Mwl. Nyerere aliuliza, Ukabila una kazi gani?

Mwl. Nyerere aliuliza, Ukabila una kazi gani?

Nchi hii Ina matatizo mengi ya ukabila Kuna taasi kubwa nyingi wamejazana watu wa kasikazini mbona hamkemei
Ukabila upo Tanzania na unafanyika waziwazi tu ila watu wametulia tu kama vile hawaoni.Kuna wapumbavu wao wakipewa nafasi tu ktk vitengo wanaanza kujaza watu wa kabila lao,ndio maana shughuli nyingi Tanzania zinakosa ufanisi kwa sababu watu wamepewa vitendo sio kutokana na uwezo wao bali kabila lao.
 
Barack Obama?
Rish Sunak?

Ukabila ni ujima.

Nyerere alikuwa mbele ya wakati wake katika hilo.
 
Mwl Nyerere, ila leo kunakitu. Jambo hili la ukabila Mwl alikemea sana; dalili au viashiria vyake, hongera Mwl. Leo hii tena baada ya miaka mingi kuna hisia za viongozi kutaka kupanda mbegu za ukabila. Tunaona kanda ya Wasukuma inaonesha bila wao, CCM itashindwa; viongozi wanahonga vyeo Wasukuma ili waichague CCM, jamani!

Uteuzi wa Biteko Doto, juzi uteuzi wa Makonda kisa ili Wasukuma wajue kuwa wao bado miamba hii kweli kwa Watanzania ni dhana mpya ili kujenga element za ukabila. Tunajifunza, Mwl alichaguliwa na Watanzania akiwa anatokea kwenye kabila dogo sana, Wazanaki; pia Mkapa kwa Wa Makua na Kikwete Wakwele. Hatujawahi taifa hili kuwaogopa Wasukuma.

Ikitokea Watanzania wakajua hili, ukabila uko njiani; kesho Wanyakyusa wataanza nao kuogopwa. Niliombee taifa letu, sisi tayari tumeshaunganishwa, hatuna ukabila.
Tulisema muda mrefu, ukiua njia halali za kidemokrasia ambayo ni kupitia vyama vya siasa. Upinzani utageuka kuwa wa kikabila, kidini ama ukanda. Utawala wa magufuli utakuwa na mkono wake kwenye hizi siasa za ukabila zinaonea kwa kasi Sasa. Na haya kwa ujumla wake yamechangiwa na kuacha chama kimoja kukaa madarakani muda mrefu kwa shuruti bila ridhaa ya wananchi.
 
Nchi hii Ina matatizo mengi ya ukabila Kuna taasi kubwa nyingi wamejazana watu wa kasikazini mbona hamkemei
Hizo taasisi zenye watu wa kaskazini unaruhisiwa kuzikemea, au unataka wengine wakemee kwa niaba yako? Mfano mrahisi ungesema taasisi Fulani ya umma imejaza hao watu wa kaskazini, tuone mahusiano Yao na utawala uliopo au zilizopita.
 
Unataka kusema sa100 anaendekeza ukabila kuliko alivyokuwa hayati Nyerere au imekaaje ? Hao viongozi wa kanda ya ziwa uliowataja ni karata ya kupata Kura Kwa kanda ya ziwa yenye idadi kubwa ya wapiga Kura na kurudisha mvuto wa Raisi hususani Kwa mgongo wa hayati Jpm. Huo ukabila alifanya muhasisi na hadi wengine wanafuata haswa Kwa makabila yenye idadi kubwa ya watu na bado Mila zao wanazidumisha kama wasukuma .
Kwani kura zina nguvu kiasi hicho Hadi wasukuma wategemewe? Isitoshe hata hiyo ccm haina uhakika wa kushinda kwa wingi hivyo huko kwa wasukuma, Bali kwa kutumia Hila zaidi. Hakuna uhakika kuwa magufuli alikuwa na mvuto hivyo huko kanda ya ziwa, maana chini ya urais wake hakuwahi kuruhusu uchaguzi wa haki ili tupime kukubalika kwake.

Sio propaganda ya vyombo vya habari kwakuwa alividhibiti ionekane kuwa alikuwa na mvuto hivyo huko Kanda ya ziwa.
 
hilo neno usiende kuliongea uchagani. watakushangaa. kwanini aliwachukia wachaga? kwanini wachaga hata wakifaulu walikuwa hawapati nafasi na wakipata watapelekwa sumbawanga au ruvuma? kwani ukabila ni nini? ukabila ni kupendelea kabila lako, au kutofanya kitu kwa kabila fulani kwasababu tu watu hao ni member wa kabila fulani. hata hivyo kuna ukabila mzuri na mbaya. ule wa kurundika watu wa mkoa wako kwenye vyombo vya ulinzi ilikuwa na faida sio ya kutenganisha watu ila kuzuia coup detat, na ile ya kutowapa nafasi za shule wachaga ilitaka wote tuwe level sawa. hata sio vibaya. kuna mangi alikuwa akipata division one na pembeni kuna mfipa kapata division three, atachukuliwa mfipa na mangi ataachwa au atapelekwa mkoa wa mbali kabisa huko. sisemi hii ilikuwa mbaya, ila hatuwezi kuuita sio ukabila. come into your senses.
Aliona ni wakabila sana ndiyo maana alipambana kvunja himaya yao na hata hivyo alifanikiwa sana tena sana.Pia naomba ujue kuwa hakuna kabila lenye wasomi halali kama Wachaga.
 
Kwani kura zina nguvu kiasi hicho Hadi wasukuma wategemewe? Isitoshe hata hiyo ccm haina uhakika wa kushinda kwa wingi hivyo huko kwa wasukuma, Bali kwa kutumia Hila zaidi. Hakuna uhakika kuwa magufuli alikuwa na mvuto hivyo huko kanda ya ziwa, maana chini ya urais wake hakuwahi kuruhusu uchaguzi wa haki ili tupime kukubalika kwake.

Sio propaganda ya vyombo vya habari kwakuwa alividhibiti ionekane kuwa alikuwa na mvuto hivyo huko Kanda ya ziwa.
Fact.
 
Back
Top Bottom