Mwizi wangu namjua, nipeni mbinu za kumkamata

mimi mtakatifu

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2019
Posts
248
Reaction score
539
Jana yamenikuta!

Nilienda zangu tips kuinjoi weekend baada ya uchovu wa kazi overtime.

Nikakutana na msichana mrembo haswa tukasimama meza moja tukaanza kula kilaji huku tukipiga story na kufahamiana. Nilivutiwa na maongezi yake as alionekana ni dada anaejielewa mtu wa biashara anafunga mzigo mpaka Dubai.

Kilaji kikakolea tukaanza kutongozana, mtoto akanielewa nikaondoka nae nikapiga mzigo. Nachokumbuka mara ya mwisho ni ananivalisha kinga baada ya hapo nilikuja stuka saa 5 kasoro asubuhi, sijui aliniwekea nini.

Nimestuka nipo peke yangu, simu yangu macho matatu haipo na wallet imeachwa nyeupe ina cards tu.

Nimeshafungua kesi polisi, ila wakati nataka kuwatafuta watu wa cyber nikakumbuka tulipeana namba mwanzoni kabisa kabla hatujafikia kutongozana.

Sasa naomba mnisaidie wadau jinsi ya kumnasa huyu mwizi wangu maana mpaka sasa nna namba yake ipo hewani ila sijafanya lolote nafikiria namna ya kumnasa. Najua nikimpigia atakimbia au atazima simu maana yeye anafikiri kuondoka na simu yangu namba yake ameondoka nayo kumbe technology sasa namba haikai kwenye simu.
 
Mfanyabiashara anaefungua mzigo adi Dubai anaiba simu? au sasa unaweza kusema kua ni mtu wa aina gani ili nikupe mbinu.
Je hapo mlipokutana ni ugenini kwa wote? make mlipiga stori kabla.
Je ukimpata unataka kufanyeje..
 
Nahisi ni changu tu sema ana exposure, pia nahisi aliniwekea kitu tukiwa chumbani ili nizime.

tumekutana tips ni pub ipo mikocheni.

mimi nachotaka ni simu yangu tu wala siitaji kumfanya kitu kingine maana atanipotezea muda.
 
Ok..huyo ni changu hivyo simu yako atakua ameitunza sehemu kusikilizia kama kuna chochote kabla ya kuipiga bei.

Tafuta rafiki yako mnaeshibana sana umpatie mawasiliano ya huyo dada then apange nae apointment ya kupigana miti...hapo ndo oportunity ya kumbana na polisi.

Taadhari akikisha kua hamfiki mahakamani wala kuwekewa dhamana kabla ya wewe kupata ukweli ilipo simu yako. Taadhari hii inatokana na jembe wengine wanaomtafuta huyo demu kuingilia kesi kisa chakula chao anashiliwa polisi.
 
Tuma hela kwenye namba yake jitahidi iwe ya kumshawishi halafu kausha kimya mpaka kesho yake.

Ikifika kesho mpigie, mwambie kuna hela uliituma kimakosa kwake, mwambie kama bado ipo akurudishie nusu,ila kama keshaitumia basi ni sadaka. Hapo kama demu ni lidangaji litasema liliitumia, baada ya hapo chati nalo mara mojamoja nataka sitaki kama wiki nzima halafu siku liombe mkutane, nakwambia litajileta lenyewe.
 
Mfanyabiashara anaefungua mzigo adi Dubai anaiba simu? au sasa unaweza kusema kua ni mtu wa aina gani ili nikupe mbinu.
Je hapo mlipokutana ni ugenini kwa wote? make mlipiga stori kabla.
Je ukimpata unataka kufanyeje..
Jamaa hakuelewa ni dubai ya dar, wauzaji wengi hujifanya wana biashara
 
Jana yamenikuta!

Nilienda zangu tips kuinjoi weekend baada ya uchovu wa kazi overtime.

Nikakutana na msichana mrembo haswa tukasimama meza moja tukaanza kula kilaji huku tukipiga story na kufahamiana. Nilivutiwa na maongezi yake as alionekana ni dada anaejielewa mtu wa biashara anafunga mzigo mpaka Dubai.

Kilaji kikakolea tukaanza kutongozana, mtoto akanielewa nikaondoka nae nikapiga mzigo. Nachokumbuka mara ya mwisho ni ananivalisha kinga baada ya hapo nilikuja stuka saa 5 kasoro asubuhi, sijui aliniwekea nini.

Nimestuka nipo peke yangu, simu yangu macho matatu haipo na wallet imeachwa nyeupe ina cards tu.

Nimeshafungua kesi polisi, ila wakati nataka kuwatafuta watu wa cyber nikakumbuka tulipeana namba mwanzoni kabisa kabla hatujafikia kutongozana.

Sasa naomba mnisaidie wadau jinsi ya kumnasa huyu mwizi wangu maana mpaka sasa nna namba yake ipo hewani ila sijafanya lolote nafikiria namna ya kumnasa. Najua nikimpigia atakimbia au atazima simu maana yeye anafikiri kuondoka na simu yangu namba yake ameondoka nayo kumbe technology sasa namba haikai kwenye simu.
Pole sana! Mwenyewe ulijiona umepata, kumbe umepatikana!! 😇 Mambo ya mjini hayo. Huku Kijijini niliko, huwezi kuyaona kabisa.
 
Back
Top Bottom