Mwongozo: Nataka kununua pikipiki kwa mtu

issawema

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2013
Posts
776
Reaction score
643
jaman wana jamvi habarin za asubuhi,

twende kwenye mada Mimi nataka knunua pikipiki ya kutembelea kwa MTU lakini sijajua taratibu zikoje,

ikizingatiwa hii ndo mara ya kwanza kufanya biashara kama hii

msaada wenu unahitajika
je inabidi nikabidhiwe vitu gan?
ntajihakikishiaje kuwa mmliki halali wa hicho chombo?
haki zangu kisheria ntazipataje ili kunilinda na lolote ?

nakaribisha mawazo yenu wazoefu mnishauri ndugu yenu
 
Ninayo pikipiki nipm kama unahitaji

Nadhani mtoa mada ameshapata piki piki anayoitaka na yupo tayari kuinunua....alichokuwa anauliza sio ulichojibu hapa......mtajie taratibu za kununua hiyo piki piki....akiwa na maana ya document ambazo anatakiwa apewe zitakazo mhakikishia umiliki halali wa hicho chombo.....
 
Kwa jinsi msg yake ilivyo haiko specific kama kuna ambayo tayari ameipata na anataka kuinunua. Kwa hiyo kama anataka kununua kwa MTU na sio mpya dukani jibu langu litakuwa valid. Ila kama keshaipata kwa MTU anahitaji kujiridhisha tu then apewe huo muongozo.
 
Hakikisha unapewa kadi ya piki piki, kadi ya piki piki iwe na jina la anaye kuuzia piki, hakikisha mnakuwa na mkataba wa mauziano kati yenu, hakikisha piki piki hiyo ina road licence ya mwaka huu, pia hakikisha piki piki hiyo haidaiwi na tra kwa sababu usipozingatia hilo unaweza kuta piki piki inadaiwa tra kiwango sawa au nusu ya bei ya mauziano.
 
Kwani dukani sio kwa mtu?
 
ntajuaje kama inadaiwa tra na huo mkataba nmpaka mahakamani au tunaweza kuandikisha wenyewe tuu
 
Ikiwa na current road licence hiyo haina deni, pia unaweza kwenda max malipo ukataja namba ya piki piki utaambiwa una daiwa sh. Ngapi? Mkataba vizuri kupitia Mahakamani au kwa mwanasheria kwa kuwa utatumia kule tra utakapokuwa una badilisha jina la kadi ya piki piki
 
sort mkuu road licence ndo insuarence? maana ndo kitu alichonionesha
 
Road licence sio insurance wengine wanaita motor vehicle. Tembelea max malipo ujue deni
aliniambia pikipiki hasa hizi ndogo za ktembelea siku hizi hazina motor vehicle, sijui kuna ukweli gani juu ya hilo
 
Mtaani inajulikana hivyo hata mimi nilikuwa najua hivyo lkn ukienda TRA au ukiangalia max malipo itaoneshwa unadaiwa motor vehicle. Tembelea max malipo utajua nini hasa unadaiwa. Namba ya piki piki inaanza na T. au MC?
 
inaanza na T
 
inaanza na T
Kama inaanza na T nenda max malipo haraka anataka kukuingiza mjini lazima itakuwa inadaiwa. Piki piki zote zinabadilishwa kwenda MC na unapo badilisha kwenda mc toka T kama una madeni lazima uyalipe. Nenda max malipo utajua inadaiwa sh ngapi? Anakuuzia bei gani? Kama hutajali
 
sory no inaanzia na mc amesema alishabadili no bei ya kawaida sana mkuu mia nane
 
Kama inaanzia Mc chukua hata kama itakuwa na deni sio zaid ya 20000 ila hakikisha jina la kwenye kadi ni lake isije ikawa ya deal alafu ukatiwa matatani
 
Vyombo vilivyo chini ya cc1000 vilishafutiwa road license toka mwaka juz cha msingi ni kuangalia kadi halisi na kuandikishiana kwa pkpk ni MC hakuna den hapo kbs
 
Kama inaanzia Mc chukua hata kama itakuwa na deni sio zaid ya 20000 ila hakikisha jina la kwenye kadi ni lake isije ikawa ya deal alafu ukatiwa matatani
jina sio lake mkuu ni jina la aliemuuzia, ila anakadi original, vip inaweza kuleta shida ?
 
Back
Top Bottom