cadey
JF-Expert Member
- Oct 14, 2014
- 1,455
- 4,419
Siku 4
Thumb up, keep on pushing pushing kazi nzuri wana siku ngapi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Thumb up, keep on pushing pushing kazi nzuri wana siku ngapi?
Hao wamekuwa maana vifo vingi hutokea siku ya kwanza na pili, na siku zinavyoongezeka vifo hupungua na huisha kabisa.Siku 4
Je nitawapa tuu hizi chanjo ,vip kuhusu vitamins za kuchanganya kwenye maji zina umuhimu wowote?Fanya hivi;
- Siku ya 7 wape chanjo ya mdondo/Kideri kwa njia ya maji au matone
- Siku ya 14 wape chanjo ya gumboro kwa njia ya maji
- siku 21 rudia chanjo ya mdondo/kideri kwa njia ya maji au matone
Zingatia: Baada ya siku 21, utarudia kuchanja kideri baada ya siku 90 ambayo ni sawa na miezi mitatu (3) na unakua unarudia hivyo kila baada ya miezi 3.
- Siku ya 28 rudia chanjo ya gumboro kwa njia ya maji.
- Wiki ya 6-8 chanja Ndui kwa njia ya sindano hii unachoma kwenye utando laini kwenye bawa.
- Wiki ya kumi na mbili (12) chanja Homa ya matumbo ( salmonellosis) hii unachoma kwenye nyama hasa pajani.
Je nitawapa tuu hizi chanjo ,vip kuhusu vitamins za kuchanganya kwenye maji zina umuhimu wowote?
Je aloevera,mwarobain na mlonge naweza kuwapa wakiwa na umri gani?Hii inategemea na mfugaji na aina ya ufugaji mtu au hata mazingira ya ufugaji.
Wafugaji wengi wanafanya kuwapa vitastress baada ya kuwapa chanjo hii inasaidia kuwachangamsha kuku maana wanapokunywa wale virusi huwa kuna mabadiliko ya miili yao, so vitamini inafanya kuwa boost kiasi.
Ila wengine pia hawatoi hizo vitastesss na kuku wanakuwa vizuri tu bila shida, so ni wewe mwenyewe kuchagua uwape au usiwape.
Hizo njia naturally sijafahamu kwa kweli sitaki kukuongopea, lakni ukienda kwenye mitandao utazikuta na wameelezea hadi namna ya kuandaaJe aloevera,mwarobain na mlonge naweza kuwapa wakiwa na umri gani?
Hali ya hewa ndani ya banda iko vipi mkuu? Na msimu huu wa mvua wafugaji wengi huwa wanajisahau wanafunga madirisha yote hivyo kutukuruhusu hewa safi ya oksijeni kuingia ndani ili kuweza kuchukua ya hewa chafu, hivyo yaweza kuwa hilo tatizo.Msaada tafadhali,vifaranga wangu wameanza kufa,nakuta amelala hawezi kusimama ameishiwa Nguvu kabisa ,chakula hali na maji pia hanywi sijui tatizo itakuwa ni nini.? Naogopa tatizo lisije kuongezeka
Dah nimeziba kote kwasababu ya mvua ilikuwa ya upepo inaingiaHali ya hewa ndani ya banda iko vipi mkuu? Na msimu huu wa mvua wafugaji wengi huwa wanajisahau wanafunga madirisha yote hivyo kutukuruhusu hewa safi ya oksijeni kuingia ndani ili kuweza kuchukua ya hewa chafu, hivyo yaweza kuwa hilo tatizo.
Fanya kucheza na hali ya hewa, hakikisha kuna mzunguko mzuri wa hali ya hewa ndani ya nyumba ya kuku.
Ndio tatizo hilo, ufanye kufungua madrisha kwa juu ( acha upenyo mdogo) kuruhusu hewa safi kuingia, mambo yatakuwa vizuri tu.Dah nimeziba kote kwasababu ya mvua ilikuwa ya upepo inaingia
Asante nimeshafanya ivyo,hizi mvua za dar nazo hazitabiriki ikanibidi nizibe kote,je na usiku niache kidogo au nizibe maana vipo karibu na dirishaNdio tatizo hilo, ufanye kufungua madrisha kwa juu ( acha upenyo mdogo) kuruhusu hewa safi kuingia, mambo yatakuwa vizuri tu.
Jaribu kuacha huo upenyo masaa 24 mkuuAsante nimeshafanya ivyo,hizi mvua za dar nazo hazitabiriki ikanibidi nizibe kote,je na usiku niache kidogo au nizibe maana vipo karibu na dirisha
Jaribu kuacha huo upenyo masaa 24 mkuu
Usijali, kama uko dar wikiendi moja naweza kuja kukutembelea kuona mambo yanakwendaje.Asante,mambo yakienda vizuri nitakupa Asante iliyonona
Usijali, kama uko dar wikiendi moja naweza kuja kukutembelea kuona mambo yanakwendaje.
Yes hizo hizo mkuu.Sawa ,namba zako ndo hizi hizi
OkayYes hizo hizo mkuu.
Kingozi naona unatoa somo zuri la ujasiriamali na mimi nataka niingie kwenye uwo ufugaj. Changamoto zangu kubwa ni aina ya mbegu bora ya vifaranga vya kuku wa mayai na kampuni gani zinatowa Vinatowa mbegu boraUsijali mkuu kama vile forum hii inavyotaka , tuko hapa kubadilishana mawazo mawili matatu ili kuweza kufanikisha mifugo yetu inakua salama salimini
Kingozi naona unatoa somo zuri la ujasiriamali na mimi nataka niingie kwenye uwo ufugaj. Changamoto zangu kubwa ni aina ya mbegu bora ya vifaranga vya kuku wa mayai na kampuni gani zinatowa Vinatowa mbegu bora