Mwongozo bora na vitu vya kuzingatia katika kuanzisha kuku wa mayai

Mwongozo bora na vitu vya kuzingatia katika kuanzisha kuku wa mayai

...Na kuna mda alishawai kuniambia kuna mbegu ya vifaranga vya kuku inauwezo wa kutaga mara mbili kwa siku ni kweli kuna mbegu kama iyo na inaitwaje
Hakuna kitu kama hicho, mzunguko wa utengenezaji yai huchukua masaa 24, kwa hali hiyo ni kwamba kuku hutaga yai moja kwa siku.
 
Kwa Tanzania ni kampuni tatu tu ninazozielewa sana katika suala zima la uzalishaji wa vifaranga waliobora;

Kampuni ya kwanza ni Silverlands Tanzania inapatikana Iringa vijijini, hawa jamaa vifaranga wao wako vizuri hasa Layers ( Hyline Brown ) maana siku ya kwanza hupewa chanjo zaidi ya tatu ambazo ni Marek's, Newcastle na Gumboro (Faida ya chanjo inayotolewa kwa kuku wao ni very effective amabapo haina haja ya kurudia tena).

Pia chanjo hizo hapo juu hupewa kuku wao aina ya Sasso, maana inategemea na lengo la mfugaji ambapo anaweza kuwafuga kama kuku wa mayai au Nyama.

Mwisho wanazalisha vifaranga vya kuku wa nyama aina ya Cobb 500 ambapo pia wako vizuri hawa hupewa chanjo mbili tu ya Newcastle na Gumboro.

Tukija kwa kampuni ya pili ni Interchick limited hawa wanapatikana hapa Dar es salaam hawa jamaa pia vifaranga wako vizuri pia, wanazalisha vifaranga wa nyama, mayai na chotara ingawa chotara wao anaitwa Kuroiler aina ya TANBRO.

Kwenye suala la chanjo hawa hutoa chanjo ya Marek's pekee tofouti na Silverlands.

Tatu, kwa mahitaji ya kuku chotara aina ya Kuroiler waweza watafuta pia AKM GLITTERS hawa wako Dar es salaam maeneo ya Sinza. Hawa huzalisha Chotara pekee.

Hawa pia kwenye suala la chanjo hutoa Mareks pekee tofouti na silverlands.

NB: Epuka kununua vifaranga kwa watu binafsi maana wanawauzia uzao wa pili hadi wa tatu mwisho wa siku performance ya kuku husikia huwa below 50%

Nimemaliza.
Asante kwa ufafanuzi wako mzuri kiongoz
 
Mkuu ni aina gani nzuri ya kuku wa mayai ( layer) na Kampuni gani wanauza hao vifaranga na kwa bei Tsh ngapi?
 
Back
Top Bottom