Mwizi wa simu anaepigwa hapa kariakoo mda huu ni hatari sana

Mwizi wa simu anaepigwa hapa kariakoo mda huu ni hatari sana

Wizi siyo, si Jambo zuri Hata nukta.

Ukisema Watu wa bongo mbona hamna utu moyoni, kuchoma Mwizi.

Maisha yenyewe ya manati kwa Watu Wengi, ukikwapua unarudisha Mtu nyuma na msongo kibao.


Simu,Nakumbuka nikiwa vidato vya awali shule ya Upili.

Nilikuwa na Simu Nokia aina 1110, Miaka(Miaka ya fagalia- wawa,)hiyo kuwa na Simu nadra sana Tena Kwa bwana mdogo wa shule ya Upili.

Ukikamatwa na Simu linakuwa tukio kubwa mbele ya umati wa Shule nzima, ukisubir kufukuzwaa shule.

Sijuii nimuite, mjanja au fala au bwege, nimuite kibaka mwizi Asiye na punje ya utu moyoni,

Aliniotea nimelala akaichomoa kwa mfuko, maana Simu nilikuwa nairinda mithili ya holy grail ya Dan brown au Almasi adimu.

Aisee karibia Wiki nzima nilikuwa Kama mgonjwa sonona, kushitaki huwezi, kuanzisha varangati chini chini lazima kisanuke,

Hapo hapo tukiwa tunaelekea kufanya mitihani tukianza na somo la bible knowledge (Maswalii ya hapa na palee Isaac means laugh).

Wizi sio, wazi haufai lakini ndio social ills, Hasa Uchumii ukiwa unayumba yumba Kama mdomo wa kuberi au uchumii ukiwa hoi bin taabani au ubepari uliookomaa haswa.

Jamaa mmoja wa Singapore anasema unaweza sahau laptop au bag njianii au garden kesho yake ukalikuta Pale pale, Wow that's Amazing.
 
Kapicha kidogo mkuu! Rai yangu kwa raia tuache kujichukulia sheria mkononi, tuna vyombo vya ulinzi kama polisi ndivyo vina haki na wajibu wa kutoa adhabu kwa mtuhumiwa yeyote yule nchini.
Wamdedishe tu hata mm wamewahi kunipiga simu simu kwa staili hiyo waliniambia eti nimekanyaga nyanya kugeuka tu mwingine akachukua simu mamaye zao
 
Anapigika sana na jezi yake ya makolo
 
Back
Top Bottom