Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Utapata urahisi zaidi ukiwa wa thamani katika jumuiya uliyopo.
Jumuiya uliyopo inaweza kuwa ni kazini, shuleni, mtaani, kanisani au sehemu ambayo unakutana na mwanamke mara kwa mara.
Hakikisha unajulikana na watu, ongea na watu wengi kadri uwezavyo. Hili litaongeza thamani yako kama tulivyoongea jana, na kumfanya mwanamke ajisikie salama kwako. Usiwe bubu muda wote alafu ghafla ndo ukaanza kuongea na huyo mwanamke, utapata shida na atakugundua mapema na atajiweka katika ulinzi.
Pia njia hii itakusaidia kuondoa shaka na aibu ya kukataliwa.
Baada ya kuhakikisha umeongeza thamani yako, na umemuona mwanamke anayekuvutia,angalia kama anaonesha ishara za kuvutiwa na wewe pia. Kama amevutiwa na wewe, atatabasamu kila ukimuangalia, atajisogeza karibu yako au atakuangalia zaidi. Ukishaona naye amevutiwa na wewe, vaa ujasiri wako kisha fuata muongozo huu. (kama unasita cha kusema soma, “Ukizingatia Haya Hautapata Shida Kuongea Na Mwanamke”)
Mara ya kwanza mpe hi na muongee kidogo. Kisha endelea na shughuli zako. Hakikisha kabla hujasilimiana naye umeongea na wengine ili naye ajisikie ni miongoni mwa watu wanaokujua. Hivyo, atajisikia kukujua
Kadri siku zinavyozidi kwenda ongea nae zaidi, na zaidi. Pia angalia ishara za mvuto anazokupa, mwanamke ambaye anavutiwa nawe atafanya mambo yawe rahisi na ataongea zaidi yako. Mfanye acheke pia.
Mada mnazoongea hakikisha unaziongoza wewe. Msiongelee mada zinazoumiza, au siasa au hali ya hewa. Kwa mada nzuri zaidi soma “Mada 4 Za Kuongea Na Mwanamke Ili Kujuana Zaidi”.
Pia mazungumzo yenu yawe na ukomo, sio unamganda mwanamke mpaka anakuzoea. Muda mwingine kata mazungumzo hata kama unaona mabo yanaenda vizuri. Usiwe na shaka kesho nayo ipo.
Kwenye kuongea kwenu mchombeze taratibu. Usijiweke kama rafiki, wala kuomba urafiki na uikatae hiyo hali. Tengeneza mahusiano ya mme na mke, jiwekee kichwani kwako kwamba tayari umempata. Mguse sehemu kama bega au mkono (mkiwa vizuri kiunoni na mapajani), mchombeze, mtanie, usimuweke juu yako, na pia usiogope kumwambia pale anapovuka mstari wa misimamo yako.
Usimwambie unampenda mapema au kuanza kumuomba awe mpenzi wako. Wanawake wanapenda ile hali ya kujuana kwanza na kuacha mapenzi yakue yenyewe bila kulazimishana. Ndio maana wanaume wengi wanaishia kuomba omba jibu la swali “nakupenda” na kuhama mtaa wakikataliwa. Usimrahisishie mwanamke kazi kiasi hiko, acha na yeye apambanie hiyo ‘nakupenda’. Acha ajithibitishe kuwa anastahili. Nakazia tena usimrahisishie iyo kazi maana ye mwenyewe anataka kulipambania ilo pendo ukimrahisishia anakua hana cha kupambania na utaishia kuomba jibu la swali “nakupenda”.
Ila msifie hapa na pale, mwambie kinachokuvutia kwake. Muite majina mazuri ya mapenzi. Na usizidishe sifa.
Muhimu: Unapomwambia kinachokuvutia kwake, usikae kusubiri jibu. We mwambie kisha badilisha mada kama vile hujamwambia kitu.
Baada ya muda mualike kwenda naye beach au sehemu yoyote ya kufurahia. Kumualika sio kumuomba, pia usilazimishe we nenda naye taratibu. Pia kama bado unaona hajiachii mwambie kuwa mnaenda na marafiki zako na yeye anaweza kujiunga na unaweza mtania “sijui kama we ni mtu wa kwenda sehemu za kufurahi”, atajielezea utapata jibu. Ukiwa naye uko wewe ndo uwe mwenyeji wake pia mtenge mara kwa mara mpate muda wenu pamoja.
Anza kumkiss. Ukiona mambo yanaenda vizuri usisite kuangusha upendo kwenye lipsi zake. Ndio maana ni muhimu kumtenga na kuwa naye pamoja. Ila usimkiss mbele ya watu anaowajua, hatojisikia amani na kujiachia.
Ila kama unaona mnaelewana vizuri mualike kwako moja kwa moja. Mualike kwa sababu, mfano, mwambie hujawahi fungwa goli zaidi ya tatu kwenye karata na umualike kucheza naye, au kama una vinywaji kwenye friji, mualike kunywa vinywaji. Yaani mualike mfanye kitu kwa pamoja. Ukiwa naye kwako usiwe na pupa, nenda naye taratibu na msogeleane kadri muda unavyoenda na uweke kiss kwenye lipsi zake kisha …
Usilazimishe penzi kama amekataa. Pia usioneshe kuumia kwa kuwa amekataa, we potezea na muendelee kufurahi. Nenda taratibu mpe nafasi naye ya kujiachia kwako.
Ukikwama sehemu rudi nyuma hatua kadhaa hadi sehemu ambayo unaona ndo mara ya mwisho kuwa naye vizuri na uanzie hapo tena. Yote hayo ni kwasababu ya utofauti wa kasi ya kupenda kati ya mwanamke na mwanaume, soma “Mwanaume, Fanya Hivi Ukishajua Tofauti Ya Kupenda Kati Ya Mwanaume Na Mwanamke” uelewe zaidi.