Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Mwaka huu tutasikia mengi na si kutoka kwa Mengi tu bali kutoka kwa wengi maana kuna mengi yamejificha ndani ya vifua vya watu na sasa yatatoka tu, vinginevyo itakuja, "Uchiteme uchimumunye", sasa waliokula nyama, "wachiteme wachimumunye" waendelee kutete nyama zao

Halisi ninakubali. Inaonyesha kama vile wamekaa nayo siku nyingi na sasa kuliko kupasuka wameonelea bora kutoka na kuyasema hayo.
Mimi hapa niko neutral ila sielewi kwa nini kwa Mengi kusema anaonekana anajipendekeza!! Huu ndio ule upuuzi ambao mwana JF mmoja alisema ukiiba unaonekana mjanja na ukifuata sheria unaambia "anafanya kampuni kaa ya babake" and so forth..hii midset yetu ndo inatufanya wa TZ tunaibiwa mpaka mwisho nchi hio itakua skeleton daa...
 
Thanks a lot MwanaFalsafa1,lakini mbona CV hii nyembamba sana, kaolewa au kapera?Anauhusiano gani na Iddi Simba na KK?

-Ni Kimada wa Kitwana Selemani Kondo
-Anamiliki ukanda mrefu wa pwani ya Kusini ya Dar es salaam bila kuuendeleza
-Akishindwa chaguzi,KK anakwenda mwenyewe Ikulu kumuombea

Hili Jimama linatisha aisee labda KK afe
 
Mhh kazi ipo!
Hizi nafasi za ubunge wa bure (kuteuliwa) zifutwe. Mtu akitaka ubunge akajinadi kwa wananchi. Haya mambo ya NIPE NIKUPE ndio yametufikisha hapa tulipo.
 
SS anajulikana ni bogus dunia nzima...amewekwa pale sababu ya umbea. Wake na kuropoka kwenye vikao....yeye ndio kana kuna jambo kumvalisha paka kengele ni yeye humaliza....ni shujaa w a kifisadi mbona anajulikana ni mtii hata kwa JK??ndio maana yuko nae karibu......
 
Sasa mtu kama huyu ndio wa kuongoza utawala bora!? JK jaribu kuwa makini katika uteuzi wako vinginevyo nawe unatupa mashaka na UADILIFU wako..
 
Sofia Simba alitoa tamko la kwake tu, la kuwa tetea mafisadi kwa sababu azazozijua mwenyewe.
Leo Bungeni Waziri Mkuu ametoa tamko rasmi kuwa aliye dhuriwa na tamko la Mengi sheria inampa uhuru wa kuchukua hatua za kisheria ,reading between the lines ana mkana Sofia Simba na tamko lake la kifisadi.
Wakuu hamna mwenye data za waziri wetu Sofia?

Mkuu hebu angalia CV ya huyo mama (Sophia Simba (Tanzania) bonyeza hii website). Mimi naona imeungwa ungwa tu. Lakini nimeshangaa kuona kuwa alikuwa na certificate ya sheria na baadaye akaingia UDS kusome LLB. Je hii inaruhusiwa?
..
1982 1983 University of Dar es Salaam Undregraduate Student - Certificant in Law
1987 1991 University of Dar es Salaam Undergraduate Student - LLB Law..
Je CV inaandikwa kuwa ulikuwa mwanafunzi au ulihitmu? Siwezi kuamini kama hii CV imeandikwa na graduate tena waziri!!
 
Yawezekana wakati umefika' kipindi cha wao kupapatika' sie hata hatukujua wao wenyewe wanapakua na kupika' walaji tu wengi tunamiminika' hahitajiki mungu mwenyezi kufika' sie wenyewe tuzidi kuandika' yalojificha tujitahidi kuyaanika' nina imani kitaeleweka' mengi kasema yake tusipuuze ya ole sendeka' ni wakati wa kutenda si kukasirika' watanzania wengi tumeteseka na sasa tumechokaa'
 
Alicho fanya mtumishi si kumshambulia bali kamweleza ukweli tupu. Alipo nifurahisha ni ombi lake kwa maulana awachanganye mafisadi waparulane!

Mungu hujibu maombi ya watu, na iwe hivo mtumishi.

Eh! kwakweli nami namuunga mkono kwenye hilo ombi lake, na iwe hivyo waparulane, ukweli ujulikane,nchi ibadilike...
 
