Kididimo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2016
- 4,153
- 3,800
Ni maoni yangu:
Kwa kuwasikiliza viongozi wetu wa juu wa chama, kuna dalili ya kurudi mfumo wa utawala wa chama kimoja.
.Sina takwimu ni Watanzania wangapi wangependa iwe hivyo,japo hakuna aliyejitokeza waziwazi ndani ya chama Tawala kusemea hii trend.
Athari mojawapo kubwa ni kuwa na utawala wenye kusikiliza upande mmoja wa shilingi kama ilivyokuwa katika utawala wa Mwl. Nyerere. Maana yake tutakuwa na proposers tu wa mbinu za kukuza uchumi, huduma za jamii nk .
Hii kwa hali ya Ufisadi na ujanja wa viongozi wetu,huenda tukajikuta kwenye hali ileile hasa mwishoni mwa enzi za Mwl. Nyerere. Tulijenga Viwanda vingi, vikahujumiwa na walewale wenye chama huku wakiwaficha wananchi.
Na ndiyo maana Mwl. Nyerere miaka ya 90, akashupalia mfumo wa vyama vingi. Kimsingi hakutaka upinzani uongoze nchi,bali uwepo kuikosoa serikali kwa yale mabaya.
Na kwa njia hiyo, wananchi wangechambua na kupata ukweli. Pia ungefanya viongozi waliopo madarakani kuwa makini zaidi.
Kwa hali ilivyo sasa na uzoefu wa Uchaguzi wa Serikali za mitaa wa Nov. 2019, kuna uwezekano huu:
1. Vyama vya upinzani vikasusia, uchaguzi Mkuu 2020 kikabaki chama kimoja.
2. Maana yake tutakuwa na uchaguzi au uteuzi wa upande mmoja, bunge la chama kimoja nk.
3. Tutaanza kuoneana aibu kiutendaji. Yawezekana ukali uliopo sasa ukatoweka kwa vile hakuna mshindani.
4. Huo utakuwa mwanzo wa kurudi tulikotoka.