na Mengi?

Mengi ndio mfadhili wa helkopta za Chadema unategemea watamsema vibaya?
kwenye ununuzi Ndege ya rais na rada kuna wafanyabiashara wazalendo toka mkoa wa kilimanjaro wanahusika na MENGI anawajua lakini hawajatajwa.
hapa kila upande unatizama maslahi yake.kama vijana wa UVCCM walivyotoa tamko kumsafisha RA na chadema nao wanamsafisha mfadhili wao.

Mkuu Bila ku type MKOA WA KILIMANJARO vidole vyako haviridhiki kabisa. Acha Chuki mkuu kama unawafahamu waweke hapa, kama huwajui tulia sio lazima Uchangie. Just sit down na Uenjoy Mjadala na Uwaachie wenye dataz wazimwage.
 
Mpaka sasa sijapata ushahidi wa kutosha kuwa Mkapa na JK ni Mafisadi,Hivyo napingana na Mawazo yako Mpaka nitakopothibitishiwa hivyo mahakamani

loooooooooooooooooooooh du dududud oooh ooh hiyo oohh ooooh haaaaa!!!1
 
watu wanamshambulia mengi kwa nini? listi kila mtu anaijua, iwe ana visa nao au vinginevyo ukweli ubaki palepale.
 
watu wanamshambulia mengi kwa nini? listi kila mtu anaijua, iwe ana visa nao au vinginevyo ukweli ubaki palepale.

Ndumbayeye, hiyo list ame-compile nani? Imehakikiwa kisheria? Kuna ushahidi? Mi nakumbuka ile kesi ya Liyumba list, ilileta mtafaruku katika familia nyingi and it was malicious.... nadhani kama Great Thinkers, we can agree to disagree na pia siyo kila mtu anayehoji kitu ni fisadi au mtetezi wa mafisadi, we need critical thinking. Tusimshikie bango Mengi eti kawataja mafisadi, hilo nakataa, nataka kuona sheria unafuata mkondo wake na siyo witch hunt! Mengi si hakimu, si polisi....na ameongea bila uthibitisho. Kaona Dr Slaa anaongea naye kaamua kujitosa....
 
Mengi:Tutajie BABA wa MAPAPA?kama hayupo tuambie nani anawalea?
Gembe Today, 04:14 PM

--------------------------------------------------------------------------------

Nataka Kumjua baba wa Mafisadi,Nani anawalea mafisadi?

Mie nimeona sasa Mengi ameenda mbali sana,Katumia Vyombo vyake vya habari vibaya sana na mpaka sasa nashindwa kuelewa ni kwanini Jukwaa la Habari limekaa kimya kuhusiana na habari hii.Tukiachia mambo kama haya siku mtu anweza kuamua kuwatangazia UMMA mambo ya ajbu ajabu tu!

Kama anajua Kila "flani" ni mapapa basi atuambie baba yao ni nani?hauwezi kuwa papa kama haujazaliwa na papa,na hauwezi kuishi kwa ujanja tu bila ya kulelewa na PAPA.Kwa maana nyingine aseme tu kuwa Na "flani" ni papa,awaorodheshe!

Inawezekana Mengi anawaju wazazi wa hawa Mapapa,ila kwa suala hili la kuchonga juzi mie nasema mzee amechemka,na maejenga chuki kati ya watu na pia ameleta "Ukaburu"!

Kama asipotaja baba wa Mapapa,anayawealea mapapa mie nitandelea na msimamo wangu kuwa Mengi ameamua kuwachafua kina RA na wenzake!

Tabia ya mtu kutaka Sympathy kwa wanachi imepitwa na wakati,

Yes,Mengi najua unaweza kuwataja wazazi wa hao mapapa.Come on do it Now!

MUULIZE BABAKO
__________________
 
Kaika sherehe ya kuhitimisha shangwe za wakomboaji nchi....ambazo ziliandaliwa na mama anna malecela..wabunge wengi wamelaani vitendo vya viongozi wa nchi tena mawaziri kutetea mafisadi wanaokula nchi....jamani katika maisha yangu na uzee huu sijapata kuona waziri anatetea ufisadi hata siku moja....yaani wananchi wanateseka kule vijijini hutosikia hata siku moja viongozi wanaingilia kati kujua matatizo yao lakini inasikitisha kitendo cha kuwataja mafisadi papa watu wenye heshima zao wanadiriki kuwatetea mbela ya waandishi wa habari....inasikitisha lakini inaumiza sana napenda kuwaambia hata kama leo hii watamuumiza anna nawahakikishieni....huko nje kuna ANNA kibao...,nae mbunge wa vunjo mh maro alisema kwa kweli ndugu wananchi tunaitaji maombi yenu sana hapa mnapotuona kuna watu wanafikiria mengi mabaya juu yetu,,viongozi wa dini hakuna la kumshinda mungu...endeleeni kutuombea mungu atatulinda........kwa kweli inatia aibu sana sasa sijui wah kama wale unaweza kusimama nao mbeele ya wananchi wakakuelewa....anya way...hii ndio tanzania
 