Masa,

Inawezekana Bashe huwa anaenda kwa Mwalimu Juma kule Urambo na kupata kizizi cha kumsaidia kidogo. Sasa akisifiwa na wale Mambumbu Manyamwezi, anakuwa kama senene aliyejificha kichwa na kuacha Kipengule chote juu. Mhaya akipita anamuona na kumchomoa.

FMes, kama ndiyo CCM mnaanda watu, basi andaeni wa maana maana huko Tabora naona hamna watu. Hawa wakipata nafasi kidogo tu, hata nyie watawauza. Tena Wanyamwezi ni kuwatafutia vibinti vyeupevyeupe na Kitaarabu kidogo, watakuwa kama Samson, tena hawa kama lilivyo joka, watatema wenyewe siri bila ya kuulizwa mara mbili. Kama Masha vilee pale Rose garden akipata kinywaji (nasikia).

Masa hebu leta tena ile picha ya Mwalimu Juma na utibabu wake.

Sikonge,

Leo asubuhi nimepata nafasi ya kuwasikiliza vijana wa CCM, nimeishiwa nguvu. Yaani hata kusoma hawawezi. Nilitamani kuwauliza nani kawaandalia hiyo taarifa? Hata mtoto wangu wadarasa la pili angesoma vizuri ile taarifa, akiweka vituo na msisitizo panapotakiwa. Kweli wajinga ndio waliowao! Watu wako kazini na hawaangalia nini kinaendelea duniani. Hata hivyo walisema mapema tu kwenye taarifa yao kuwa wamekuja Dar kuchangisha pesa. Kwa hiyo harakati za kuchangisha inabidi ziaze kwa kuwatafuta wachangiaji. Tayari wameshampta RA na kwa maana hiyo hata wale wengine wanne. Mungu awasaidie wafike salama!
 
Viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM wa Mkoa wa Tabora, wamemtaka Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, kuacha kutukana viongozi wa chama hicho na kama anataka siasa aingie kwenye chama chochote na kupambana na wanasiasa majukwaani. Sambamba na hilo, wamemtaka kuwaomba radhi wana CCM wa Tabora kwa walichadai ni kumkashifu na kumdhalilisha Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz kuwa miongoni mwa mafisadi papa watano aliowataja.

“Tunahoji nafasi yake ni nini kwenye CCM… Mengi ana historia ya kulumbana kwa kashfa na mawaziri wengi nchini, tunamtaka aache mara moja na kama anataka siasa aingie kwenye ulingo wa siasa na tutakutana naye kwenye majukwaa ya kisiasa,” alisema Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa, Patrick Kabaye, aliyesoma tamko la viongozi hao wa UVCCM Tabora mbele ya waandishi wa habari Dar es Salaam.

Kabaye aliyefuatana na Mwenyekiti wa UVCCM wa Mkoa wa Tabora, Robert Kamoga na wenyeviti wa UVCCM wa wilaya zote za mkoa huo, alisema wanalaani kitendo cha Mengi kumkashifu kiongozi wao ambaye wananchi wake wana imani naye.

“Tumefuatilia kwa karibu mwenendo wa ziara za Mengi akiwa na msafara wa wabunge, huku akitoa misaada mbalimbali na tumepata taarifa anakuja Wilaya ya Tabora, UVCCM inatoa angalizo kama misaada yake inaendana na kutukana na kuwaundia majina mabaya viongozi wetu, hatutavumilia hilo, wananchi wa Tabora wana matatizo, lakini wanaheshimu utu na viongozi wetu tuliowachagua kidemokrasia,” alisema.

Viongozi hao waliitaka serikali kuchunguza kauli za Mengi na kumchukulia hatua kali za kisheria ili iwe funzo na watu waheshimu utawala wa sheria. “Tunaiomba serikali iangalie upya sheria na matumizi haya mabaya ya vyombo vya habari ambayo yanaweza kuleta mtikisiko kwenye nchi na serikali ipige marufuku tabia hii ya Mengi kutumia umasikini wa Watanzania kupandikizia chuki watu wengine,” alisema Kabaye kwa niaba ya wenzake.

Walisema vijana hawatakuwa tayari kuwabeba wabunge mwaka 2010 wanaoshiriki katika ziara za Mengi ambazo wameziita zinakichafua chama na serikali kupitia kivuli cha kusaidia wanyonge. Viongozi hao wameeleza kumuunga mkono Rostam na kutokuwa tayari kuona anadhalilishwa bila kuwa na ushahidi wa jambo lolote na imani ya serikali haitaruhusu tabia ya watu kujitafutia umaarufu kwa gharama za kuchafua wengine.

