Mwl. Nyerere aliuliza, Ukabila una kazi gani?

Nchi hii Ina matatizo mengi ya ukabila Kuna taasi kubwa nyingi wamejazana watu wa kasikazini mbona hamkemei
Ukabila upo Tanzania na unafanyika waziwazi tu ila watu wametulia tu kama vile hawaoni.Kuna wapumbavu wao wakipewa nafasi tu ktk vitengo wanaanza kujaza watu wa kabila lao,ndio maana shughuli nyingi Tanzania zinakosa ufanisi kwa sababu watu wamepewa vitendo sio kutokana na uwezo wao bali kabila lao.
 
Barack Obama?
Rish Sunak?

Ukabila ni ujima.

Nyerere alikuwa mbele ya wakati wake katika hilo.
 
Tulisema muda mrefu, ukiua njia halali za kidemokrasia ambayo ni kupitia vyama vya siasa. Upinzani utageuka kuwa wa kikabila, kidini ama ukanda. Utawala wa magufuli utakuwa na mkono wake kwenye hizi siasa za ukabila zinaonea kwa kasi Sasa. Na haya kwa ujumla wake yamechangiwa na kuacha chama kimoja kukaa madarakani muda mrefu kwa shuruti bila ridhaa ya wananchi.
 
Nchi hii Ina matatizo mengi ya ukabila Kuna taasi kubwa nyingi wamejazana watu wa kasikazini mbona hamkemei
Hizo taasisi zenye watu wa kaskazini unaruhisiwa kuzikemea, au unataka wengine wakemee kwa niaba yako? Mfano mrahisi ungesema taasisi Fulani ya umma imejaza hao watu wa kaskazini, tuone mahusiano Yao na utawala uliopo au zilizopita.
 
Kwani kura zina nguvu kiasi hicho Hadi wasukuma wategemewe? Isitoshe hata hiyo ccm haina uhakika wa kushinda kwa wingi hivyo huko kwa wasukuma, Bali kwa kutumia Hila zaidi. Hakuna uhakika kuwa magufuli alikuwa na mvuto hivyo huko kanda ya ziwa, maana chini ya urais wake hakuwahi kuruhusu uchaguzi wa haki ili tupime kukubalika kwake.

Sio propaganda ya vyombo vya habari kwakuwa alividhibiti ionekane kuwa alikuwa na mvuto hivyo huko Kanda ya ziwa.
 
Aliona ni wakabila sana ndiyo maana alipambana kvunja himaya yao na hata hivyo alifanikiwa sana tena sana.Pia naomba ujue kuwa hakuna kabila lenye wasomi halali kama Wachaga.
 
Fact.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…