Wakuu,

Sioni kwa nini Mengi anasakamwa. Yeye ametaja tena waziwazi kwenye mkutano wa waandishi wa habari wote. Hakuvieleza vyombo vyake vya habari tu ndio maana hata magazeti yasiyo milikiwa na Mengi yaliandika. Sasa anayeona hakutendewa haki aende mahakamani adai fidia. Kuna sababu gani ya kuja hapa kuwatetea watu ambao wameliangamiza taifa kiuchumi kwa kuweka rushwa mbele na kutetewa na walio kwenye madaraka. Mengi hajafanya kosa mpaka hapo wanaodai kuzushiwa watakapoweza kutuonyesha kwamba Mengi hakusema kweli.

Mbona Dr. Slaa alifanya hivyo hivyo na waliotajwa wako kimya mpaka leo? Ni lipi la ajabu alilolifanya Mengi? Labda wengine watasema mbona amewataja Watanzania wenye asili ya wahindi tu!!! Nafikiri hapa tusiangalie rangi bali tuangalie ukweli.

Hawa jamaa ni mafisadi na iko siku watakuja imba haleluya!!!! Mnaowatetea endelea kuwatetea lakini ukweli unabaki pale pale kwamba hawa ni mafisadi. Period.
 
Mwanahabari una chuki na watu wengine siyo!Tutajie ni wkanini uwaone hawa wazee Mafisadi?acha mambo ya kizushi..Mie nimemuomba Mengi atutajie tu sababu yeye si ndiyo mtu wa kuhukumu watu na kuwapa makosa..

Mpaka sasa sijapata ushahidi wa kutosha kuwa Mkapa na JK ni Mafisadi,Hivyo napingana na Mawazo yako Mpaka nitakopothibitishiwa hivyo mahakamani!

Wanaweza kuwa na mapungufu yao katika utendaji ila bado sijafikia hatua ya kuwapaka Matope kiivyo ila wana matatizo yao na sikatai!

lakini si umeuliza nani anawalea, jibu ni hilo...hawa wawili ndio wanalea mafisadi, mafisadi wamewasaidia kuwaweka walipo ndo maana hamna mtu anayechukuliwa hatua. Rostam hataguswa pamoja na kwamba anahusika na uchafu wote mnaouona sasa. Ben alipewa hela na guarantees nyingi akihakikisha JK anapita, JK campaign yake yote ilipewa hela za wizi za Rostam na wenzake..bado mnadhani hayo ni matope?

Mahakamani sahau maana wameweka wenzao kila sehemu (Mramba na mgonja walishtakiwa ati hawakutumia madaraka vizuri na kuiliingiza taifa hasara, mbona Lowassa hakukamatwa?), kilichobaki ni waandishi wetu wanasaidia kuanika uozo wao, ndo maana kila siku wananchi wazalendo serikalini wana-leak information left and right, wamechoka!
 
Wadau hivi huyu Sofia Simba nyuma yake kuna akina nani? Binafsi siamini ni mafisadi pekee wako nyuma yake inaonekana huwa anatumwa specifically kutoa matamko yenye utata ili kutokana na haiba yake ya mtu wa hovyo hovyo basi watu makini wa-assume ni kauli yake tu sio ya serikali. Nakumbuka alivyo-comment baada ya Kitine kuongelea mambo muhimu ya nchi, leo tena anajiunga kuwatetea wafanyabiashara badala ya kuongelea matatizo mbali mbali yanayowakabili wananchi. Kauli zake hizi za ajabu ajabu nafikiri angeongea waziri makini kama Mama Sitta au Shamsa Mwangunga kila mtu angeshtuka, lakini kwa vile kaongea kilaza ndio maana watu wanapuuza! Hivi CV yake ikoje, embu wadau iwekeni hapa tumjadili!
 
Mazee hapa hii habari mtirirko wake haueleweki kwa saana....
 