Rostam ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Mjumbe wa NEC wa Mkoa wa Tabora na Kamanda wa UVCCM Wilaya ya Igunga. Kauli hiyo ya vijana hao ni mfululizo wa watu waliopingana na Mengi tangu kutoa tamko lake la kuwataja mafisadi papa watano kati ya 10. Wengine ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na watuhumiwa wenyewe akiwamo Yusuph Manji waliodai kauli hiyo inaleta uchochezi kwa jamii na kuonyesha ubaguzi wa rangi.
 
Sita shangaa kwa UVCCM Tabora kumtetea Rostam sio kitu cha ajaabu tena nyie mmekosea mngeandamana pindi Mh. "WENU" atakaporudi jimboni, kisha kiongozi wenu atoe hotuba ya kumponda MENGI. Kwani hata kina CHENGE na LOWASSA walipo tajwa na katika kashfa za ufisadi, kwenye majimbo yao walichinja nyama wakala, wakanywa na kusaza. Ndiyo, mlivyo zoea leo hii sio kitu cha ajabu sana ni SHUJAA wenu TABORA amkeni SHUJAA WENU wanamwita FISADI na Mnakubali haki ya nani tena!
 
halafu kama nilimquote msemaji wao akisema UMOJA WA VIJANA WA TAIFA. jamani jamani huu ni ubaklaji wa katiba. umoja huu ulianza lini na viongozi wake ni nani? mimi nijuavyo ni uvccm na si umoja wa vijana wa taifa.
 
Pinda comes to Mengi`s defence on corruption `sharks` comment

2009-05-01 14:55:17
By Bilham Kimati

Prime Minister Mizengo Pinda has defended IPP Executive Chairman Reginald Mengi, saying he exercised his constitutional right to air his views just like any other citizen.

Without mentioning directly Mengi`s name, the prime minister said, ``It is not proper to claim that the statement made was synonymous to deliberate abuse of privately-owned media outlets because anyone could have done that through any means of communication,`` Pinda clarified.

The prime minister was responding to a question by leader of the opposition in parliament Hamad Rashid Mohamed who inquired about disciplinary measures to be taken by the government against people allegedly misusing own media channels.

The prime minister quickly realized that the legislator was referring to a recent bold initiative taken by Mengi to name five individuals he said were implicated in serious corruption allegations.

He named five out of ten suspected corruption `sharks` whose names featured high on a list yet to be fully disclosed.

``He (Mengi) has exercised freedom of speech enshrined in the constitution. It is for those implicated to react. If they want to go to court it’s upon them to decide. It is better for Tanzanians to be careful when commenting on issues pending in court,`` Pinda said.

He said he should not be expected to stand up in parliament and pronounce a verdict on the issue because there were responsible institutions, such as the Tanzania Communications and Regulatory Authority, that could determine whether media regulations had been breached.

Pinda was answering a question during the PM's question time, which is usually held on Thursday morning covering a wide range of issues.

Among other issues raised was the presence in the country of a businessman, Chavda, who, in 1994, was ordered to leave the country after he was discovered to have swindled the government of millions of shillings through an abortive sisal investment scheme.

Zitto Kabwe (Kigoma North, Chadema) asked the prime minister whether he was aware that Chavda was still living in the country despite the deportation order.

``Personally I have no contact with Chavda and it becomes difficult for me to know whether he is in the country or not. If you provided me with some hints I could find out how he returned to the country against the order of the government,`` the PM said.

William Shelukindo (Lushoto, CCM) requested the government, through the ministry of Health and Social Welfare, to visit Kihitu village in his constituency where two pupils were killed and 40 others wounded by lightning that struck for the third time in mid March, this year.

Shelukindo wanted experts to find out reasons behind the recurring lightning and have the health status of the victims examined closely.

The prime minister expressed sympathy for the loss of the pupils and for those injured and pledged a close follow-up on the unusual incident.

The PM made the House burst into laughter when he quipped: ``Lightning in Lushoto? Had it been Rukwa I could understand that,`` evoking jokingly a mythical belief that Rukwa, the region he comes from, was leading in sorcery.

Regarding the fate of 520 employees at Kiwira coal mine who had gone for ten months without salaries, according to a question posed by Harrison Mwakyembe (Kyela, CCM), the prime minister said it was hurting to learn about the affliction of the employees.

