Mwizi aliyekuja kuiba saa tisa usiku

Mwizi aliyekuja kuiba saa tisa usiku

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Usiku wa kuamkia leo kibaka aliingia ndani na akafanikiwa kuchomoka na decoder ya Dstv, uzuri tukashtuka tukaanza kupiga kelele za mwizi huku tukimfukuza.

Tukiwa tunaendelea kumfukuza mwizi wetu, tukasikia tena kelele zikitokea kwenye nyumba jirani, mwizi huyo anaruka kaiba simu!!!! Majirani wakaunga tela kufukuza mwizi wa simu.

Wale wezi wakawa wamekimbilia njia moja, huku kelele zikiendelea, mwiziii huyoooo, kaiba dekodaaaaa. Kundi lingine, mwizi huuyooooo kaiba simuuuuu.

Baada ya dakika kadhaa mwizi mmoja kapiga kelele, wote tusimame, naye akasimama, tukawa kwenye bumbuwazi.
Mwizi wa dekoda akasema, mbona kundi kubwa linaniandama?

Mnaofukuza mwizi wa simu kaeni upande wa kushoto.

Mnaofukuza mwizi simu kaeni kulia.

Jamaa wakaenda kulia. Mwizi akasema kila mtu afukuze mwizi wake.

Akaanza Tena kutoka mbio ili tuanze tena kumfukuza🤣😂😅
 
Haya ni mafanikio makubwa ya awamu ya tano --- watu hawana tena hasira za umaskini za kumponda mwizi -- mwendo ni urafiki kwenda mbeli. Thanks kwa ushuhuda Bujibuji 🙂
Tabia hurithishwa, Wala tabia si sera ama itikadi, ila ni sehemu ya matunda ya utamaduni.
Tabia za CCM ni wizi, uhuni wa kila aina , ufisadi, fitina na roho mbaya. Ndio maana huku kwetu haikubaliki kabisaaaaaa
 
Huyu kibaka wa Dar na si mwizi, hata wafukuzaji wa Dar pia, nilishudia anapigwa mmoja zipu ikafunguka jamaa wakaacha kupiga wakamwambia "mshikaji funga basi zipu yako hapo chini" [emoji15][emoji15][emoji15]. Yaani kibaka anawapangia jinsi ya kumkimbiza!! [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Sisiemi imekujaje hapo sasa na wewe mbukulalo!???
 
Huyu kibaka wa Dar na si mwizi, hata wafukuzaji wa Dar pia, nilishudia anapigwa mmoja zipu ikafunguka jamaa wakaacha kupiga wakamwambia "mshikaji funga basi zipu yako hapo chini" [emoji15][emoji15][emoji15]. Yaani kibaka anawapangia jinsi ya kumkimbiza!! [emoji3][emoji3][emoji3]
Wanamezaga madawa
 
Back
Top Bottom