Dk. Slaa awindwa bungeni
• Waziri Kombani, Ghasia waongoza mkakati

na Mwandishi Wetu



MWENENDO wa mambo katika mkutano wa 15 wa Bunge, unaoendelea mjini hapa, unazidi kuwa na utata mara baada ya kuwapo taarifa kuwa serikali imeanza mkakati maalumu wa kummaliza kisiasa na kumfungulia kesi ya jinai, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa.
Habari za uhakika zilizolifikia Tanzania Daima Jumatano kutoka kwa baadhi ya wabunge, zimedai kuwa, kwa siku kadhaa sasa, mawaziri wawili wamekuwa wakipanga mkakati huo wakishirikiana na wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baadhi wa kutoka kambi ya upinzani.
Mawaziri wanaotajwa kuendesha mkakati huo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi, Hawa Ghasia na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI), Celina Kombani.
Habari hizo zinadai kuwa, mawaziri hao wamekuwa wakipita kwa wabunge wakiwaeleza kuwa serikali imetambua kuwa ni jambo la hatari kuendelea kuwa na mtu wa aina ya Dk. Slaa bungeni, akiwa na wadhifa wa unyekiti katika Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa.
Mbunge mmoja aliyefuatwa na mmoja wa mawaziri hao na kushawishiwa kushiriki katika mpango wa kumshughulikia Dk. Slaa na kufanikiwa kuzungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa sharti la jina lake kutotajwa gazetini, alieleza kuwa, Waziri Kombani anasimamia mpango wa kumuondoa Dk. Slaa katika wadhifa wake wa Uenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa, huku Waziri Ghasia akiwa ameweka watu maalumu wanaochunguza maofisa wa serikali anaozungumza nao, wanaodhaniwa kuwa ndio wanaompatia nyaraka za siri za serikali zinazohusu ufisadi.
“Mimi nilifuatwa na Waziri Kombani mwenyewe, kwa mdomo wake akaanza kunishawishi niisaidie serikali kumshaghulikia Dk. Slaa, kwa sababu ni mtu hatari anayeinyima usingizi. Aliniambia kuwa ni vigumu kujua watu wanaompatia nyaraka za siri za serikali, hasa zile zinazohusu ufisadi, kwa sababu Waziri Ghasia ameweka watu maalumu wanaofuatilia maofisa wa serikali alio karibu nao, lakini mpaka sasa hakuna mafanikio.
“Waziri Kombani aliniambia kuwa, Waziri Ghasia alifikia uamuzi huo ili kujua maofisa wa serikali anaowasiliana nao kwa sababu hao ndio wanaompatia nyaraka za siri za serikali, na kwamba kama akikamatwa nazo safari hii, hatapona,” alisema mbunge huyo.
Mmoja wa viongozi wa kambi ya upinzani aliyezungumza na gazeti hili na kutaka jina lake lihifadhiwe kwa sababu ameteuliwa kuongoza timu ya kuchunguza madai hayo dhidi ya Dk. Slaa, alisema kambi ya upinzani inazo taarifa hizo na inazifanyia kazi kwa siri, kwa sababu baadhi ya wabunge wa kambi hiyo wamenunuliwa ili kumuangamiza.
Alisema uchunguzi wa timu yake umebaini kuwa, Dk. Slaa alianza kuingia katika mgogoro na wabunge baada ya kuzuia posho ambazo wajumbe wa kamati walikuwa wakilipwa na halmashauri mara wanapokwenda kuzikagua.
“Hali ni mbaya, lakini tunafanya kazi na tutalipua bomu ili wananchi wajue kuwa vita hii inapiganwa pia na mawaziri na si wabunge peke yao.
“Uchunguzi wa timu yangu umebaini kuwa, Dk. Slaa alianza kuchukiwa na wabunge wenzake alionao katika kamati moja ambayo yeye ni mwenyekiti wake, baada ya kuzuia malipo ya posho kutoka halmashauri walizokuwa wakifika kuzikagua kwa sababu ni kinyume cha taratibu.
“Lakini Dk. Slaa, alikuwa na sababu ya msingi ya kuzuia posho hizo, kwa sababu Bunge linawalipa wabunge kila wanapokuwa katika shughuli halali za Bunge. Kulipwa na halmashauri ni kinyume cha taratibu, kwa sababu wanakuwa wamelipwa posho mara mbili kwa kikao kimoja. Sasa alipozuia kwa sababu walikuwa wamezoea, chuki ikaanza,” alisema kiongozi huyo wa upinzani ambaye pia ni mbunge.
Akizungumzia wabunge na mawaziri wanaoongoza mkakati huo wa kummaliza Dk. Slaa, alisema taarifa za uhakika alizonazo ni pamoja na Waziri Kombani na Mbunge wa Kibakwe (CCM), George Simbachawene, ambao wamekuwa wakipita kwa wabunge wakiwataka kuungana kwa pamoja kupinga hatua za upotoshaji zinazofanywa na Dk. Slaa kwa lengo la kulichafua Bunge.
Alisema Waziri Kombani tayari amekwishakutana na Mbunge wa Viti Maalumu, Grace Kihwelu (CHADEMA) na kumshawishi akubali kuchukua wadhifa wa Dk. Slaa wa uenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa mara tu atakapoondolewa, na kwamba alimuahidi kuwa serikali itakuwa pamoja naye katika shughuli zake zote zinazohusu ubunge.