``It is necessary for the government, in collaboration with other stakeholders, to find an appropriate solution to the problem. Sound investment would be appreciated and, if possible, Kiwira could be assisted to secure a bank loan to offset the current financial burden exceeding 800m/- and pay it back after coming on stream`,`` Pinda said.
 
tofauti iliyopo hapo ni kwamba huyo mchungaji ni mtu wa jamii yote, ni mtu anaejua mapenzi ya mungu na hayuko hapa kwa kumfurahisaha mtu, yupo kwa sababu ya mungu, na anajua kabisa kwamba hazina yake haiweki hapa ambapo nondo na kutu zinaiharibu, yeye anaweka kwa mungu
Mama Sofia Simba kwa upande wake yeye japokuwa ameteuliwa kwa ajili ya kuwasaidia watu bila kutegemea malipo, lakini yeye yupo bize kuwasadia watu ambao watamuwezesha katika maisha haya ya kupita, hebu angalia hizo mali ambazo wanalimbikiza watazitumia lini, kwa hiyo wanakuwa na hiyari watu wafe kwa kukosa dawa hili hali wana mapesa kibao ambayo hayana kazi na wameyaweka tu kwenye mabenki ya nje
papa mkubwa ni papa na papa mdogo..........., sasa yeye ndio anatafuta kufika pale kileleni na uwezi kufika bila kuwa karibu nao na uwezi kuwa karibu nao bila kujipendekeza na uweji kujipendekeza bila kuwatetea hadharani ili wajue upo upande wao
kaaazi kweli kweli
 
Nimekuwa nikifuatilia habari mbali mbali toka Mengi atoe tamko la "mafisadi papa". Nilicho gundua ni kwamba tokea atoe tamko hilo watu na hata makundi mbali mbali kila leo yanaitisha mikutano na vyombo vya habari. Wengi wao huongea pumba tupu na kuonekana ni kutaka tu umaarufu.

EVERYBODY IS SEEKING THEIR 15 MINUTES OF FAME!!!!!!

jE WOTE HAO WANA NIA NJEMA AU KITU CHA MAANA CHA KUSEMA? AU NI KUTAKA TU KUONEKANA NA KUSIKIKA?

Maana sawa ni vyema tamko la Mengi lime hamasisha watu kuongea iwe wana kubaliana na Mengi au la. Lakini. unakuta kuna watu wana jitokeza wanaongelea yale yale yaliyosha semwa na wengine au wana jitokeza na kuongea pumba tupu.

nimeona thread kuhusu wazee wa Yanga kumtetea Manji. Sawa kila mtu ana haki na mawazo yake lakini je ilikua na ulazima wao kutoka kwenye vyombo vya habari na kuongea?

Mara una sikia vikundi mbali mbali vya CCM. Leo sijui umoja wa vijana wa wapi kesho sijui kiongozi wa kundi gani. Jamani kuna ulazima wote mtokee muongee? Si muunde kauli moja kama chama badala ya kila mmoja kuji tokeza?

Katika hali yote hii nimeona kuna kupendelea kwenye tamko la watu wengi. Kuna BIAS kubwa sana. Leo wazee wa Yanga wanao fadhiliwa na Manji watokee kumtetea Mengi tena kwa kujiamini ina maanisha nini? Au kufanyika survey na kituo kinacho milikiwa na IPP na kuonyesha kwenye tv yao watu wote wakimsupport Mengi. Yote haya yana changia kupungu a kwa credibility.

NI WAKATI MUAFAKA WA KUSIKIA WATU AMBAO HAWA TETEI MASILIHI YAO WALA UPANDE WOWOTE ULE. MAANA WENGI TUNAO WASIKIA NI WATU WANAO JULIKANA MOJA KWA MOJA KUWA WATA TETEA UPANDE FULANI.

Jamani waTAnzania tuache kutafuta umaarufu wa kipuuzi. Tuache ushabiki tu. Haswa hawa wanaoji tokeza kwenye vyombo vya habari ongeeni kwa kutumia akili maana ukishaenda wazi kwenye umma unaweza kunakiriwa na unacho ongea wewe kika tumika dhidi yako baadae.

TUACHE UPAMBE NA KUJI PENDEKEZA. KAMA UTATETEA UPANDE MMOJA AU KUPONDA UPANDE MWINGINE FANYA HIVYO KWA KUTUMIA FACTS. KAMA UNA TOA PERSONAL OPINION BASI ISIWE YA KUPENDELEA(BIAS) AU ANGALAU IWE NA MISINGI

Tatizo ni kwamba kwenye matatizo kama haya ya kinchi kuna makundi mawili:

1.Wenye nia ya kweli na nchi(wachache sana)

2.Wanao tetea maslahi yao kwa kujidai wana tetea maslahi ya nchi(wengi sana)

Haya maoni yangu tu wana JF sijui nyie maoni yenu nini.
 
