Mwonekano mzuri huvutia kuanzisha Mahusiano, Utu au Tabia nzuri ndio hudumisha mahusiano

Mwonekano mzuri huvutia kuanzisha Mahusiano, Utu au Tabia nzuri ndio hudumisha mahusiano

Blue G

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2012
Posts
5,339
Reaction score
3,667
Habarini Wana MMU,

Nimekuwa nikijaribu kufikiria hii kauli ya "mke sio sura bali tabia" na matumizi yake,wengi hasa vijana wa siku hizi wanaichukulia kauli hii kama kauli iliyopitwa na wakati hasa kwa kuwa vijana wengi siku hizi ni wazee wa pisi kali wakiamini kuwa na pisi kali au smart handsome guys katika mahusiano,kutawafanya wawe na furaha,hamasa na kufarijika sikuzote za mahusiano yao just kwa kuangalia tu na kufurahisha macho kwa uumbaji makini wa muumba.

Binafsi nina maoni tofauti kidogo, nadhani mwonekano mzuri una nafsi ndogo sana kwenye mahusiano(unless otherwise uwe unaolea au unaolewa for macho ya watu au sifa kutoka kwa watu jamaa ana mke mzuri au Fulani ana mume mzuri sana) nafasi ya mwonekano hasa ni pale ambapo mtu huamua kuingia kwenye mahusiano,mwonekano humvuta kisha kazi ya mwonekano huishia hapo, kinachofuatia hapo ni utu au tabia ya mtu ambayo ndiyo ina nafasi kubwa sana ya kuamua mstakabali wa mahusiano yoyote yale, eiza yawe mazuri,mabaya,matamu,machungu,yadumu au yaishie njiani.

naomba nieleweke vizuri hapa simaanishi watu wasijali kuhusu mwonekano wapendwa lakini ebu karibuni tujadili kwa pamoja wengine mna maoni gani juu ya mwonekano? Nini nafasi ya mwonekano katika mahusiano? Inawezekana mwonekano pekee ukatosha kudumisha mahusiano? Kuna mtu amewahi kushuhudia mahusiano au ndoa ambayo imedumu kwa ajili ya mwonekano wa wahusika au mhusika mmojawapo?

Karibuni tujadili kwa pamoja
 
ukioa mwanamke mwenye sura mbaya kwa kigezo Cha tabia nzuri utawahi kumchoka


Kuna pisi Kali zinajielewa japo sio zote.
Uko sawa kiongozi ndo maana pale juu nimekazia kuwa simaanishi mtu asijali kuhusu mwonekano wa mtu anayetaka kwua naye kwenye mahusiano,ila ningependa tu kujua nini mtazamo wako juu ya nafasi ya mwonekano katika mahusiano?mwonekano unaweza kudumisha mahusiano?

Lakini pia nikukumbushe tu mkuu kuna wanawake wakipatiwa nafasi licha ya mwonekano labda mbaya kwa maoni yao wewe muhusika,ila kwa sababu ya utu wao au tabia zao baada ya muda wanaweza kukufanya uhisi Maisha bila uwepo wao yanaweza kuwa magumu sana kiasi ikafikia wakati usiuone ubaya kabisa kwake na ukawa husikii wa huoni ukafika mazima kabisa
 
Ndoa/mahusiano hudumishwa na upendo ulio kati ya wahusika, tabia/muonekano havijawahi dumisha mahusiano ikiwa hakuna upendo.

Kuna watu wana tabia mbaya/hawana muonekano mzuri bt mahusiano yao yamedumu ajili ya upendo baina yao.
 
Ni mwendo wa kuangalia muonekano wa nje chura na shape kwanza tabia tutarekebishana ndani ya Ndoa, ndiyo maana ndoa nyingi siku hizi hazidumu.
Mvuto kwanza, tabia mtatumia za kwako bwana. Ukiona haijadumu ujue tabia zako hizo ndio hazifai inatakiwa uzibadilishe.
 
Ni mwendo wa kuangalia muonekano wa nje chura na shape kwanza tabia tutarekebishana ndani ya Ndoa, ndiyo maana ndoa nyingi siku hizi hazidumu.
sure kiongozi ni kama tunajisahau sana kukubali kuwa mwonekano una sehemu ndogo sana katika kuyafanya mahusiano yadumu,tunaupa mwonekano kipaumbele sana kiasi tunasahau kabisa kuwa kuna mengi yatahitajika huko mbeleni Zaidi ya mwonekano
 
ndoa/mahusiano hudumishwa na upendo ulio kati ya wahusika, tabia/muonekano havijawahi dumisha mahusiano ikiwa hakuna upendo.

kuna watu wana tabia mbaya/hawana muonekano mzuri bt mahusiano yao yamedumu ajili ya upendo baina yao.
kiongozi unamaanisha upendo ndio kila kitu,bila kujali tabia au mwonekano?

say umempenda binti lakini labda ni mchoyo,mchafu,katili still utampenda kwa sababu tu unampenda?na mtadumu tu kwa sababu unampenda bila kujali anakutendea vipi wewe,jirani watoto au ndugu zako na wake pia?
 
Back
Top Bottom