Kuhusu Waziri Ghasia, alisema baadhi wa wabunge wameishasikika wakieleza kuwa wamepewa kazi maalumu na waziri huyo ya kuchunguza na kumpatia taarifa iwapo Dk. Slaa ana nyaraka mpya za serikali na mahali alikozihifadhi ili akamatwe na kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria za nchi.
Alipoulizwa kuhusu madai hayo, Waziri Kombani alilieleza gazeti hili kuwa, hana ugomvi na Dk. Slaa, hivyo hana sababu yoyote ya kushiriki katika mpango wa kumuangamiza kisiasa au kumfikisha katika vyombo vya dola.
Aliongeza kuwa, alichokisema Dk. Slaa hakihusiani na wizara yake na kwamba tangu alipoingia katika utumishi wa umma, hajawahi kuhusika katika tuhuma au kashfa yoyote na jambo hilo hataruhusu litokee.
Tanzania Daima Jumatano lilipowasiliana na Kihwelu na kumuuliza kuhusu madai hayo, alisema hana taarifa hizo, lakini lilipomueleza kuna ushahidi kuwa alikutana na Waziri Kombani na akashawishiwa kukubali kuchukua nafasi ya Dk. Slaa katika kamati yake atakapoondolewa, alinyamaza kwa muda kisha akasema ni jambo la kweli, lakini hapendi kulizungumzia.
“Jamani hili jambo umelijuaje, sikiliza ndugu yangu, mimi Waziri Kombani alinifuata pale ofisi za benki bungeni, akaniambia jambo hilo, lakini nilikataa hapo hapo na nilimueleza wazi kuwa siwezi kumsaliti kiongozi wangu kwa sababu hana kosa na anachokitetea ni cha kweli. Sikuendelea kusikiliza maneno yake, nilimuacha hapo benki,” alisema Kihwelu.
Baadaye gazeti hili liliwasiliana tena na Kombani na kumueleza kuwa kuna taarifa alikutana na Kihwelu na kumshawishi awe tayari kushika nafasi ya Dk. Slaa, waziri huyo alikana, na kueleza kuwa katika maisha yake yote bungeni hajawahi kufika katika ofisi hizo.
“Naomba mniamini, simo katika mkakati huo, hapo benki ya Bunge mimi sijawahi kufika na hata leo nilikuwa sina hela kabisa, lakini nilimtuma mtoto wangu benki akaenda kunichukulia. Mimi ni msafi, simo katika kashfa hizo,” alisisitiza Waziri Kombani.
Naye Simbachawene alipoulizwa kuhusu madai ya kushiriki kwake katika mpango huo alikana na kueleza kuwa, Dk. Slaa ni shemeji yake, hivyo hawezi kushiriki katika mpango wowote wa kumuumiza.
Simbachawene alieleza zaidi kuwa, ingawa hakubaliani na vitendo vya Dk. Slaa, hasa kutangaza maslahi ya wabunge, lakini hata kama yeye na wenzake wana nia hiyo, hawawezi kufanikiwa kwa sababu suala hilo halihusiani na kamati.
“Dk. Slaa ni shemeji yangu, siwezi hata kidogo kushiriki mkakati wowote wa kumuumiza. Mimi sikubaliani naye anapotangaza maslahi ya wabunge, kwanza tunalipwa kidogo sana kulingana na wabunge wenzetu wa nchi nyingine. Lakini hata kama mimi na wenzangu tuna mpango wa kumshughulikia, naamini hatuwezi kufanikiwa kwa sababu suala hilo halipo katika kamati yake,” alisema Simbachawene.
Tanzania Daima Jumatano ilipowasiliana na Dk. Slaa kuhusu madai hayo, alikiri kuwa anazo taarifa za kuwapo kwa mikakati hiyo, lakini haimtishi kwa sababu uenyekiti wa kamati si uhai wake, bali ni sehemu ya majukumu ya kuwashughulikia wananchi.
Alisema hashangazwi na hatua ya mawaziri hao kuandaa hujuma dhidi yake, kwa sababu anatambua kuwa mtu yoyote anapokuwa mwiba kwa serikali, lazima ifanye mkakati wa kumshughulikia.
“Nina taarifa kuhusu mipango hiyo, lakini mimi ni mbunge ninayejua majukumu yangu, jambo hilo halinisumbui. Hawa mawaziri wamepoteza mwelekeo, hawamsaidii rais, wanamuumiza. Niwaambie kwamba nikiletewa nyaraka hizo wanazoita za siri lakini zinaeleza ufisadi, nitazichukua wanikamate. Wakinikamata nitafurahi sana kwa sababu tutakwenda mahakamani, tutapambana, huko kila kitu kitajulikana kuhusu siri za serikali,” alisema. Alipoulizwa anavyojisikia baada ya kuzomewa na wabunge na hata kubezwa na Spika wa Bunge, Samuel Sitta kutokana na hatua yake ya kutaja mishahara na posho za wabunge alisema kwa kujiamini: “Hata Spika akiwa mkali ninapozungumzia mishahara na posho kubwa za wabunge, hanisumbui, kwani mara ngapi amenitaka nifute kauli zangu bungeni, kama sifuti au nafuta najua mimi. Mara ngapi ameniambia atanipeleka polisi? Muhimu afahamu kuwa jabali huwa halitikisiki.” Tangu kuanza kwa mkutano wa 15 wa Bunge, Dk. Slaa amekuwa katika wakati mgumu kutokana na wabunge kumshambulia kwa maneno na kumzomea anaposimama kuzungumza bungeni, wakimtuhumu kuwa amefanya kosa kutaja kiwango cha mishahara na posho wanazolipwa wabunge.
 