Ukweli ni kwamba watanzania wengi huwa tuna 'ROHO YA KWA NINI' hatupendi kuona mafanikio ya mtu mwingine!!!.

Mengi mwenyewe kwa namna moja au Nyingine amefanya vile kwa ajili ya kutetea maslahi yake binafsi na wala sio maslahi ya nchi. Hao kina Partel, Rostam na wengine walishazungumzwa sana kwenye swala la EPA sasa sijui yeye alirudia ili kupigia mstari jibu au vipi!!!

Kinachotakiwa kwa wadanganyika wengi ni kubadilisha 'ATTITUDES' zetu ili kuongeza kundi la wenye nia ya dhani na maslahi ya nchi.
 
hii issue ya Mengi nilishasema Tangu mwanzo ina Baraka za mkulu mwenyewe, na Mkulu alishaona Mikakati ya kina RA,EL,Kalamagi etc ya kutaka kumtoa kwenye power, Mkwere anatafuta pa kutokea na aliona ni Mengi pekee atakae weza kumtoa kimasomaso, Pinda mchezo mzima anaujua na ndio kisa nae kurudia kusema kama wanaona wamesemwa vibaya waende mahakamani,
 
Ukweli ni kwamba watanzania wengi huwa tuna 'ROHO YA KWA NINI' hatupendi kuona mafanikio ya mtu mwingine!!!.

Mengi mwenyewe kwa namna moja au Nyingine amefanya vile kwa ajili ya kutetea maslahi yake binafsi na wala sio maslahi ya nchi. Hao kina Partel, Rostam na wengine walishazungumzwa sana kwenye swala la EPA sasa sijui yeye alirudia ili kupigia mstari jibu au vipi!!!

Kinachotakiwa kwa wadanganyika wengi ni kubadilisha 'ATTITUDES' zetu ili kuongeza kundi la wenye nia ya dhani na maslahi ya nchi.

Mawazo yako si ya kweli, labda kama hujui hata chanzo cha ufisadi kujulikana Tanzanania, Mengi hajaanza leo kuwataja mafisadi, magazeti ya Mengi ( kulikoni na thisday ndiyo ya kwanza kuaanza kueleza nini kimefanyika kwenye ufisadi, na magazeti mengine yote yame copy and paste !! Kwa hiyo bila Mengi of course na vyombo vyake You wouldnt ever be able to know what happened in BOT, NSSF, PSPF richmonduli, etc. !!! So you need to see that Mengi is a fighter of the nation regardless of your personal conflicts
 
Hizo ni siasa za Sultani CCM kuwachanganya waTz ,tatizo ambalo nalishangaa ni Vyama vyetu vya upinzani kujihusisha na sakata linalowahusu mafisadi ,jamani hili ni kosa ,tena kosa kubwa sana ,katika mambo ya siasa ,unasapoti nini,unasapoti kitu gani ,unamsapoti nani na kwa nini ,ambacho kitasaidia upinzani ,kama tulitoka toka tulikotoka hatuwategemea wahusika ,ni kwa nini leo hii jua linazama tunawakumbatia na kuwaona wapo katika mstari mzuri ,hii ni aibu na kutokujiamini kabisa katika harakati tulizoanza nazo ni kupoteza dira ,kitu gani tumekikosea hata ikawa tunarudi na kutoa ubavu au sijui kukingia kifua ,kama tuonavyo CCM imegawika katika hali iliyojitokeza kati ya Mengi na wahindi kiasi kumeonekana kutoelewana kati yao.

Nini ameandika kwenye magazeti yake isiwe ndio asali ya kutuvutia na kuonja,hapana kuandika na kutangaza huko ni katika kunufaisha kundi kati ya makundi ya CCM au kambi kama zinavyojulikana ,kinachoonekana sasa ni kutaka kuwaburusa WaTz katika kambi hizo na kutugawa hata upinzani tuonekane tupo na kambi fulani.Na halafu ndio kazi ya magazeti bila ya kujali upande fulani.

Upinzani tuna kazi kubwa inayotukabili kupambana na Sultani CCM na makundi yake ,haitokuwa jambo jema kujihusisha na kundi fulani.
 
Back
Top Bottom