semenya Binafsi nimeshukuru na kufurahi na changamoto yako, lakini naomba kukuliza wewe mwenyewe ungekuwa kwenye kamati ya kuscreen watu wa kuwapa Nobel Prize ungeweza kumteteaje mwalimu JKN kuwa apewe na anastahili hiyo award/prize? Maana katika bandiko lako unasema kafanya mengi kwa bara la Africa mengi yepi? Nobel Prze zilianzishwa na mtu ambaye alilaani vita JKN alipigana vita na Uganda, vita ambayo hata hapa JF tumequestion mantiki yake. Sababu alizosema tulikuwa nazo za kwenda uganda leo hii wengi wetu hatuzioni?? wangapi walikufa Uganda? kwa kufa kiasi hicho cha watu tayari anakuwa disquliafied kupata NOBEL.jamani mwaka 1984 Desond Tutu alipata Nobel Peace prize, me nachoshangaa kuona mtu kama mwalim JK Nyerere hakuwahi kupata tuzo hiyo...sababu moja nayoona ni kwamba Mwalim alikua anapenda socialism, labda ndo maana hawakumpa...nikifika kwenye hayo mawazo napata pia wasiwasi na hizi tuzo.....nikiangalia Obama na JK Nterere na Tutu, hata mandela mwenyewe hawajafanya makubwa kwa waaFrica kama Nyerere....mnaonaje hili jamani? Me naona alistahili kupewa....
mkuu tutu kapewa mwaka 1984, unataka kuniambia mwalim hakustahili hata kipindi hicho?It is water under the bridge. Mwalimu mchango wake mkubwa ulikuwa barani Afrika na enzi hizo Afrika haikuwa na uzito wowote katika medani ya siasa za kimataifa.
Mbogela,semenya Binafsi nimeshukuru na kufurahi na changamoto yako, lakini naomba kukuliza wewe mwenyewe ungekuwa kwenye kamati ya kuscreen watu wa kuwapa Nobel Prize ungeweza kumteteaje mwalimu JKN kuwa apewe na anastahili hiyo award/prize? Maana katika bandiko lako unasema kafanya mengi kwa bara la Africa mengi yepi? Nobel Prze zilianzishwa na mtu ambaye alilaani vita JKN alipigana vita na Uganda, vita ambayo hata hapa JF tumequestion mantiki yake. Sababu alizosema tulikuwa nazo za kwenda uganda leo hii wengi wetu hatuzioni?? wangapi walikufa Uganda? kwa kufa kiasi hicho cha watu tayari anakuwa disquliafied kupata NOBEL.
Ukiangalia hotuba zake, tafuta hata You tube zipo utaioona hotuba moja anayosema kuwa aliombwa apatanishwe na Idd Amin lakini kwa maneno yake mwenyewe anasema aliwauliza watu wanaosema kuwa aache kumpiga Idd Amini kuwa walikuwa wapi??? Sasa Mkuu Nobel Prize haaziendi kwa Jicho kwa jicho, zinaenda kwa ukipigwa shavu la kushoto geuza la kulia.
Desmond Tutu siku moja alipokuwa anatembea mtaanzai aliona Mob wanamtandika kijana alienda akamwangukia juu akamfunika watu wakaanza kumpa kibano yeye mpaka alipookolewa na dola. Nelson Mandela alipoteza uraia wake kwa kuchoma Passport, kuna watu wameadnika Historia kubwa sana kama akina Steve Biko, Chris Hann, Bob Moses lakini bado hawajatambuliwa.
JKN alihamisha watu kutoka kwenye vijiji vyao kwa nguvu, watu wengi walipigwa na migambo, walichomewa nyumba zao, walipoteza mifugo, waliliwa na simba, acha waliokufa kwa maralia, Taifodi, vipindupindu kwenye maeneo waliyowekwa yasioyofaa kwa maisha ya Binadamu.
JKN alitaifisha mali za watu kwa azimio lake la arusha (hii ni sawa na anachofanya comrade Mugabe-Jongwe)
Pitia vigezo vya Nobel alafu toa mchanganuo cha alichofanya JKN kuweza kutunukiwa hiyo Prize. Ni Mtazamo Tu
Richard,Lakini wakulu hii Nobel Prize ilianzishwa katika kumuenzi yule mzungu Alfred Nobel kupitia mfuko wa Nobel yaani Nobel Foundation.
Mfuko huo unatoa tuzo kwenye maeneo ya Sayansi, Fisikia, Kemia, Madawa, Fasihi na mwisho ni hio Amani.
Sasa ukifanya jambo la maana la ama kuvumbua au kutatua kama si kutafuta suluhisho la suala moja kati ya hayo basi jina lako linaweza kuorodheshwa katika orodha ya wanaopendekezwa kupewa tuzo mojawapo.
Kuna orodha ndeefu ya waliowahi kupewa tuzo hio lakini tuangalie wachache
1964 - Martin Luther King Jr.
1984 - Desmond Tutu
1993 - Nelson Mandela, F.W. de Klerk (hii bado najiuliza)
1994 - Yasser Arafat, Shimon Peres, Yitzhak Rabin (hawa pia sielewi)
2001 - United Nations, Kofi Annan
2004 - Wangari Maathai
Raisi Obama alikuwa ni miongozi mwa wale waliopendekezwa kupewa tuzo hio na akapewa.
Sasa si kuna Nyerer Foundation nao wangejaribu kutoa mfano kwa kutoa tuzo kwa watanzania mbalimbali halafu baadae kwa waafrika kama ikiwezekana.
Anashindwa kumfahamu Nyerere na undergorund zake ,msione watu wanapewa hizo Nobel mkaona ni mambo ya kuonekana ukiwa mstari wa mbele ,unachunguzwa sana sana kiasi ya kutoonekana ni mnyanyasaji na mwenye kubeba lawama ,Nyerere amevamia Zanzibar ,amevania Uganda amevamia Malawi kuna watu wametoweka katika Tanzania chini ya utawala wake na hawajulikani walipo hadi leo ,sasa hayo mambo wanaotoa hiyo Nobel wanayafuatilia japo ni shutuma na hazina ushahidi lakini ni madoa ambayo hayatakiwi yawepo. Sasa huo utakatifu mliombatiza kwani haujamtosha huko aliko ? Obama huyo hapo hata mwaka hajatimiza amepewa Nobel ,watu serikalini wamejaa utajiri usiojulikana wameupata vipi afu mnataka kiongozi bado apewe na Nobel ? Nyie vipi ?We semenya vipi??????hii umeiposti mara ngapi humu???????
Hii thread ya tatu but topic ni hiyo hiyo,why????
We nyerere ni babu yako wa damu nini???????