The

Sasa sijui watu wote waliohojiwa ilitokea by coincident wakawa in favour of Mengi au wale walioponda walieditiwa na kuondolewa wasisikike!!

Ukitaka kuliona hili vizuri angalia pia serikali/ccm inavyotumia vyombo vyake vya habari. Angalia pia magazeti kama Rai, Matanzania nk. I basically see the same trend. I really dont see why should Mengi/IPPMedia behave differently!
 
Mwana halisi habari hii ni yamuhimu hebu jaribu kuiweka vyema mkuu.
 
Kaika sherehe ya kuhitimisha shangwe za wakomboaji nchi....ambazo ziliandaliwa na mama anna malecela..wabunge wengi wamelaani vitendo vya viongozi wa nchi tena mawaziri kutetea mafisadi wanaokula nchi....jamani katika maisha yangu na uzee huu sijapata kuona waziri anatetea ufisadi hata siku moja....yaani wananchi wanateseka kule vijijini hutosikia hata siku moja viongozi wanaingilia kati kujua matatizo yao lakini inasikitisha kitendo cha kuwataja mafisadi papa watu wenye heshima zao wanadiriki kuwatetea mbela ya waandishi wa habari....inasikitisha lakini inaumiza sana napenda kuwaambia hata kama leo hii watamuumiza anna nawahakikishieni....huko nje kuna ANNA kibao...,nae mbunge wa vunjo mh maro alisema kwa kweli ndugu wananchi tunaitaji maombi yenu sana hapa mnapotuona kuna watu wanafikiria mengi mabaya juu yetu,,viongozi wa dini hakuna la kumshinda mungu...endeleeni kutuombea mungu atatulinda........kwa kweli inatia aibu sana sasa sijui wah kama wale unaweza kusimama nao mbeele ya wananchi wakakuelewa....anya way...hii ndio tanzania


Mhh naona hata kukusubiri uirekebishe siwezi....tupatie source tukasome wenyewe huko....
 
katika taarifa ya habari saa mbili usiku leo, mbunge ole sendeka amesikitishwa na kauli ya waziri sophia simba kuwasemea mafisadi na kuwatetea kuwa wao ni safi, badalla ya kuwasemea wafugaji, na wakulima wanaoteseka huko simanjiro na sumbawanga.

waliomwona akiongea ITV wataelewa hisia kaili alizokuwa nazo kuhusu vita dhidi ya maafisadi
 
Back
Top Bottom